maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Baada ya kumalizika kile kizazi cha viongozi wazalendo wa Afrika akina Kwame Nkrumah, Julias Nyerere, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba, William Tolbert, Sekou Toure, Leopold Sengho, Gamal Abdel Nasser, Tafewa Balewa, Siaka Stevens, Haphoet Boigny, Keneth Kaunda n.k waliolipigania bara la Afrika kwa damu, jasho na mali ili waafrika wawe huru, bara la Afrika liliingia kwenye giza la machafuko na vita.
Kilifuata kizazi cha vijana na wanajeshi wakorofi akina Fredy Akufo, Mengistu Haile-Mariam, Iddi Amin, Mobutu Sese seko, Siad Barre, Hissene Habre, Jaafar Nimeiry, n.k ambacho hakikufanya lolote la maana katika tawala zao za mabavu mbali na wizi na kujilimbikizia mali na raslimali za nchi zao baada ya kuzipindua serikali za watangulizi wao.
Katika zama hizi naanza kukiona kizazi kipya cha kizalendo kitakachofufuka na kuibuka katika bara letu kikiiga na kufuata nyayo za Rais wetu John Pombe Magufuli.
Ninaamini katika siku za usoni vikao vya Umoja wa Afrika vitapata changamoto mpya, vitakuwa vya mijadala mikali itakayokuwa ikiongozwa ama na Magufuli au wajumbe kutoka Tanzania. AU inaweza kupata starring.
Namwona Magufuli kama kiongozi shupavu atakayekuwa na uthubutu wa kuwaambia wenzie kwamba kujadili kujitoa kwa nchi za kiafrika kutoka mahakama ya kimataifa ICC kunafanywa kwa nia ovu hakuna faida. Atakuwa akiwapasulia viongozi wenzie ukweli ulio mchungu. Hatawaogopa, subirini tutayaona.
Tatizo ni kwamba ujumbe wa Tanzania hautakuwa ukiongozwa na vijana machachari na wajuzi wa kujenga hoja kwenye mikutano ya kimataifa, watakuwa wanachaguana wazee wa saizi ya Mahiga.