Rais Magufuli atengua na kusamehe baada ya sala

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
Rais John Pombe Magufuli amemtengua na baadaye kumsamehe mkuu wa polisi wilaya ya Njombe kutokana na mauaji ya watoto yaliyotokea miezi miwili iliyopita mkoani Njombe na kusababisha doa kubwa Nchini na nje ya Tanzania.

Rais Magufuli ametoa uamuzi huo mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi mkoani humo katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe.

“Hata hili swala la mauaji lilitokea hapa halikutakiwa lichukue mda mrefu hivyo,ndio maana RPC wa hapa nimemtoa wala msitafute sababu nyingine nimemtoa kwasababu alishindwa kusimamia hii kazi,ninataka mambo yawe yanatendeka haraka wewe mtu anapotea mtoto wa kwanza anapotea wa pili mpaka wanafika saba haiwezekani na OCD wa hapa bado yupo naye aondoke najua yuko hapa ananilinda naye sio OCD hapa ni lazima watu wawajibike kila maeneo yao watoto saba wanapote mpaka tunaleta polisi wakina Sabas mkoa wa njombe umepata doa kubwa”alisema Magufuli

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa endapo yatatokea mauaji hayo kwa mara nyingine mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine watawajibishwa.

“Siku nyingine yakitokea ya namna hiyo Mkuu wa mkoa unaondoka, Dc unaondoka, DAS unaondoka katibu tarafa unaondoka mpaka mwenyekiti wa kijiji ikiwezekana na katibu wa CCM wote wanaondoka ili kusudi tufike mahali wote tunachukua hatua mapema,wakina mama waliopotelewa na watoto wao wameumia lakini nitoe wito kwa ndugu zangu huwezi kutajirika kwa kutoa mtoto”aliongeza Magufuli

Hata hivyo Rais Magufuli aliomba mchungaji yeyote kuongoza Toba kwa mkutano huo huku naye akishiriki toba na kuamua kumsamehe OCD huyo.

“Asante sana mchungaji kwa toba na huyo OCD nimemsamehe kutokana na maombi haya abaki hapa hapa naomba RPC umwambie nimemsamehe kutokana na maombi haya naomba asitoke mtu mwingine kufanya mabaya na kila mwananjombe akafanya kazi”alisema Rais Magufuli

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka aliomba radhi kwa niaba ya wananchi huku akimueleza Rais wale wote waliohusika na mauaji ya watoto wamekwishafikishwa mahakamani

“Mheshimiwa Rais ulinipa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama tumeshirikiana nao na hivyo mimi kwa niaba ya wananchi wote wa mkoa wa Njombe nakuomba radhi kutokana na vifo vya watoto saba bila sababu ya msingi lakini tumesimamia kwa nguvu na wote waliohusika kwa sasa wapo mahakamani”alisema Olesendeka

Katika hatua nyingine Magufuli amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Njombe rambi rambi kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya familia zilizokumbwa na matatizo hayo.
 
Atuambie Azory gwanda Yuko wapi? Nani alituma watu wamuue Lissu ambapo mpaka leo yeye anafurahia?Kama anauchungu mbona hatengui uteuzi wa RPC Dodoma mwenye sura mbovu Kama maiti ya msudani....Pathetic
 
Dua za wanyonge zinaanza fanya.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Wakati mwingine NYUMBU mkikosaga swaga huwa mnatukana tu. Kwani sema na makengeza ya DJ bro
Makengeza unayajua wewe Mimi nilichokitaka atuoneshe mauaji anayoyafanya huku mashoga Kama nyinyi mkiendelea kumsifia au huwa anawagonga nini maana ajali haziishi kwenye Akili zenu mnawaza Kama majitu ya kuzimu vile
 
Kichaaa kimepamba moto, mpunzisheni Magufuli2020. Nchi yetu ipo katika fedheha na aibu kwa kweli.
 
Back
Top Bottom