Leo kulikuwa na matukio mawili makubwa, likitanguliwa na mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media, Ruge Mutahaba kukiri uvamizi uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa kutumia vyombo vya dola na kulaani Kitendo hicho akifuatiwa na waziri wa habari, Nape Nnauye ambae naye alisema kitendo hicho kimenajisi tasnia ya habari mwisho mwenyekiti wa MOAT, Reginald Mengi kupigilia msumari kwa kuwataka waandishi wasirudi nyuma na wasiogope.
Matukio yote hayo ya mapema na sauti iliyopazwa jana, ilitegemewa leo mkuu wa mkoa wa Dar aidha aachie ngazi kwa hiari au kwa kushurutishwa. Tofauti na matarajio, Rais Magufuli ametaka mkuu wa mkoa achape kazi na amewaasa wana Dar kuacha kutekwa sana na udaku japo ni uhuru wao lakini wajikite katika ujenzi wa uchumi.
Rais amesisitiza watu wanahangaika kuposti mitandaoni na wapo waliodiriki kumpangania lakini yeye ni Rais anayejiamini na ndie anapanga nani akae wapi.