Rais Magufuli avunja Katiba?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,565
Reaction score
27,564
Marufuku ya kupiga siasa iliyotolewa na Rais Magufuli kwa wanasiasa wapinzani wake huku Chakubanga ,Bi Tukinao, Professa wa Jalalani, Bashiru, Shaka na wengine wakizunguka nchi nzima kufanya siasa, tena wengin wakiwa si wabunge wa majimbo ni uvunjwaji wa katiba, na kama ndiyo ama siyo Je Msajili wa Vyama Vya Siasa Alishindwa kukemea Tamko lisilo halali?

Kama anafikiri Wapinzani ndio wanamzui kufanya afanyayo, si apitishe sheria ya kuvifuta vyama, siku akichoka maana jana kasema hawezi mwachia mtu, avirudishe?

Je, kufuta vyama ndio kamfuta Nappe, Makamba, Mwigulu[Mwigulu ni mpinzani wake mkuu anayecheza kwa step], Mahiga, na wengine wengi?


Unatambua wazi kuwa rais alivunja katiba na sheria za nchi kutangaza marufuku ya vyama vya siasa kufanya shughuli za kisiasa, hili kama Prof msomi ulitakiwa kumshauri rais kwamba anavunja katiba.

Hakukuwa na sababu za amri hiyo ya kirais katika nchi ya kidemokrasia inayofuata mfumo wa vyama vingi, isipokuwa tu kunapokuwa na vita katika nchi au hatari yoyote inayoweza kupimwa kwa Def Cond walau 001 hivi. Kitendo cha wewe kushindwa kumshauri rais vizuri juu ya hili, kiliondoa uhalali wako katika taifa juu ya mapambano yako ya miaka mingi kuhusu Demokrasia, yaani taifa halijanufaika juu yako katika hili kwa mtu uliyepigania demokrasia kwa miaka zaidi ya 30.

Rais akasema Wabunge tu wakuchaguliwa na madiwani ndio wafanye mikutano yao. Zingatia Mkutano wa kibunge sio wa chama cha siasa, ni mkutano wa kiutumishi. Hivyo John Heche hajafanya mkutano wa Chadema, amefanya mkutano wa Kibunge. Hili usipotofautisha utakuwa huna tofauti na akina Chakubanga tu.

Bashiru, Polepole, Pinda na makada wa ccm wengine nchi nzima wanazungunga nchi nzima wanafanya mikutano ya hadhara ya ccm huku wao sio wabunge wala sio watumishi wa umma bali wanaccm. Wakati huo Mbowe ambae ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa au Mashinji ambae ni Katibu Mkuu wa Chadema hawaruhusiwi kufanya mkutano wa hadhara Dar au popote na hata jimboni kwa Mbowa anazuiwa na polisi.

Tumia taaluma yako kulisaidia taifa kuliko kujali maslahi binafsi huku taifa likiangamia kwa ubaguzi nakulijaza chuki za kisiasa zisizo na ulazima.

Na Yericko Nyerere
 
Mbona mbowe yupo hai anaunguruma huko?
 
Wanaogopa wakiachia amsha amsha la upinzani si la kitoto
 
Yericko; Leo umeamka mapema, huenda bado una usingizi kwa sababu:-
1. Inaelekea unazungumza na mtu, lakini hajajijua nasi pia hatujamjua.
2. Uandishi huu sio wa kwako na huenda kuna mtu kahack.
Z
 
Hizi za rais Magufuli kukiuka katiba sasa ni kelele. Rais wa Tanzania ana uwezo kufanya chochote, popote na kwa yeyote kwa mujibu wa katiba.

Kwa muudo wa katiba yetu, kwenye freedom of expression kila mtu yuko huru kusema chochote popote alimradi hajavunja sheria ikiwemo kumuita rais dikiteta na kusema amevunja katiba, lakini mamlaka pekee yenye uwezo wa kutamka kama rais amekiuka katiba ni Mahakama au Bunge, no one else!.

Hivyo tuendelee tuu kusema sema tuu chochote na kupiga kelele tena tunaweza kupaza sauti hadi mbinguni, as long as hakuna matendo, then kelele hizi ni bure tuu, hazisaidii kitu, na sana sana...
P
 
Sheria za vyama vya Siasa inaruhusu mikutano ,haijaweka ukomo kwenye jimbo, no one is above the law, never, brother Mayalla unajiongoza vibaya, never.
Pili, Katiba inatambua uwepo wa upinzania na lengo la kupinga si kukuunga mkono na maendeleeo yako, ni kukutoa ulipo, that means lengo la CUF, TLP, ACT, JAHAZI ASILIA, NLD na CHADEMA ni kuitoa CCM MADARAKANI na si kuisifia.

Kwako, personally utaona ni kelele kwakuwa hata LIBYA , MISRI, SUDAN walisema ni kelele lakini zikawa kelele kweli kweli, okay time will tell, hi ni nchi ya wanyonge, wakishiba huenda wakapata uwezo wa kufikiri, najua mnyinge hawezi kufikiri aidi ya njaa zake, hana innovation, anawaza njaa yake ya mda huo tu
 
Mkuu Jaji Mfawidhi, kuna hoja za kisiasa na matatizo ya kisiasa na mitanzuko ya kisiasa, zinatatuliwa kwa suluhisho la kisiasa ikkwemo kufanya majadiliano na kupiga kelele as pressure group.

Hoja za kisheria na matatizo ya kisheria yanatatuliwa kwa ufumbuzi wa kisheria na sio kisiasa iliwemo kupiga kelele.

Zuio la mikutano ya kisiasa japo limetolewa kisiasa, ni tatizo la kikatiba na kisheria, linahitaji ufumbuzi wa kisheria na sio kelele za kisiasa.

Angalia majibu yangu kwa hoja za Lissu na Zitto

P
 

Kuna kesi za Kikatiba na hukumu zinaelekeza kuwa vifungu fulani ni uncostitutional na pia tamko fulani halifai, SERIKALI HAITEKELEZI.
Sasa anayekataa kutekeleza ndiye haeshimu mhimili mwengine, mahakama haiwezi kutoka kwenda kuikamata serikali.
Hata adhabu ya kifo, imetamkwa kwenye hukumu kuwa unconstitutional na iondolewe lakini ip0.

Tukubaliane, kuna muhimili mmoja umejitunisha sana na kujionyesha kuwa juu kuliko mingine
 
Ile siku ulipopata nafasi ya kumuuliza maswali Rais, yale maswali yanafanana fanana na thread hii. Lakini, nina amini kuwa, ukipata tena nafasi kama ile, sidhani kama utaweza kuuliza maswali KIGONGO kama yale!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…