Rais Magufuli anafanya siasa za maendeleo bila kubagua

JOYOPAPASI

Member
Jan 10, 2016
57
150
JPM hafanyi siasa za ubaguzi, bali anafanya siasa za maendeleo kwa mustakabali wa taifa

Na Hamis Shimye

KUMEKUWEPO na kampeni ya kitoto kwenye mitandao ya kijamii inayoongozwa na viongozi wa vyama vya upinzani nchini ambavyo vinadai Rais Dk. John Magufuli ni mbaguzi, ambapo wanafanya hayo ili waweze kuungwa mkono na hatimaye kupata kura za huruma kwa wananchi kwa hoja za kubumba zisizokuwa na mashiko.

Kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020, wapinzani wameanza kuonekana kuishiwa hoja na badala yake wamekuwa watu wa kudandia matukio na kumzushia uongo na uzandiki hata pale anapokuwa anataniana na mtu wao wanaichukulia ni kauli rasmi ya Rais wakati sio kweli huku wakishindwa kung'amua ukweli wake kuwa anafanya maendeleo kwa ajili ya jamii nzima ya watanzania.

Mambo makubwa aliyoyafanya Rais Dk. Magufuli katika kipindi cha miaka mitano angekuwa MBAGUZI angeyafanyia nyumbani kwake, leo mkoani Kigoma pekee kuna barabara lukuki, amesaidia wakulima wa michikichiki, kuna mradi wa Uwanja wa Ndege unataka kuanza, kuna vituo vya afya na Hospitali zinajengwa huku barabara nazo wakandarasi wako 'site'. Huu ni ubaguzu gani wanaomzungumzia Rais anautenda?.

Rais Dk. Magufuli amefanya makubwa katika kipindi chake chote cha awamu ya kwanza kinachokwenda kumalizika na ametoa shahuku kubwa ya kuendelea kupigiwa kura za kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, ambao ameshaumaliza mapema kutokana na utendaji kazi wake na si kwa porojo ya UBAGUZI wanayoiaminisha wapinzani ambao hawana maono na uthubutu.

Uimara na uthubutu wake, ndio unafanya kuwa moja ya sababu kuu ya Rais Dk. Magufuli kupata kura nyingi na za kishindo kwenye uchaguzi mkuu unaokuja kwa kuwa amekuwa kiongozi mwanamageuzi mwenye kuleta maendeleo makubwa kwa taifa na hata kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati, ambapo kwa jitihada zake amekuwa mkombozi kwa taifa ambalo lilikuwa linanyonywa kwa kiasi kikubwa na hatatengeneza TABAKA lolote kwa mtu yeyote kwa kuwa amekuwa na sera ya UMOJA na sio UBAGUZI.

Dk. Magufuli amekuwa msaada tosha kwa nchi hasa kutokana na kuitoa nchi kiuchumi kutoka asilimia 6.2 hadi asilimia 6.9 kwa mwaka huu, ambapo ameweza kuboresha huduma za kijamii kwa kiwango kikubwa na hata kuondoa umasikini kwenye kaya mbalimbali maeneo yote ya nchi kuanzia Lindi, Mtwara hadi Kilimanjaro huko kote kuna miradi mikubwa ya serikali inatekelezwa.

Rais Dk. Magufuli ameshamaliza uchaguzi mapema kutokana na kuwa kiongozi anayetatua shida za wananchi wake waliompa kura na ndio maana amekuwa akikerekwa na umaskini wao na sio kitu kingine na sababu hiyo ndiyo inayompa ushindi wa kura nyingi za NDIYO Rais Dk. Magufuli katika uchaguzi huu kwa kuweza kusambaza umeme kwenye vijiji vyote nchini na kuwa historia kubwa ambao hadi sasa vijiji 9112 vina umeme wa uhakika na hata kuondoa matatizo ya kukosekana kwa umeme ambao baadhi yao toka tulipopata Uhuru walikosa kupata umeme wa uhakika. Sasa hapo amefanya UBAGUZI gani?

Pia, kumekuwepo na mafanikio makubwa kwenye sekta ya viwanda, ambayo ilikuwa ni msingi wake mkuu wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 ambayo aliahidi kufufua viwanda na amefanikiwa kwa viwanda 61,110 kupatikana katika kipindi cha miaka mitano na kufanya kuwepo na msingi mkubwa kuelekea uchumi wa kati 2025, ambapo viwanda vipo kwenye kila mkoa huku Pwani ikiwa inaongoza. Je tuwaulize wapinzani makanjanja huo ni UBAGUZI wa Rais ambaye anatoka Kanda ya Ziwa anayepeleka maendeleo Pwani?

Kukua kwa mapato kutoka sh Bilioni 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi Sh Trilioni 1.3 kwa mwezi mwaka 2020 ni hatua moja kubwa kwa taifa kupiga hatua kubwa kimaendeleo na hata kuondokana na umaskini ambapo Rais Dk. Magufuli amesimamia nchi kujiendesha kimapato na kuondokana na umaskini huku mapato hayo yakiwa wazi na matumizi yake yanaonekana kwa taifa huku yakitumika kwa shughuli za maendeleo bila ubaguzi wowote.

Wapinzani wanapaswa kutambua uongo na maneno ya kitapeli wanayoyatoa hayana uwezo wa kubadilisha fikra na mawazo ya watanzania kumpa kura Rais Dk. Magufuli kwa kuwa sababu kubwa inayofanya kupewa kura nyingi za NDIYO zinatokana na utendaji kazi wake uliotukuka na hata kuwa na matumaini makubwa kwa watanzania ambao amewatendea haki katika kuleta mapinduzi ya kimkakati katika nchi ya Tanzania bila UBAGUZI wowote.

Amefanikiwa kupunguza umasikini kutoka asilimia 28.2 kwa mwaka 2015 hadi asilimia 26.4 kwa mwaka 2020, ambapo hayo yametokana na uthubutu wa utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli kutumia rasilimali zilizopo katika kuleta maendeleo kwa taifa na 2020 ni sehemu ya yeye kupewa kura za heshima za NDIYO kama shukurani za Watanzania ambao wanaongozwa kwa USAWA na bila UBAGUZI wowote.

Rais Dk. Magufuli amefanya makubwa ikiwemo ujenzi wa miradi ya kimkakati kwa fedha za ndani ikiwemo reli ya kisasa ya standad gauge, ununuzi wa ndege mpya kwa ajili ya Shirika la Ndege ATCL na ujengaji wa bwawa la umeme la Mwalimu Julius Nyerere. Haya ni matunda ya kuwa na rais mwenye maono ya kuleta maendeleo kwa taifa letu na asiye kuwa na UBAGUZI kama wanauhubiri wapinzania uchwara.

Chemchem ya mafanikio haya yanapaswa kuenziwa kwa kila mtanzania na heshima pekee anayopaswa kupewa Rais Dk. Magufuli ni kura nyingi za NDIYO ambazo zitakuwa chachu ya kuendelea kutupa maendeleo makubwa watanzania ambao awali ilikuwa ndoto kuyapata maendeleo hayo hasa kutokana na urasimu uliokuwepo ambapo jamii ilikuwa inakosa kupata maendeleo kutokana na ubabaishaji uliokuwepo.

Uthubutu na utayari wake wa kuwatumikia watanzania ni sifa moja kuu ya Rais Dk. Magufuli kuwa ni mzalendo namba moja mwenye shahuku ya kuwatumikia watanzania kwa moyo wa kizalendo na ndio maana amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia maendeleo ya nchi kwa moyo mkubwa licha ya uwepo wa changamoto za wasaliti ambao sasa "wanampakazia" maneno kuwa ni MBAGUZI wakati katika mioyo yao wanaamini kuwa mtu huyu ni jembe lenye kuleta maendeleo kwa jamii.

Oktoba 2020 ni wakati wa kwenda kutoa shukuran za dhati kwa Rais Dk. Magufuli juu ya utendaji kazi wake kwa watanzania ambapo amejitoa kwa hali na mali kwenye shida na kwenye tanuri la moto pale mabeberu walipotaka kutukwamisha kwa maslahi yao yeye alisimama imara kama askari shupavu namba moja kwenye kuleta maendeleo ya taifa la Tanzania na wala si mzandiki kama walivyo wanasiasa wa UPINZANI.

Kwa mantiki hiyo, huu ni wakati wa kila mtanzania siku ya uchaguzi kwenda kumpa kura nyingi za NDIYO Rais Dk. Magufuli kama ishara ya kumshukuru kwa kuonyesha vitendo tafsiri ya kiongozi imara na mwenye maono makubwa kwa taifa letu la Tanzania katika kuleta maendeleo kwa kila mwananchi na bila UBAGUZI wowote ule kama wanavyoeneza wanasiasa wa upinzani waliofilisika sera za kuzungumza kwa jamii.

Screenshot_20200801-112606_1.jpg
 

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,166
2,000
Hao wasema hivyo na vipofu wapinga yote tumewazoea Kama watz na watatuelewa Oct 28 2020!
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
5,186
2,000
Pole sana kwa kuwa na kazi nzito ya kumtetea mtu ambaye wananchi wanaona waziwazi jinsi anavyobugi step. Ubaguzi upo sana sema tu vyombo vya habari siku hizi vimepigwa stop kusema kitu ila twashukuru kuna social media na watz wanajitahidi kuitumia. Kuna ubaguzi mkubwa sana awamu hii, kwa kifupi tu:
-ubaguzi wa vyama kama ilivyokuwa wazi wiki hii huko kusini.
-ubaguzi wa kikabila
-ukurupukaji katika maamuzi
-uonevu mkubwa kwa wanasiasa wa upinzani, linajulikana wazi jambo hili
-vitisho kwa wateule wake, tumeona wengi wakikimbilia ubunge kuliko kubaki katika nafasi za uteuzi
-hata ndani ya ccm watu wamekimbia kwa kukosa nafasi za kutumia demokrasia yao, akina Membe hata wazee wa chama akina Makamba wametupwa
-visasi, hivi ni vingi sana, akina January Makamba wametupwa bila hata sababu nzuri
-nk,nk,nk
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,087
2,000
Nilidhani mleta atapinga kuwa Rais hakusema maneno aliyoyasema akiwa Kilwa. Mkuu wa wilaya na DED wamechaguliwa na yeye mwenyewe. Wakifanikiwa kufanya jambo inasifiwa CCM, wakishindwa atalaumiwa mbunge au diwani wa upinzani.

Aliyosema Rais Kilwa hayana tofauti na maneno ya Spika kuwa anayepinga bajeti ya serikali maendeleo hayatapelekwa kwenye jimbo lake, ya mwenyekiti wa UVCC Taifa kuwa CCM ndio inaamua maendeleo yaende wapi.

Maneno haya yatakumbukwa daima!!
 

Black Mirror

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
350
500
Ninachokiamini vijana wengi wa kitanzania akili zao ni finyu sana tena sana tena sana, yaani ufinyu wao ni kwamba hawalijui vizuri Taifa lao la Tanzania, wakifika mjini na baadhi ya maeneo machache wanaamini Tanzania nzima iko hivyo, mkitaka kuijua vizuri nchi yenu zunguka kote, mijini na vijijini mfanye ulinganifu wa maendeleo alafu ndipo muweze kuandika kama kuna ubaguzi au hakuna ubaguzi wa kuleta maendeleo kwa Watanzania.
 

Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,811
2,000
Umeandika vizuri hata kama deep down moyoni mwako unajua ulichoandika si sahihi!

Umekosea pahali padogo tu, hukuweka Namba yako ya simu. Ila picha yako ni nzuri sana na hiyo ya Mh. Mwenyekiti akimwaga chozi katika mazishi ya Hayati Mkapa haikufaa kuambatana na propaganda ulichoandika.

Next time uweke na email address yako ili walioko jikoni wakufikie kwa uharaka na urahisi zaidi.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 

mr.London

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
2,776
2,000
Juzi alisema anamjengea mkuu 1 barabara kupitia kodi za watanzania ambazo hazikuwa katika mpango na matumizi sababu kubwa ni kwamba alikuwa analipa fadhila kwa mema waliyotendeana wao kwa wao binafsi
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
16,259
2,000
Hoja zipi wameishiwa wapinzani? Aliyemtuma magufuli kwenye Rufiji kutoa kauli za ubaguzi ni wapinzani? Kule kilosa ni wapinzani walimtuma magufuli kutoa kauli za kibaguzi? Acha ujinga wewe kama unasaka uteuzi kwa ujinga huo hupati uteuzi, wapinzani wanazo Hoja nyingi kama ulikuwa hujui, CCM mmeanza kampeni kabla ya wakati Rushwa zimetawala kura za maoni na kuna vituko vinaenda kutokea Dodoma kurejesha majina ya watu wasio na sifa kuwaonea walioshinda kura za maoni kisa Takukuru wamewakomoa kwa kuwapendelea wale wasio na sifa lakini wana pesa za kutengeneza fitna propaganda kwa washindi ambao hawana uwezo wa kuongea na Takukuru kwa sababu ni watu safi.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
16,259
2,000
Maendeleo siyo Hisani za CCM, maendeleo siyo pesa binafsi zinatoka mifukoni mwa CCM, maendeleo ni lazima kwa walipa kodi acheni siasa za kishamba zilizopitwa na wakati
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
16,259
2,000
Ninachokiamini vijana wengi wa kitanzania akili zao ni finyu sana tena sana tena sana, yaani ufinyu wao ni kwamba hawalijui vizuri Taifa lao la Tanzania, wakifika mjini na baadhi ya maeneo machache wanaamini Tanzania nzima iko hivyo, mkitaka kuijua vizuri nchi yenu zunguka kote, mijini na vijijini mfanye ulinganifu wa maendeleo alafu ndipo muweze kuandika kama kuna ubaguzi au hakuna ubaguzi wa kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Nchi ya Tanzania ina zaidi ya miaka 50 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, pesa nyingi inatumika kudidimiza demokrasia, kuihujumu kuidhoofisha chadema badala ya maendeleo
 

Mhujumu Uchumi

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
943
1,000
Kazi kweli kweli kumtetea shetwain na kuwaaminisha binadam kuwa shetani ni malaika mzuri!

Mataga poleni sana, huyo jiwe kapoteza mwelekeo kabisa, ni roho mbaya, mbaguzi, katili, hata umtetee vp huwezi kuwashawishi Watanzania wampigie kura huyo mtusi kutoka nchi jirani
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
16,259
2,000
Ubaguzi upo mwingi sana kwenye utawala huu wa awamu ya tano hata mje na utetezi upi hamuwezi kuwafanya watu waache kuamini hakuna ubaguzi
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
16,259
2,000
Kazi kweli kweli kumtetea shetwain na kuwaaminisha binadam kuwa shetani ni malaika mzuri!

Mataga poleni sana, huyo jiwe kapoteza mwelekeo kabisa, ni roho mbaya, mbaguzi, katili, hata umtetee vp huwezi kuwashawishi Watanzania wampigie kura huyo mtusi kutoka nchi jirani
Naunga mkono hoja yako kwa 100%
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,647
2,000
Magufuli 2020..
Wananchi hatuwezi kumtosa.. huku tunaona yupo supaaaa.. kutuongoza tena.. kwa mazuri anayoifanyia nchi yetu hii.. Bora watayarishe akili zao mapema..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom