G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,012
Unajua Tanzania ina watu wa ajabu sana na wa hovyo sana. Watu hawa ni wanachama wote ma mashabiki wa CCM. Nitaeleza kwa nini?
Miaka ya 1999 hadi miaka ya 2002 aliyekuwa rais wa enzi hizo ndugu Benjamin Mkapa alikuwa na ngonjera hizihizi za kudai kuwa wapinzani wanatumika na nchi zinazomendea uwekezaji wa Tanzania eti wao wenyewe wanawataka wawekezaji na sasa wamewakosa hivyo wanawatumia wapinzani kutoa maneno ya kichochezi ili wawekezaji hao waende kwenye mataifa yao. Wapinzani wakminywa kwelikweli na hapo wana CCM wakaimba kuwa Mkapa ni mzalendo atakayeleta utajiri Tanzania.
Miaka 17 baadaye amekuja mwingine na wapinzani wanampa njia sahihi ya kushughulikia matatizo yaliyojitokeza huko nyuma anaendeleza utamaduni ule ule wa Mkapa kuwa wapinzani wanatumika na sasa eti wamehongwa na majizi. CCM nao wameunga uzi wa kumuimba mkuu wao eti ni mzalendo kwelikweli aliyeletwa na Mungu.
Kwanza kabisa nimwambia rais Magufuli kuwa ni ndoto ya mchana kutegemea Tshs trilioni 100 kutoka kwa ACACIA. Ni kama wale wenzangu wa Kinondoni wakiwa wamepiga vitu wanapiga hesabu za eti wanakaribia kutua USA au "State"
Ni vyema kuwa huu muda tunaotumia kupoteza kujadili yasiyowezekana tukautumia kufanya yanayowezekana. Tusioteote tu na kisha tukaanza kuwakamata mazuzu akili!
Rais Magufuli abadilike na kufuata ushauri wetu sisi tunaokosoa serikali yake. Aachane na hawa watu wanaobadili rangi kuendana na hali ya maficho. Leo anasema hivi wanamshangilia, kesho atakuja mkuu wao mwingine ambaye atamchanachana Magufuli hadharani na watamshangilia pia. Ndivyo walivyo na watu kama hao ni kuwaepuka na kukubali kuambiwa ukweli.
Tusikae tukaanza kutarajia ndoto ambazo ni ngumu kuzifanikisha.
Any way kama hii ndoto ya kupewa hizo trilioni 100 itakuwa kweli basi na mimi niwape kaakaunti kangu nipatepo kamgao maana tutatajirika mpaka tuchizike.... thcheeeeee hili ndumu linanipeleka wapi tena?