Rais Magufuli amuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu wa Tanzania

benja

JF-Expert Member
May 10, 2011
320
215
Imagee.jpeg
 
ibra_juma.jpg
Wanabodi

Kama ilivyo ada ya JF be the first to know, Kaimu Jaji Mkuu Prof.Ibrahim Juma ataapishwa leo Saa 10:00 Jioni.

Tukio hilo litatangazwa live na TBC.

Source: Reliable under the confidentiality of the source.

Paskali.

Kumhusu Prof. Juma huu ni wasifu wake.

(Full disclosure: Prof. Ibrahim Juma ni mwalimu wangu na mtu ninaye mheshimu sana). Naweza kuwa sifahamu sana utendaji wake ndani ya Mahakama, lakini humtendei haki ukisema ni msomi wa Ovyo. He is an accomplished scholar. And no scholar I know in the judiciary can match his scholarship. None.

For your info:

Academically: Judge Ibrahim Juma ana:

1. Bachelor of Laws, University of DSM.
2. LLM, University of DSM
3. LLM Ghent University, Belgium (specialty: Law of the Sea)
4. Masters of Laws (International Human Rights Law), Raoul Wallenberg University, Lund, Sweden.(One of the very best Human Rights institutions in Europe).
5. PhD, Ghent University Belgium (specialty: Law of the Sea).

Google hivyo Vyuo (na Thesis zake zipo online)

Prof. Juma ni mbobezi kwenye sheria za Bahari (he is an expert in the law of the sea-PhD na LLM yake alibobea humo).

Alivyorudi UD, ni katika wasomi wachache ambao walikuwa na utaalam wa sheria za bahari (mwingine kwa Tanzania ni Prof. Mahalu na Prof. Nasila Rembe-Huyu aliishia huko kusini mwa Africa na of course wapo wengine wachache-lakini yeye ndo alikuwa mtaalamu mbobezi).

Prof. Juma ameandika sana, I mean ana maandiko kwenye journals nyingi za kimataifa. Amefanya compilation ya Index of cases za Criminal Law (yeyote aliyepita Faculty ya sheria mlimani aliitumia), ame-publish vitabu kwenye Human Rights, Law of The sea, refugee law, international law, environmental law etc-jaribu hata ku-google) utapata kazi zake nyingi online. Ame-edit vitabu kama vinne na Professor Chris Maina Peter nk.

NAWEZA KUSEMA KWA DHATI KABISA Profesa wa UDSM anayeweza kumzidi publications Prof. Ibrahim Juma (na weledi labda) ni Prof. Chris Maina Peter na Issa Shivji (amestaafu) (hawa wako kwenye dunia yao-again kwa aliyepita UD ananielewa). No body else. I repeat no body else. Hata Prof. Kabudi, kwangu mimi hafiki hata nusu ya Prof. Ibrahim Juma (ingawa na yeye ni mtaalamu in his own right).

Prof. Juma ni katika walimu wachache sana pale UDSM waliokuwa very thoughtful, fair in their dealings with students, straight forward with unimpeachable integrity.

Siwezi kuongelea kipindi ambacho ame-join judiciary 2008 onwards. Lakini as a matter of fact, kwangu mimi Prof. Juma anastahili hata kuwa Judge International Tribunal for the Law of the Sea (Hamburg) au International Court of Justice (The Hague). Kwamba alimsaidia Ridhiwani Kikwete asi disco-it is just garbage and not even worth a discussion. By the way ninavyomfahamu Prof. Juma, hata kama angekuwa na hiyo nafasi asingeweza. He simply cant.

Narudia kusema, jamani hata kama tunachukia mtu Fulani tujitahidi kuwa fair in our assessment. Maana mimi ninavyomfahamu Prof. Juma, kusoma bandiko la ndugu yangu Lusungo naona ni chuki zimemjaa kabisa au humjui Huyu bwana (excuse my language).

Again, Prof. Juma anaweza kuwa na mapungufu yake kama binadamu mwingine yeyote. lakini tuwe waangalifu. Kama hatuna information za kutosha tusidharau watu kwa chuki zetu au kwa kuambiwa.

Masanja
Mkuu Masanja Asante kwa kumtendea haki Prof. Ibrahim Juma, sisi wengine tumejaaliwa kuiona integrity ya mtu kwa macho tuu, hivyo watu wote wenye jicho la uoni wa ndani ya mtu, watakubaliana na mimi, Prof. Ibrahim Juma is a man of integrity and you can see it just by naked eyes!.

Pamoja na madudu yote ya rais Magufuli kukanyaga katiba lakini kuna machaguo anaongozwa na Mungu na ndio maana kati ya majina matatu aliyopelekewa, aliweza kumuona Prof. Juma.

Paskali
Jaji Othman Chande astaafu, Magufuli amteua Jaji Prof. Ibrahim Juma kukaimu
 
Utamuapishaj nusu nusu?? Angempa full tu ajue moja kustaafu sio sawa na kitengua!! Alishajua kuwa anatoka....unateua moja kwa moja....hakuna haja kumjaribu kama umeshamuamini! JM nafasi nyeti sana inabidi awe na confo nae n kumpa moja kwa moja
 
Kwani Rais atateua jaji mkuu tena!!.Atakuwa huyo huyo au mwingine.na kama atakuwa huyo huyo kumteua sasa ni jaribio au nini?
 
Kwa hiyo vituo vingine vya habari haviruhusiwikuonyesha mubashara!?
 
Utamuapishaj nusu nusu?? Angempa full tu ajue moja kustaafu sio sawa na kitengua!! Alishajua kuwa anatoka....unateua moja kwa moja....hakuna haja kumjaribu kama umeshamuamini! JM nafasi nyeti sana inabidi awe na confo nae n kumpa moja kwa moja
Ndicho nilitaka kuuliza pia, anayekaimu huwa anaapishwa kwa kiapo kile kile kama aliyeteuliwa!?
 
IKULU, DAR: Rais Magufuli amuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania leo January 18, 2017 saa kumi kamili jioni.
 
Hivi ni lini wakina mama wataanza kupewa nafasi ya ujaji mkuu, au hakuna majaji wanawake?, hili linapaswa kuangaliwa
 
Sijaelewa kulikuwa kuna sababu gani ya kuteuwa mtu wa kukaimu kwanza kwa nafasi ambayo ipo wazi..!!??

Au ndio anampima kama ataweza kufuata maelekezo yake??!

Haha ngoja tuone.
 
Utamuapishaj nusu nusu?? Angempa full tu ajue moja kustaafu sio sawa na kitengua!! Alishajua kuwa anatoka....unateua moja kwa moja....hakuna haja kumjaribu kama umeshamuamini! JM nafasi nyeti sana inabidi awe na confo nae n kumpa moja kwa moja
Nafikiri ana cross check kama atakuwa mtu wa kufata maelekezo yake.
 
Back
Top Bottom