Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti Bodi Benki ya TIB Prof. Lyakurwa na Kumteua Prof. Kabudi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.

Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Mhe. Rais amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:

Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
Dkt. Razack B. Lokina
Bi. Rose Aiko
Prof. Joseph Bwechweshaija
Bw. Said Seif Mzee
Dkt. Arnold M. Kihaule
Bw. Maduka Paul Kessy
Bw. Charles Singili


Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.

Cml5FVxXYAA1EEX.jpg:large
 
Uyu profesa ni mwenyekiti pia pride Tanzania,kwaiyo mwenyekiti zaidi ya nafasi moja?
 
Rais John Pombe Joseph Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa na kumteua Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi kwa muda wa miaka mitatu.

Cml0iUAWEAAtzBQ.jpg





Cml2AGEWYAAvnij.jpg:large
Hivi jamani naomba kuuliza kwani mheshimiwa rais huwa hana watu wa kumshauri kabla ya kufanya hizo teuzi?
 
Atumbue tu ila mtaani watu hawamuelewi.

Hii single ya utumbuaji majipu imeshachuja!
Naona ule utaratibu wa kumfuatilia mtu tabia na mienendo yake kiutendaji kabla ya kumkabidhi nafasi husika alikufa nayo baba wa taifa jk nyerere
 
Back
Top Bottom