kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
TANGU alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli amekuwa akitajwa kwa kupongezwa kwenye maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kwenye nyumba za ibada.
Utendaji wa Rais Magufuli unawagusa viongozi wa dini hivyo kumekuwa na maombi katika makanisa kumuombea kiongozi huyo Mungu amlinde akamilishe ndoto yake kuwapeleka Watanzania kwenye nchi ya asali na maziwa. Kwa nyakati tofauti, Rais Magufuli ameomba wananchi wamuombee na kwamba, yeye ni mtumishi na amejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania.
“Mungu ameikumbuka Tanzania, sasa hata sisi viongozi wa dini kazi yetu inakuwa nyepesi kwani Mungu kamleta kiongozi anayesemea maovu ya nchi hii na waovu pia,” ni kauli ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Dk Barnabas Mtokambali. Anayasema hayo wakati wa sherehe ya kuweka wakfu jengo la kanisa la TAG Nkuhungu mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa kanisa, Dk Magufuli ni tunu ya pekee kwa nchi ya Tanzania. “Mungu ameikumbuka Tanzania kwa kuwapatia kiongozi mkuu wa nchi mwenye uchungu na taifa Lake.” Dk Mtokambali anasema, Rais Magufuli ni miongoni mwa viongozi wachache Afrika wenye malengo na nchi na hutokea kwa nadra sana. Amemfananisha Dk Magufuli na viongozi kadhaa akiwemo Hayati Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania) Patrice Lumumba (Kongo) na Kwame Nkrumah (Ghana).
“Magufuli tumemkubali wanyang’anyi wezi hawatampenda, kanisa tunampenda, tunamkubali na tunamuombea. Ni nadra kupata Rais mwenye uchungu na nchi, hutokea mara chache sana,” anasema Dk Mtokambali. Anasema Rais Magufuli amekuwa na maadui wengi kutokana na kugusa maslahi ya watu. Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu anawataka Watanzania waendelee kumuombea Rais Magufuli kwa kuwa utendaji kazi unawagusa Watanzania wa hali ya chini.
Anasema kanisa litaendelea kumuombea ili aweze kufanya kazi anayoifanya kwa sababu hata vitabu vitakatifu vinataka usawa katika uchumi wa kipato kwa kila mtu. ‘’Tunawaomba Watanzania wazidi kumuombea Rais wetu, kasi aliyonayo aendelee kuwa nayo kwani Mungu anapenda haki katika maisha pamoja na uchumi ulio sawa,’’ anasema Askofu Kinyunyu. Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (CCC) Miyuji Dodoma, Samson Mkuyi anasema, utawala wa Rais Magufuli unaonekana kuwa ni jibu la Watanzania wengi na kanisa.
Anasema, wanafurahishwa na utendaji wake hasa kwenye maadili ikizingatiwa kuwa kanisa linataka maadili ya kiroho na kimwili. ‘’Tulianza kuyaomba haya miaka mitano. Sisi kama kanisa tunamwambia asiogope kwani Mungu yupo pamoja na yeye, sisi tunaendelea kumuombea ili Mungu aendelee kumpa ulinzi,’’ anasema Mkuyi. Askofu la Kanisa la Anglikana Central Tanganyika Dayosisi ya Kati Dk Dickson Chilongani anawataka Watanzania kumuombea Rais Magufuli na Baraza la Mawaziri wafanye kazi kwa ajili ya Watanzania.
‘’Rais ameonekana kutumbua majipu yaliyokuwa yamejificha, katika hili tutaendelea kumuombea ili aweze kuyatumbua zaidi, pia na kuwafanya watendaji wafanye kazi kwa usahihi,’’anasema Askofu Chilongani. Baraza Kuu la Maaskofu la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) limetoa tamko la kuukubali utendaji wa Rais Magufuli. Linasema, litaendelea kumuombea kiongozi huyo na wasaidizi wake kwa sababu ya juhudi za kurejesha uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali, kupiga vita ufisadi na rushwa.
Wametoa mwito kwa Rais Magufuli amalize mauaji kwenye maeneo mbalimbali nchini. Wametoa mfano wa mauaji yaliyotokea mkoani Tanga na kwamba, yamesababisha wananchi wawe na hofu kwenye nchi yao. Wanayasema hayo wakati wa kikao cha maaskofu kilichofanyika Dodoma. Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania, Askofu David Batenzi anasema, tangu uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano uingie madarakani wameshuhudia mambo mengi mema yakiwemo maadili kwa viongozi.
“Sisi Maaskofu wote wa Kipentekoste kwa kauli moja tunaikubali kazi kubwa inayofanyika na kumpongeza Dk Magufuli kwa kudhibiti matumizi ya mapato ya Serikali pamoja na juhudi za kuongeza ukusanyaji wa kodi na kuhimiza bidii ya kazi na usafi wa mazingira.” anasema. Askofu Batenzi anasema, Rais anafanya kazi kubwa kukemea viongozi wasio waaminifu kwa Serikali wakiwemo mafisadi, wala rushwa na wanaotumia vibaya rasilimali za umma.
“Sisi kama maaskofu wa CPCT tunaipongeza serikali kwa kuonesha nia ya kuwatumikia wananchi bila ubaguzi na tutahakikisha nyumba za ibada zinaendelea kumwombea ili Mungu ampe afya njema, hekima, na busara katika kufanya maamuzi mbalimbali anapotekeleza wajibu wake wa kuiongoza serikali,” anasema. Baraza limeahidi kuendelea kuombea mihimili yote ya dola ikiwemo Serikali, Bunge na Mahakama ili kuwepo na hekima busara na uaminifu wa kutenda haki kwa hofu ya Mungu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Maaskofu wamekemea vitendo vya mauaji na ubakaji kwa kuwa vinaashiria kupungua kwa maadili na ukosefu wa hofu ya Mungu. Wameitaka serikali ichukue hatua kubaini wahusika na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria ili haki itendeke. “Vitendo hivi visipodhibitiwa vitasababisha wananchi kuishi kwa hofu katika nchi yao jambo ambalo litaliondolea taifa sifa yake njema machoni pa mataifa mengine, pia litatisha wageni wanaolipatia taifa kipato lakini zaidi ya hayo taifa linaweza kujikuta linaangukia kwenye hukumu ya Mungu jambo ambalo halitatufaa,” wanasema kwenye tamko.
Askofu wa Kanisa la Eagle Gospel Mission Dodoma, Merick Zitto anasema Tanzania imepata kiongozi mkuu wa nchi mwenye uchungu na maisha ya Watanzania. Anasema Watanzania wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kumpata Rais wa aina ya Magufuli. Askofu Zitto anasema, kanisa hilo litaendelea kuiamini Serikali ya Dk Magufuli ili haki ipatikane kwa Watanzania wote.
Anawataka wasaidizi wa Rais wakiwepo mawaziri, manaibu wao, wabunge, madiwani na viongozi wengine kutorudisha nyuma jitihada zinazofanyika za kuisafisha nchi kwa kuwaondoa wote wanaobainika kuwa ni wezi, wala rushwa na mafisadi. “Kwa kushirikiana na kanisa na serikali ya awamu hii ya tano hakuna sababu ya kutompa ushirikiano Rais wetu Magufuli ambaye amejitoa sadaka kwa ajili ya Watanzania walio wanyonge, wanaoteseka na umasikini kutokana na baadhi ya watu wachache kujilimbikizia mali,” anasema Askofu Zitto.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Ajira Athony Mavunde anasema mjini Dodoma kuwa, Mungu amesikia kilio cha Watanzania kwa kuwapatia kiongozi mwenye uchungu na nchi. Anayasema hayo wakati wa ibada kumshukuru Mungu kwa kujibu maombi ya Watanzania wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita. Katika ibada hiyo kwenye Kanisa la Eagle Gospel Mission Uzunguni, Mavunde anasema kutokana na msaada wa maombi yanayoendelea nchini, Serikali ya Rais Magufuli inaendelea kupata mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwabaini viongozi wabovu.
Anasema Rais na wasaidizi wake wanaiamini kazi inayofanywa na waumini wa madhehebu ya dini katika suala la kuwaombea hivyo ndiyo maana kuna mafanikio. “Hivyo madhehebu ya dini tunaomba endeleeni kuiombea Serikali hii ya Awamu ya Tano chini ya Dk Magufuli pamoja na wasaidizi wake waweze kufanikiwa kuisafisha viongozi wabovu wanaohujumu uchumi wa taifa hili kwa kujimilikisha mali pamoja na madaraka waliyokuwanayo,” anasema Mavunde.
Anawataka waumini wa madhehebu ya dini kuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma zinazohusiana na mambo ya kiroho badala ya kuelekeza michango hiyo kwenye masuala yanayohusu starehe. Askofu wa Kanisa la Methodist Tanzania Jimbo la Dodoma, Joseph Bundala anasema, uamuzi wa wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa kususia Bunge ni upungufu wa hekima na kutojua wajibu wao.
Anasema wanafanya hivyo kwa sababu ya uchanga wao katika kidemokrasia kwa kutokutambua wajibu wao kuwawakilisha wananchi waliowaamini. Askofu Bundala anasema, wabunge wa Ukawa kususia vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika Dk Tulia Ackson hakuna maana na wanatakiwa wafahamu kuwa wanawanyima wananchi uwakilishi bungeni. “Kama kiongozi wa dini ninawasihi wabadilike haraka wa kutoka katika hali ya uchanga na kufikiria utimilifu wa kidemokrasia,” anasema.
Askofu Bundala anasema, wabunge hao wanapaswa kutambua kuwa, hakuna nchi isiyo na sheria hivyo Jeshi la Polisi ikibidi litumie nguvu kulinda amani na utulivu nchini. “Hakuna sababu ya kuoneana aibu katika suala la kulinda amani iliyopo ambayo Mungu ametutunukia Watanzania,” anasema. Amewataka Watanzania wasijiingize kwenye mivutano ya kisiasa.