MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Jana Rais alitembelea hospitali yetu ya taifa Muhimbili kumtembelea Mufti mkuu sheikh Aboubakar Zuber, lakini wakati wa safari yake hapo akadakwa na kina mama ambao walikua wakiuguza ndugu zao waliokwishajifungua hospitalini hapo, ndipo Rais alipoamua kuwasikilaza na kuongozana nao hadi wodi ya wazazi na kukuta idadi kubwa ya kinamama wamelala kiholela chini.
Binafsi nimekaa hospitalini hapo muda mrefu sana wakati nikimuuguza kaka yangu aliyekua amelazwa wodi ya mwaisela kiasi kwamba nilifikia mpaka kufahamiana na matabibu wengi na wauguzi na kujihisi kama mwenyeji.
Lakini kwa udukuzi wangu wa mambo ilibidi nijue niñi hua kinaisibu hospitali hiyo mpaka huduma kuzorota?
TATIZO
Ndani ya hospitali hiyo kuna idara nyigi sana na kurugenzi zake ambazo zinawajibika moja kwa moja kwa Mkurugenzi mkuu wa hospitali, lakni cha ajabu ni kwa wakuu wa idara hizi hukalia nafasi zao kwa muda mrefu mfano idara ya uuguzi,tiba, utumishi, fedha,ufundi,maabara,Radiolojia nk, hawa wakuu wa idara wengi wao hawatoi taarifa za kuaminika kwa Mkurugenzi mkuu ili aweze kushughulikia kama kuna matatizo, wamekua wakitoa taarifa za kumridhisha mkurugenzi tu tofauti na uhalisia.Wakuu hawa wa idara zote wamekalia nafasi zao kwa muda mrefu na wengine hujirudia mara kwa mara hali iliyowanya kufanya kazi kwa mazoea na ndio maana fiksi zinakua nyingi.
Kuna mzee mmoja Daktari hospitalini hapo waliniambia kwa mfano kuna idara kama ya ufundi vifaa zinaibiwa sana lakini uongozi uko kimya, idara ya tiba iko kimya ilihali kuna wagonjwa wanafika hospitalini hapo wanatibiwa na kupona lakini wanacheleweshwa kuruhusiwa na kubaki kulipia tu kila siku tu na kusababisha msongamano wodini.
TATIZO LA KINA MAMA KULALA CHINI!
Hapa tatizo liko idara ya tiba ambapo hata wale wagonjwa wasiokua na complicated cases za kupelekwa Muhimbili lakini wanalekwa na kupokelewa badala ya matatizo yao kushughulikiwa hata kwenye vituo vya afya huko, maana wanaopenda Muhimbili wagonjwa wasiostahili kupelekewa pale unategemea wenye hali mbaya wanaostahili kwenda pale wakipokelewa watalala wapi kama sio chini?
Kiingine ni Madaktari kuchelewa kuwaruhusu wagonjwa ambao waliokwisha pona hali inayopelekea wale wapya waokuja kulala chini.
Idara ya fedha nayo inalalamikiwa kwa kujumlishia wagonjwa bili ya gharama kubwa tofauti na gharama halisi alizotumia mgonjwa.
Kwahiyo Rais wangu Magufuli tumbua majipu badili idara zote na kurugenzi zote ndani ya hospitali hiyo! Hiyo kazi hata mawaziri wako wanaweza kufanya maana lasivyo utatwanga maji kwenye kinu miaka yako yote mitano bila mafanikio! Mbona Prof Sarungi aliiweza hospitali ya taifa Muhimbili?