Mambo yanayoendelea yananikumbusha story ya Pakistan, ukijiona uko kwenye group la wengi jiulize, sio muda wote mnakua correct, mnaweza kua very wrong.
Pakistan watu walijitokeza kumsupport jamaa moja aliyemuua bosi wake kwa kummiminia risasi nyingi wakidai kua alikua anatenda kazi ya Mungu, kesi yake lawyers zaidi ya 300 walitaka kuichukua kumtetea japo mwisho wa siku serikali ya Pakistan iliamuru jamaa auliwe, na kwenye msiba wake watu maelfu ya watu walijitokeza kumsupport. Sababu ya jamaa kumuua bosi wake ni kua bosi wake alimtetea mdada moja wa kikatoliki ambaye alishtakiwa kua kamkufuru mtume, kwa sababu ya wivu tu, mdada wa watu alikua ananawa mikono na wenzake yeye kama mkristo na wao kama waislamu wakawa wanamwita mchafu.
Ukiwa brainwashed kila kitu unachoambiwa unaamini 100% bila ku~question, ndiyo situation iliyopo sasa hivi, hivi tutajiitaje watu wenye elimu kama hatutakiwi ku~question kinachoendelea kama ni sahihi au la? Hao mafisadi mnaowaongelea sijui wako wapi, mbona hatujasikia mtu anafilisiwa au anatupwa jela? tunasikia story tu kua wanapambana na mafisadi, wapi?? Yule ambaye alikua anapiga milioni kadhaa kila dakika naye aliishia wapi maana hata jina walificha kumtaja. Naona biashara za watu innocent tu ndo zinafungwa bila kupewa sababu ya msingi zaidi ya neno "uchochezi"