Rais Magufuli anaiua CCM kifo cha mateso makubwa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,757
729,975
Wote tunajua watu waliouliwa kwa style tofauti kwa risasi moja kwa kuchinjwa shingo kwa kuchomwa moto kwa kipigo nk nk.

Pia kuna ule utaratibu wa kuunyima mti chakula kwa kuuchuna maganda kwenye mzunguko wake hivyo kuunyima supply ya chakula na virutubisho muhimu kwa kufanya hivi mti hufa taratibu, hiki nacho ni kifo cha mateso, kifo cha taratibu sana.

Hata kwenye mfumo wowote unaweza kuuangamiza mfumo mmoja maramoja au ukaupukuchua taratibu mpaka unaumaliza kabisa.

Kifo cha leo kukatwa mkono kesho mguu keshokutwa sikio mtondogoo kung'olewa jicho ni wazi hakuna ambaye angependa kifo cha namna hii ni kifo kibaya na cha mateso makubwa na udhalilishaji pua huku muuaji alikikiuka haki za kuishi au kufa za mwanadamu.

Magufuli anachoifanyia CCM ni kifo cha taratibu dhalili na kilichojaa mateso ni furaha yangu ni furaha ya wengi hakuna asilofanya kwasasa lisilogusa maslahi ya CCM, kuanzia kwa wafanyakazi wafanya biashara mpaka kwenye taasisi za umma.

Ukiliweka hili kwenye mtazamo wa mwili unaona kabisa anavyonyofoa kiungo kimoja kimoja, CCM ya sasa imebaki dhaifu na dhalili hasa!

Hakuna hata mmoja wao anayeweza kusimama kifua mbele na kupaza sauti akisema Rais Magufuli anatekeleza ilani ya chama.

Nina hamu ya kuona kichwa kitakatwa lini
 
Wote tunajua watu waliouliwa kwa style tofauti kwa risasi moja kwa kuchinjwa shingo kwa kuchomwa moto kwa kipigo nk nk
Pia kuna ule utaratibu wa kuunyima mti chakula kwa kuuchuna maganda kwenye mzunguko wake hivyo kuunyima supply ya chakula na virutubisho muhimu.kwa kufanya hivi mti hufa taratibu, hiki nacho ni kifo cha mateso, kifo cha taratibu sana
Hata kwenye mfumo wowote unaweza kuuangamiza mfumo mmoja maramoja au ukaupukuchua taratibu mpaka unaumaliza kabisa
Kifo cha leo kukatwa mkono kesho mguu keshokutwa sikio mtondogoo kung'olewa jicho ni wazi hakuna ambaye angependa kifo cha namna hii ni kifo kibaya na cha mateso makubwa na udhalilishaji pua huku Muuaji alikikiuka haki za kuishi au kufa za mwanadamu
Magufuli anachoifanyia ccm ni kifo cha taratibu dhalili na kilichojaa mateso.. ni furaha yangu ni furaha ya wengi....hakuna asilofanya kwasasa lisilogusa maslahi ya ccm, kuanzia kwa wafanyakazi wafanya biashara mpaka kwenye taasisi za umma
Ukiliweka hili kwenye mtazamo wa mwili unaona kabisa anavyonyofoa kiungo kimoja kimoja, ccm ya sasa imebaki dhaifu na dhalili hasa! Hakuna hata mmoja wao anayeweza kusimama kifua mbele na kupaza sauti akisema Magufuli anatekeleza ilani ya chama....

Umeandika kinyume!
 
Anaelewa sana ila basi tuu. Ndio maana chama chake sasa kimekuja na style ya kudandia ziara za kiserikali za viongozi wa nje na kujifanya zinawahusu. Kweli ccm iko katika kifo cha mateso
Utachakazwa dogo!barafu limetiwa ndani ya maji moto lazima yatapoa tuuu!
 
Wote tunajua watu waliouliwa kwa style tofauti kwa risasi moja kwa kuchinjwa shingo kwa kuchomwa moto kwa kipigo nk nk
Pia kuna ule utaratibu wa kuunyima mti chakula kwa kuuchuna maganda kwenye mzunguko wake hivyo kuunyima supply ya chakula na virutubisho muhimu.kwa kufanya hivi mti hufa taratibu, hiki nacho ni kifo cha mateso, kifo cha taratibu sana
Hata kwenye mfumo wowote unaweza kuuangamiza mfumo mmoja maramoja au ukaupukuchua taratibu mpaka unaumaliza kabisa
Kifo cha leo kukatwa mkono kesho mguu keshokutwa sikio mtondogoo kung'olewa jicho ni wazi hakuna ambaye angependa kifo cha namna hii ni kifo kibaya na cha mateso makubwa na udhalilishaji pua huku Muuaji alikikiuka haki za kuishi au kufa za mwanadamu
Magufuli anachoifanyia ccm ni kifo cha taratibu dhalili na kilichojaa mateso.. ni furaha yangu ni furaha ya wengi....hakuna asilofanya kwasasa lisilogusa maslahi ya ccm, kuanzia kwa wafanyakazi wafanya biashara mpaka kwenye taasisi za umma
Ukiliweka hili kwenye mtazamo wa mwili unaona kabisa anavyonyofoa kiungo kimoja kimoja, ccm ya sasa imebaki dhaifu na dhalili hasa! Hakuna hata mmoja wao anayeweza kusimama kifua mbele na kupaza sauti akisema Magufuli anatekeleza ilani ya chama....
Nina hamu ya kuona kichwa kitakatwa lini
kwa hili bandiko lako leo nadhani mshana umeandiko isivyo kwa maoni yangu,

tangu utawala huu uanze jpm amechukua hatua mbalimbali za kubana matumizi na kuwawajibisha wabadhirifu serikalini, na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wakwepa kodi,

hizi hatua asimia kubwa ya wananchi kama sio wote wanaziunga mkono,
utasemaje kwa hatua hizi anaiua ccm taratibu?
wewe unaamini uhai wa ccm ulishikiliwa mikonono mwa wabadhirifu?

jaribu kunisaidia kidogo sijaelewa.
 
Mleta mada ameandika/anafikiri kinyume ili aufariji moyo wake ila ajue tu ukweli ni mchungu na haupendi kupuuzwa.
 
kwa hili bandiko lako leo nadhani mshana umeandiko isivyo kwa maoni yangu,

tangu utawala huu uanze jpm amechukua hatua mbalimbali za kubana matumizi na kuwawajibisha wabadhirifu serikalini, na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wakwepa kodi,

hizi hatua asimia kubwa ya wananchi kama sio wote wanaziunga mkono,
utasemaje kwa hatua hizi anaiua ccm taratibu?
wewe unaamini uhai wa ccm ulishikiliwa mikonono mwa wabadhirifu?

jaribu kunisaidia kidogo sijaelewa.
Kimsingi ni kwamba anachofanya Magu sio style ya ccm..ccm ilijaa kulindana (January makamba)kulikuwa hakuna kuwajibishana labda uwe wewe sio mwenzao...
Sasa hivi Magufuli hacheki na kima wala ngedere, ccm walidhani angekikumbatia chama kwa mikono mirefu na mbeleko ya kijani...matarajio yamekuwa kinyume
 
Umepanik dogo!
Sawa kubwa...!haya turejee kwenye mada sasa
e2a306c68fdf90aea38f49d488e05280.jpg
 
Ukawa wameishiwa pumzi..manake walitegemea angalau chai ikulu hamna kitu...wao ni movie tu.
Kama unaweka mawazoni mwako kitu kama chai ni ishara ya umasikini uliotukuka katika maisha yako. Tafuta kazi ya maana ufanye hii ya buku 7 utaishia kulalia Hindi la kuchoma. Ni ushauri tuu
 
Back
Top Bottom