Rais Magufuli ameyaagiza mashirika ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda badala ya majengo

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Leo Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya mashirika ya NSSF na PPF mjini Arusha ameyataka mashirika hayo kuwekeza kwenye viwanda kwani pamoja na mambo mengine viwanda vinaajiri watu wengi zaidi.

Amesema kama pesa walizotumia kujenga majengo hayo wangezitumia kuanzisha viwanda ingekua na tija zaidi.

Habari zaidi...

Rais Magufuli: Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania kwanini Asife? Hivi Hatuhurumii hata Kidogo?


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao wengi wao wako vijiweni.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60 yaliyojengwa jijini hapa.

Rais Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo.

Alisema suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana.

Alisema NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifanye biashara na wanachama wa mfuko huo wapate faida haraka haraka na kuachana na uwekezaji wa majengo.

"Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya

"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kampuni ya madini ya Signature iliyopanga katika jengo la mfuko huo la Mafao House imeajiri vijana zaidi ya 47 wa kuchonga tanzanite na watashirikiana katika kuanza biashara hiyo.

Profesa Kahyarara alisema kauli ya Rais ya shirika hilo kujikitaka katika biashara ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo wataifanyia kazi haraka iwezekanavyo bila ya wasiwasi wowote.

Hata hivyo, serikali ilishapiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi na kutaka madini yote kuchongwa nchini na wazawa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo.


===================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaagiza mashirika yote ya Hifadhi ya jamii kutoendelea kuwekeza katika miradi ya majengo na badala yake yajielekeze katika ujenzi wa viwanda na miradi mingine inayozalisha ajira na kuchangia zaidi katika patoIa taifa.

Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu tarehe 09 Mei, 2016 alipofungua majengo mawill ya vitega uchumi ya Mfuko wa Pensheni (PPF) na Shirika Ia Hifadhi ya Jamii(NSSF) yaliyopo Jijini Arusha.

Pamoja na kuyapongeza mashirika hayo kwa kujenga majengo ya kisasa jijini Arusha na maeneo mengine hapa nchini, Dkt. Magufuli amekosoa uwekezaji mkubwa unaofanywa na mashirika hayo kwa kujenga majengo ya gharama kubwa ambayo licha ya kuwa wananchi wa kawaida hawawezi kumudu gharama za kupanga kwa ajlli ya kuendesha shughull zao, hayana manufaa ya kutosha ikilinganishwa na endapo mashirika hayo yangewekeza katika miradi inayozalisha ajira nyingi, faida ya haraka na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika palo Ia taifa.

'Hii mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzia leo muache kuwekeza katika majengo, wekezeni kwenye viwanda, leo mngekuwa na viwanda vya sukari hawa watu wasingetuchezea kuficha sukari, na inawezekana hata kama ingepungua tungewambia nyinyi agizeni sukari.

'Mchango wa mifuko ya hifadhi za jamii katika nchi yetu, ambayo iko saba, imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 12, lakini hifadhi ya jamii sehemu nyingine duniani, imekuwa ikichangia palo la taifa kwa asilimia 40, kwa hiyo kuna mahali tumekosea, na ndio maana mlipokuwa mkizungumza hapa sijui mlijua nitakayowaambia, ninawapongeza mliwekeza katika majengo, jengo Ia PPF na jengo IB NSSF ukipiga hesabu za kawaida haya majengo yamegharimu zaidi ya shilingi bllioni 60, lakini tujiulize hawa wananchl waliosimama hapa watayatumiaje haya majengo' Amesema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na wananchi wa Arusha waliojtokeza kushuhudia ufunguzi huo.
 

Attachments

  • Magufuli.png
    Magufuli.png
    91.9 KB · Views: 105
Leo Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya mashirika ya NSSF na PPF mjini Arusha ameyataka mashirika hayo kuwekeza kwenye viwanda kwani pamoja na mambo mengine viwanda vinaajiri watu wengi zaidi. Amesema kama pesa walizotumia kujenga majengo hayo wangezitumia kuanzisha viwanda ingekua na tija zaidi.
Hayo ndo mawazo ya maana kuliko kufukuzana na kununua viwanja na kujenga majengo chini ya viwango.

Sasa ndo tutawaona wanavyoweza kupanga vitu vya maana badala ya upuuzi wa madaraja na office space.
 
Leo Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya mashirika ya NSSF na PPF mjini Arusha ameyataka mashirika hayo kuwekeza kwenye viwanda kwani pamoja na mambo mengine viwanda vinaajiri watu wengi zaidi. Amesema kama pesa walizotumia kujenga majengo hayo wangezitumia kuanzisha viwanda ingekua na tija zaidi.

Hili wazo la kwamba haya mashirika yalipaswa kuwekeza kwenye viwanda niliwahi kulitoa miaka ya nyuma. Kwa bahati mbaya waliojenga majengo hayo wanaishi mijini na kwenye majengo hayo wana 10% zao. Niliishia kukebehiwa eti, wao wameona hela zao zinafaa kwenye majengo kwani eti kusimamia kiwanda kuna changamoto zake. Nilisema hata hayo majengo hayatalipa kwa hivyo kwani bei ya kukodisha hizo ofisi ni ghali sana na ni sehemu tu ya kutoa huduma na sio uzalishaji mali. Nchi yetu kwa sasa inatatizo la ulazalishaji mali na sio kutoa huduma. Kwa mfano wangeenda mahali wakajenga kiwanda na pembeni yake wakajenga green house, je wangetao ajira kiasi gani achia mbali uzalishaji mali wa enoe husika.
 
Leo Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya mashirika ya NSSF na PPF mjini Arusha ameyataka mashirika hayo kuwekeza kwenye viwanda kwani pamoja na mambo mengine viwanda vinaajiri watu wengi zaidi. Amesema kama pesa walizotumia kujenga majengo hayo wangezitumia kuanzisha viwanda ingekua na tija zaidi.
Hakuna shida
 
Aliwahi kusemaga haya mambo Dk. Dau kwa vile sis watanzania ni wazee wa figisu figisu, akaonekana hakuna alichoongea. Mifuko ya hifadhi ya jamii ina nguvu sana ya kuwekeza, na sio lazima iwe asilimia 100, inaweza kuwekeza asilimia 60, public ika own asilimia 40. Kwenye miradi inayohitaji uwekezaji mkubwa mifuko ya hifadh ingekuwa inaungana kufanya "Syndicated lending" ikiwezekana na public inachangia pia. Kama ikatokea mifuko ikashindwa kulipa wastaafu kutokana na liquidity basi kwa vile serikali ndo trustee anaweza kuingilia kutumia hata kwa policy tools za benki kuu.
Haya mambo yameongelewa mpaka basi, hakuna wa ku act, kila mtu anaogopa risk.
Uwekezaji unapofanywa na taasis za ndani, unakuza uchumi, unaongeza ajira na kupunguza umasikin, ukitegemea sana uwekezaji wa nje, faida wanayopata inatoka nje kwa namna ya uwekezaji kwenye securities, hivyo kudhoofisha thamani ya shilingi.
 
Ni lini Serikali italipa madeni yake kwenye mashirika hayo? Halafu yeye mbona hajaonesha seriousness kwenye viwanda.Bajeti yake ya Viwanda ametenga bilioni 81 halafu Recurrent ni Bilioni 41 (51%) na Iliyobaki 49% ndio ya Maendeleo.Ahubiri anachotenda sasa.
 
Viwanda vina risk kubwa kuliko majengo/real estate, na haya mashirika lazima yawekeze kwenye low risk investments ili kulinda hela za members wao.
Hata mimi najua hivyo japo kuna kipindi niliskia NSSF wanataka kuwekeza kwenye mradi wa chuma na kufua umeme, nikahisi kuna some conditions labda wanaruhusiwa. Wazo la Rais ni jema ila anatakiwa kufikiria kwa kina kwani mashirika ya hifadhi ya jamii ndio pekee yamebaki imara kwenye serikali ukiacha PSPF, Magu asije kumalizia na huko kwa kuyalazimisha kujiingiza kwenye high risk investments bila kujipanga na kuwasotesha wastafu.
 
Rais Magufuli amewaasa wenye dhamana ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa badala ya kujenga magorofa mjini ambayo yananeemesha matajiri wachache sasa wanatakiwa kujenga viwanda ili wananchi wengi wanufaike na ajira.

Amewapongeza kwa kupendezesha mji lakini akahoji uwezo wa wanyonge kupanga katika maghorofa hayo!
 
Rais Magufuli amewaasa wenye dhamana ya mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa badala ya kujenga magorofa mjini ambayo yananeemesha matajiri wachache sasa wanatakiwa kujenga viwanda ili wananchi wengi wanufaike na ajira.
Mzee Magufuli ni mbunifu sana ~~~ Jakaya Kikwete ( 2015).
 
Back
Top Bottom