Nyamtalakyono
JF-Expert Member
- Dec 17, 2015
- 795
- 479
Rais wangu mpendwa John Pombe Magufuli Salaam. Napenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa zawadi nzuri ya Reli uliyotupatia sisi watanzania wanyonge. Naona baadhi ya watu wanabeza jitihada zako lakini najua ipo siku watakukumbuka na kudai tume kumiss. Binafsi nimependezwa sana na kuanza kwa ujenzi wa Reli na najua ikikamilika itafungua fursa nyingi za kiuchumi hasa kwa wafanyabishara wadogo. Na niwahakikishie watanzania wa hali ya chini katika kipindi hiki cha utawala wa John Pombe Magufuli ndo wakati wa kunemeeka cha msingi ni kuchapa kazi. Reli hii itatuwezesha kusafiri na kusafirisha mizigo kwa bei nafuu tofauti na tunavyogongwa hivi sasa na wenye Malori na Mabasi.