Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) .
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18Juni, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Dkt. Jim James Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkmugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
21 July, 2016