Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya kijamii

Rais Magufuli azidi kuiandama mitandao ya kijamii

Kaenda kutibiwa kwa niaba ya raisi na kwa niaba ya inji, inji inaumwa hii na rahisi ni ngonjwa ile,

Akipona na inji&rahisi kapona, tutarejea kwenye mstari mnyoofu kama tahifa
 
Magufuli anaita mitandao ya hovyo wakati anagombea matangazo yake yalijaa kwenye mitandao hii, au imekuwa ya hovyo baada ya yeye kuwa raisi?

Nitaanza kumsikiliza pale atakapo mwondoa mwizi wa elimu bwa Daudi, kinyume na hila hana uhalali wa kuwanyoshea vidole watu wengine.
 
147a9f0bc85aa9172a3966b63a537cbc.jpg
 
Tafadhalini sana mods naomba msiunganishe uzi huu, kufanya hivyo ni kubinya Tafakuri za kina.

[HASHTAG]#HATUPANGIANI[/HASHTAG].

Rais anasema "mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi" amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.

Tujiulize: Hivi ni nani asiyejua madhara ya migogoro kati ya wafugaji na wakulima?, je kuna hatua gani za kudumu zilizowahi kuchukuliwa kutatua suala hili? Je media zifumbie macho jambo hili?, Media kufumbia macho suala hili na maovu/mabaya mengine ni sawa na kuwasaliti wafugaji na wakulima au kuona mauaji yanayoendelea baina yao si kitu, labda kwa sababu ndugu yako hajawa sehemu ya mgogoro huo. Ni lazima media ziseme juu ya uovu wowote ule ili hatua stahiki zichukuliwe. Unachotakiwa kujua Mh. Ni kwamba siku zote ukweli huwa hauwapendezi watu wengi kwa sababu unafichua/unaanika madhaifu yao. Kama migogoro ipo ni lazima isemwe sana ili hatua stahiki zichukuliwe mapema sehemu husika.
Njia pekee itakayofanya USISIKIE habari hizi ni serikali yako kuwa na suluhisho la kudumu juu ya migogoro/habari mbaya zinazo ripotiwa. Suala kama bado ni bovu lazima li ripotiwe.

Hatuwezi kusoma habari ya daraja la kigamboni mwezi mzima kwa sababu tayari limekwisha kamilika, ila ikitokea likapata udhaifu/itilafu wa/ya aina fulani ni lazima udhaifu huo utasemwa sana mpaka pale hatua madhubuti zitakapo chukuliwa.

Raisi ameshangaa "magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo", well, Mh. Kwa suala kama hilo sisi tumeshangaa tofauti kidogo na wewe, sisi tumeshangaa pale ambapo siku moja baada ya waziri uliyempatia dhamana, kutoa ripoti ambayo moja kwa moja imemgusa 'mteule wako' kufanya jambo lisilo la kiungwana na lililoshuhudiwa na mamilioni ya watanzania, Mh. badala ya kutizama kwa umakini ama kusikiliza pande zote mbili, au ku balance yaliyosemwa kwenye ripoti na hali halisi ilivyo, moja kwa moja umemtumbua waziri kwa kuleta aina ya habari/ripoti usizopenda kusikia. Hili suala ni la kushangaza

Rai Yangu: Mh. Nikueleze tu tazama kwa makini sana wanaokusifia kwa kila jambo. Najua unajua kila kitu lakini HAUJUI kilichomo ndani ya maoyo yao. Inawezekana una nia nzuri sana kwa Taifa hili, lakini hata wanaokosoa wana nia nzuri pia. WASIKILIZE FANYIA KAZI MAPUNGUFU.

Wako mtiifu a.k.a KIRAKAPACHA.
 
Akiongea leo wakati anaapisha wateule wapya Ikulu. Amesema mitandao yetu ni ya ovyoovyo na inaandika mambo ya ajabu ajabu.

"Jana nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa eti Mwakyembe hawezi kuja kuapishwa, na mimi nilikuwa nasubiri asifike nione. ''Sasa si huyu hapa amefika"

Ameongeza kuwa..... "Jana kuna mwingine kapost Kinana kuongea na waandishi wa habari kesho, wakati ukweli Kinana nimemtuma India Kwa siku kumi na mbili"

Amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari kwa kuzipa nafasi habari mbaya mbaya tu, "mfano kuna tv habari za migogoro ya wafugaji ndio wanaipa nafasi kubwa zaidi, amesema hayupo tayari kuvumilia hayo mambo.

Ameshangaa magazeti ya leo kujaza mbele picha ya mtu mmoja, na hata kurasa za ndani kujaza habari hiyo hiyo.

Amemwambia Mwakyembe akasimamie kwa umakini hasa tasnia ya habari, amesema hayupo tayari kuona nchi ikichezewa..l

Ameshangaa kutangaza kutoandika habari za mtu, wakati huo huo wanaandika mbaya tu.... "Kama hamtaki kumwandika si masiandike yote mazuri na mabaya"


Hiyo Mikopo ya World Bank Atakuja Kuilipa Kwa kuuza Sangara au Urithi wa Pesa za Babaake au Zitalipwa na Kodi za Watanzania? Na inawezekana pia Amekubaliwa Mikopo hiyo kwa kuwa anataka sifa za haraka haraka, hakujali Masharti na Riba ya Mikopo hiyo au Ameweka Gas na Mafuta yetu rehani? Kuna Kitu tutafatilia hapa.
 
that where we go wrong, we take words from unreliable sources and claim they are from Mr president. ndio maana sihamini mitandao na watu wake wajinga wa akili
 
Back
Top Bottom