Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa familia 12 zilizopoteza watu ajali ya city boy

Kazi Mkuu

Member
May 24, 2017
21
100
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, nawapa pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa.

“Aidha, nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na Mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani?”

Ni sehemu ya salamu za rambirambi na maelekezo aliyoyatoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Aprili, 2018 kufuatia ajali iliyotokea katika Kijiji cha Makomero, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora jana tarehe 04 Aprili, 2018 saa 2:00 usiku na kusababisha vifo vya watu 12.

Ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa na kutoa maelekezo hayo, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.

Aidha Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na majeruhi wote 46 wapone haraka ili waungane na familia zao katika ujenzi wa Taifa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

05 Aprili, 2018

Habari zaidi soma=>Ajali Igunga, Tabora: Basi la City Boy limegongana na Fuso. Vifo kadhaa vyatokea...
20180405_125620.jpg
 
Rais amewaombea wapumzishwe mahali pema peponi.
Hayo ndio mambo bana
Heko sana mh rais kujali raia wako
 
Ili kupunguza ajali za kugongana uso kwa uso, bara bara zote tunazojenga sasa ziwe na buffer zone yenye kadiri ya mita moja na nusu.
Yani mfano mzuri ni barabara ya kutoka Ubungo mataa to Mwenge.
Bara bara inapojengwa ile ya kushoto na ya kulia inaatenganishwa kati kati kwa eneo la udongo wazi ila inakuwa inakutana kwenye eneo lililonyooka ili kuruhusu magari kuweza ku overtake.
Sehemu ambazo hazieleweki eleweki ziwe na utenganisho baina ya upande wa kushoto na wa kulia upatao upana wa mita moja na nusu. Hii itapunguza sana ajali za kugongana uso kwa uso hasa zile zinazosababishwa na ku over take.

Tunaweza kuanza hili tukiwa tunajenga bara bara mpya ya Moro-Dodoma. Ile ya sasa iachwe katikati alafu wajenge mpya ya kwenda upande wa kushoto na mpya ya kurudi upande wa kulia kaisi kwamba magari ya huku na kule yanakuwa hayapishani kwa ukaribu. Hii ya sasa ya zamani inaachwa katikati kama buffer zone itakayotumika sana sana kwa ajili ya ku over take!

Buffer zone.png
 
Rais Magufuli amempa pole mkuu wa mkoa wa Tabora kufuatia ajali mbaya ya basi iliyopoteza maisha ya raia wema 12. Kufuatia ajali hiyo Rais Magufuli amelitaka jeshi la polisi kujipima kufuatia kuongezeka kwa ajali zinazosababishwa na uzembe wa madereva. Source ITV habari!
 
Kamwambie barabara ambazo alikuwa anazisimamia kipindi kile akiwa waziri wa ujenzi zote ni mbovu zina mashimo kama tenga
 
haya ndiyo mambo ambayo wanasiasa wanahitajika kutumia platforms zao kuyapigania but unfortunately wamewekeza kwenye porojo
 
Back
Top Bottom