Rais Magufuli awateua Abdallah Bulembo na Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Wabunge

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhmi ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuii ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.

Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamaganiba John Aidan Mwaluko Kabudi. Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi. Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa baadaye.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,
IKULU
Dar es Salaam
16 Januari, 2017


6e6b614751483d8f55be746188b7379d.jpg
 
Kuna umuhimu kama sio ulazima wa kupigana kufa au kupona ili kupata PhD hivi sasa hata kama ni ya online...!! Unatafuta PhD sio tena kwa ajili ya kuwa academician ili hatimae usaaidie taifa kwenye elimu bali unasaka PhD ili kulia mingo teuzi za Mheshimiwa Sana!
 
Tangu kwenye Bunge Maalum la Katiba, nilishamuona kabisa Professor Kabudi anatafuta nafasinya kuingia Bungeni. Hongera Mwalimu wa Sheria Kuingia Bungeni.

Lakini naanza kupuuzia kabisa watu wanaoitwa Prof hapa Bongo. Alianza Prof Limaharage, sasa huyu naye kajilelengesha......

Vipi nafasi yake kama Mwenyekiti wa Bodi ya TIB? Ataendelea kuikamatia kama kawaida?
 
Kabudi mwanasheria wa kanisa la Anglican kwa askofu mokiwa na mshauri Mkuu wa sheria wa bwana yule.

Nadhani mwakyembe atapisha njia pale wizara ya sheria NA muda si mrefu mabadiliko ya Baraza la mawaziri yanakuja.

Kwa kuwa bwana yule pia watu wa madini na nishati wanamtikisa,anaweza pia kumuweka kabudi.

Pia anaweza kumwacha kabudi achuane na tundu lissu japo navyojua kabudi atataka uwaziri kwa kuwa huwa hakubali nafasi za chini.

Kabudi pia anaweza kuwekwa ofisi ya makamu wa rais mazingira na kumuondoa January makamba,ambae nadhani hayuko comfortable sana NA hii awamu,kabudi ni mtaalamu wa environmental laws na kwa kuwa masuala ya muungano ni ya kisheria zaidi NA kabudi ni mwanasheria

Nahisi nape atampisha bulembo
 
Back
Top Bottom