Rais Magufuli ashiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha Sokoine

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575

Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akimaliza kuweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo hicho katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Katibu Mkuu wa TEC Fr. Raymond Saba alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na mtoto Balozi Joseph Moringe Sokoine alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Wajane na binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine wakiwa katika Ibada Maalumu ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo chake katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Ibada Maalumu ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo chake katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa wakishiriki katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Sehemu ya waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Viongozoi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapa mikono familia ya Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwapa mikono wajane wa Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstafu Mzee Benjamin William Mkapa wakiwapa mikono wajane wa Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisi dikizwa na Balozi Joseph Moringe Sokoine baada ya Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016.

PICHA NA IKULU
 
Moringe ilikuwa mtu muadilifu sana, sijui tulikosea wapi mpaka watu wa namna hii hawapatikani tena, sijui tulilogwa, sijui tulirubuniwa, sijui nini kilitokea mweee, sijui ni laana mweee
 
Ibada ya Wafu ...

Haitusaidii sisi vijana wa leo kuambiwa kuna kumbukumbu ya Sokoine BILA kuelezwa alifanya nini. Vijana wengi hawamfahamu huyu mtu kwa kina. Kwa nini historia yake imefinyangwa?!

Anyways!
 
Ingekuwa vizuri kwa wanaomjua kuandika kitabu kumuhusu na yote aliyolifanyia taifa hili..sisi wengine tunasikia jina tu!
 
Inawezekana tukitaka kwa ajili ya kuweka rekodi sawa.

Hakuna sababu ya kuchunguza kifo chake kwasababu walihusika wote wametangulia mbele ya haki na walio hai wapo katika hatua za mwisho za kuonana na Muumba kwaajili ya kujibu makosa waliyotenda ya kutoa uhai wa mtu wakati wakijua hiyo si kazi yao.
 
Moringe ilikuwa mtu muadilifu sana, sijui tulikosea wapi mpaka watu wa namna hii hawapatikani tena, sijui tulilogwa, sijui tulirubuniwa, sijui nini kilitokea mweee, sijui ni laana mweee
Wapo lakini hawapati nafasi...
 
Hakuna sababu ya kuchunguza kifo chake kwasababu walihusika wote wametangulia mbele ya haki na walio hai wapo katika hatua za mwisho za kuonana na Muumba kwaajili ya kujibu makosa waliyotenda ya kutoa uhai wa mtu wakati wakijua hiyo si kazi yao.
Kama nilivyosema awali zoezi liwe kwa dhumuni la kuweka rekodi sawa
 
Kama nilivyosema awali zoezi liwe kwa dhumuni la kuweka rekodi sawa
Rekodi sawa haziwekani tena vichwa muhimu kwaajili ya uchunguzi vimeshakatwa huo uchunguzi utaufanje iwapo wahusika wakuu hawapo.Hapo itakuwa majungu tu hakuna namna tena Sokoine aliwatoa kimaso maso wamaasai sana sema wamasaai wenyewe wamekuja jiharibia badala ya kuchunga Ng'ombe wanasuka nywele wadada powa.
 
Basi kama haiwezekani tena tumwachie Mungu, yeye anamipango yake na kama kuinua mtu, atainua tena mwingine kwenye hiyo jamii husika.
 
Naomba kuuliza, hivi hakuna picha yake halisi hadi watu wanaweka picha ya kuchora?
 
Tutapoteza muda na fedha, halafu kwa miaka 32 hakuna chochote kitakachosaidia baada ya uchunguzi
Kaka unafikiria familia yake ipo hepi....? Inapaswa uchunguzi ufanyike....!
 
Basi kama haiwezekani tena tumwachie Mungu, yeye anamipango yake na kama kuinua mtu, atainua tena mwingine kwenye hiyo jamii husika.
lakini si alishamuinua mwengine kutoka kwenye iyo jamii NYINYI mkamdhulumu haki yake?? Lakini haidhuru yupo kwa kila mioyo ya watanzania
 
Back
Top Bottom