leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,585
- 3,179
Rais Magufuli akiomba pamoja na Mzee Kazimoto na wanafamilia.
Mzee huyu wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyaka Bugene alikuwa ni miongoni mwa watu ambao nyumba zao zilipaswa kuvunjwa ili mradi uweze kutekelezwa, Mzee Kazimoto alipinga ubomoaji huo ndipo walipokutana na Rais Magufuli wakati huo akiwa waziri wa ujenzi.
Ubomoaji ulifanyika chini ya usimamizi wa waziri kipindi hicho na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kipindi hicho lakini baadae mzee huyo alikuja kubaini nia nzuri ya Serikali kuhusiana na maendeleo na hivi sasa ni marafiki.
Rais Magufuli abaini kuugua kwa mzee huyo baada ya kuuliza uwepo wake kwenye ufunguzi wa barabara hiyo,na baadae kupata taarifa kuwa mzee huyo ni mgonjwa na kuamua kwenda kumjulia hali.
Maendeleo hayana adui asante rais kulitambua hilo.