Rais Magufuli atinga benki ya CRDB leo asubuhi, azua taharuki

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
800
RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya "Adamu na Hawa" wala bendera ya Rais.

Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora, bila kutarajiwa.

Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya barabara hizo yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo.

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia.

Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.

Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
20160418103453 (2).jpg

1461000831556.jpg
1461000847496.jpg
 
Habari wanajamvi?
Hii habari nimeipata kwa grup la whatsapp... kama ni kweli aisee wanausalama wanakazi kubwa.
RAIS John Magufuli amezua mjadala baada ya kuvamia tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya "Adamu na Hawa" wala bendera ya Rais.

Tukio hilo lililochukuwa dakika 25, limetokea majira ya asubuhi jijijni Dar es Salaam katika tawi hilo ambalo liko katika makutano ya barabara za Ohio na Samora, bila kutarajiwa.

Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo, makutano ya barabara hizo yalifungwa ndipo Rais aliposhuka kwenye gari na kuingia ndani ya benki hiyo.

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliyokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyoi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliyokwishaingia.

Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa sitaili ile. Baadhi ya wananchi walisema hawajaona tukio kama lile kwa Marais wote waliyopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa taxi, alisema baadhi ya wananchi waliyokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimarishwa walishituka na mara wakamuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari, hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB, tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja? Hata hivyo tujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu. Haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule. Ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,”alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma. Kwa ujumla kila mmoja wetu alishituka lakini hatukujua kilichomleta,” alisema.

Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.View attachment 340113View attachment 340114

Ni kwamba wewe na watu wengine ndiyo mlikuwa hamjui, lkn vyombo vya usalama vyote vilikuwa vinafahamu hata wiki kabla na walikuwemo humo ndani ya Benki, usifikiri ni kwamba kaibuka tu Ikulu na kuamua kwenda hapo Benki!
 
Tatizo ni nini, kwa hapa Tanzania kuna shida gani wadhani? To me is Ok, kwa nchi ya amani kama hii. Sanasana watamshangilia!!
Ndugu yangu... unajua rais anawasaidizi wangapi?kweli rais si swala la kupiga simu tu au kutuma memo na taarifa zinamfikia?
To me it is too december
 
Kiranga Nyani Ngabu

sijui hata niseme nini kwa hili

Acha unafiki wewe! Angekuwa Obama kafanya hivyo hapo ungetafuta sababu 200 za kumtetea lkn kwa kuwa kafanya raisi mweusi wa Kiafrika unataka kuleta ligi, kwani mara ngapi tunaona Obama anakwenda kununua burger mc donald na anapanga foleni kulipa? Au raisi wa Ulaya akienda kazini na Baiskeli au kupanda treni kwenda kazini??? Mbona huwa hamshangai???

Acheni kufanya maisha ya Mwafrika yawe magumu bila ya sababu! Hii yote ni sehemu ya siasa kama wewe haijakuvutia kuna Watz mamilioni ambao watapendezwa na jambo la kumuona Raisi wao akienda benki yao kuchukuwa fedha kama wao wafanyavyo kila siku, ni sehemu ya Uongozi!
 
Back
Top Bottom