Hakuna uhakika wala mahali pa kuthibitisha kuwa ujenzi wa reli utayaleta hayo unayoyasema yakiwemo kushuka kwa bei za kusafirisha bidhaa kutoka point A kwenda either point katika nchi hii.
Hii dhana sijaitoa ulaya, ni humu humu na nitakupa mifano kuntu na jadidi ya faragua mlengo wangu.
Tuliambiwa gesi asilia ya kule msimbati mtwara itapunguza bei kama sio kuufanya umeme kuwa wa uhakika nchini. Kiko wapi????
Treni sio njia au namna nzuri ya kupunguza bei za usafirishaji bidhaa. Nenda railway stations yoyote uliza bei ya kusafirisha Kg moja ya bidhaa fulani ni shilingi ngapi halafu ingia kwa wadau kwa mtaa uone kama bei za railway sio za usafiri wa kianasa.
Tuliwahi kuambiwa barabara ikikamilika nauli zitashuka kutoja point A to either points. Tena wakajibasibu kuwa hata muda wa kusafiri utapungua. Sitaki kuongea mengi bei za nauli zinajulikana na muda unaotumika umekuwa mara dufu na tochi nazo zimeongeza mapato kuliko TRA.
Hasara za ujenzi wa miundombinu hii ni kuongezeka kwa deni la taifa, madalali kuvuna hela za kutosha, ajali na watu kupoteza makazi na hicho ndicho huharibu uchumi hasa katika ngazi ya familia.
Hapo ndipo Prof. wangu unaweza m-google anasema "as concurred to previous premise that, do not trust those guys the only and only if truth that they can utter are neither their names as powered by bashite'z sagga"