Rais Magufuli atembelea TBC. Mkataba wake na Startimes kuchunguzwa, Wafanyakazi kulipwa Malimbikizo

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,772
23,003
Habari wakuu..

Leo Mh Rais ana ziara ya KUSHTUKIZA kulitembelea shirika la habari la taifa nchini TBC..

Tuwe pamoja kujuzana na kutabiri kile ambacho kitajiri leo ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kila wakati juu ya utendaji mzima wa shirika hili nchini ambalo limekuwa likiendeshwa na kodi zetu!

Stay tuned!
---------

Updates..

MaguTbc].jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) yaliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa ambaye hakutaka jina lake kutajwa alieleza kuwa, Rais Magufuli aliwasili kituoni hapo majira ya saa 5 asubuhi, na miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusikiliza changamoto zinazowakumba wafanyakazi wa shirika hilo.

maguryoba.jpg

magutbc1.jpg

tbcmagu.jpg


=======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Mei, 2017 amefanya ziara katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo amekagua miundombinu ya shirika hilo na kuzungumza na wafanyakazi.

Mhe. Rais Magufuli amejionea jinsi miundombinu ya shirika hilo inavyokabiliwa na changamoto mbalimbali za uchakavu na teknolojia duni na amesema Serikali itafanyia kazi changamoto hizo ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya ya studio za kisasa za kurushia matangazo katika makao makuu ya nchi Mjini Dodoma.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Magufuli ambaye hivi karibuni ametoa Shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya kuisaidia TBC amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Ayub Rioba kutumia fedha hizo kutatua matatizo ya uhaba na uchakavu wa vifaa vya uzalishaji wa vipindi na urushaji wa matangazo, kununua vyombo vya usafiri na kufanya ukarabati wa majengo.

Kuhusu maslahi ya wafanyakazi amewahakikishia kuwa Serikali itaboresha stahili zao kwa mujibu wa utaratibu uliopo na papohapo amemuagiza Dkt. Rioba kulipa mara moja malimbikizo ya posho zote ambazo wafanyakazi hao wanadai kuanzia Mwezi Oktoba 2016, zilizofikia shilingi Bilioni 1 na milioni 285.

Mhe. Rais Magufuli ametaka wafanyakazi wa TBC kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na ubunifu wa hali ya juu ili matangazo ya chombo hicho cha Taifa yawavutie Watanzania wengi, na kiwe chombo kinachoongoza nchini.

“Msemaji wa Serikali mkubwa ni TBC1 na Redio ya Taifa, nyinyi hamuwezi mkawa kama vyombo vingine ambavyo vina malengo yao ya kufanya biashara, nyinyi kazi yenu ni kutoa taarifa sahihi kwa Watanzania bila kubagua vyama vyao, bila kubagua dini zao, bila kubagua makabila yao, huo ndio uwe msimamo mkuu.

“Mmetoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa hili, hilo ni lazima niseme, hata vipindi vyenu ukiviangalia ni vizuri vinaeleza mpaka maisha ya vijijini, na mimi ni shabiki mkubwa sana wa TBC, lakini tatizo lenu mnashindwa kwenda na wakati wa sasa” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe aliyekuwepo katika ziara hiyo kuuangalia Mkataba kati ya TBC na Star Times na kuchukua hatua zinazostahili endapo itabainika kuwa mkataba huo hauna manufaa.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bw. Tao Zhang na kuishukuru IMF kwa kuendelea kuwa wadau wa maendeleo wa Tanzania.

Mhe. Rais Magufuli amemueleza Bw. Tao Zhang kuwa Tanzania inatekeleza mpango wa pili wa maendeleo utakaoiwezesha kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na hivyo ameiomba IMF kushirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu, uwekezaji katika viwanda na kuwahamasisha wadau wengine kuwekeza hapa nchini.

Kwa upande wake Bw. Tao Zhang amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kusimamia uchumi wa Tanzania na amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kukua vizuri tangu miaka 20 iliyopita ukichagizwa na uwepo wa sera nzuri na mipango imara ya mageuzi, na kwamba anaamini kuwa uongozi mzuri wa Mhe. Rais Magufuli akishirikiana na wadau wa maendeleo wataendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoukumba uchumi duniani.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

16 Mei, 2017
9a9beefa964533e6d4966cb671ba76d0.jpg
fe8f3d227c1f604dfcdfde64da09cf69.jpg
 
Wafukuzwe wote na watangazaji wote Ili iundwe upya, haiwezekani wanashindwa kutuletea vitu vya maana kama timu yetu ya Serengeti badala yake wamekalia taarabu na chereko chereko. Kama haiwezekani basi ni bora hili shirika livunjwe tu tujue hatuna Tv ya Taifa.
 
Habari wakuu..

Leo Mh Rais ana ziara ya KUSHTUKIZA kulitembelea shirika la habari la taifa nchini TBC..

Tuwe pamoja kujuzana na kutabiri kile ambacho kitajiri leo ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kila wakati juu ya utendaji mzima wa shirika hili nchini ambalo limekuwa likiendeshwa na kodi zetu!

Stay tuned!!
Mbona unataarifa? Mna km anaenda kushtukiza t means hakuna anaejua hyo itakua ziara ya kawaida tu
 
Habari wakuu..

Leo Mh Rais ana ziara ya KUSHTUKIZA kulitembelea shirika la habari la taifa nchini TBC..

Tuwe pamoja kujuzana na kutabiri kile ambacho kitajiri leo ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kila wakati juu ya utendaji mzima wa shirika hili nchini ambalo limekuwa likiendeshwa na kodi zetu!

Stay tuned!!
ya kushitukiza kivipi wakati wewe ushatapakaza maneno humu? uongo
 
TBC imepoteza muelekeo kabisa wa kila kitu Raisi wetu akiangalie hiki chombo kwa upande mwingine tena ,,,,,,ngoja tusubirii atamtumbua nani leo??
 
Habari wakuu..

Leo Mh Rais ana ziara ya KUSHTUKIZA kulitembelea shirika la habari la taifa nchini TBC..

Tuwe pamoja kujuzana na kutabiri kile ambacho kitajiri leo ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kila wakati juu ya utendaji mzima wa shirika hili nchini ambalo limekuwa likiendeshwa na kodi zetu!

Stay tuned!!
Kama unataarifa ya hiyo ziara na umeileta hadi huku JF hiyo sio ziara ya kushtukiza tena.
 
Back
Top Bottom