Rais Magufuli ameanza vizuri, wananchi tumuunge mkono

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
IJUMAA iliyopita Rais John Magufuli alitimiza siku 100 tangu alipoapishwa Novemba 5, 2015 kushika wadhfa wa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano.

Wananchi wametoa maoni yao kuhusu mafanikio na changamoto zilizopo za utendaji wake kwa kipindi hiki kinachoweza kuonesha mwelekeo wake. Mara baada ya kuapishwa, Rais alimteua na baadaye kumwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kisha kazi ya kwanza aliyofanya ni kufanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Fedha ambapo aliwashangaza watu pale alipoamua kutembea kwa miguu kutoka Ikulu hadi wizarani hapo.

Baada ya hapo, Rais aliendelea kuunda serikali yake kwa kuteua viongozi na watendaji mbalimbali pamoja na kuunda Baraza la Mawaziri, kisha akaliapisha tayari kwa kuanza kazi. Katika maagizo yake kwa watendaji hao, alisisitiza jambo moja la Hapa Kazi Tu, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi kwa weledi na kujibu matatizo ya wananchi hasa kwa viongozi hao kuhakikisha wanafanya ziara zaidi maeneo ya vijijini kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi.

Mapema, Rais alikuwa ametoa agizo la kusitisha safari za nje kwa watumishi wote wa umma na iwapo watasafiri, ni lazima wapate kibali kutoka Ikulu, hiyo ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi na dhamira yake ya kubana matumizi ya serikali. Pamoja na hayo yapo mengi ambayo Rais Magufuli ameyafanya ndani ya siku 100 za kuwa madarakani ikiwemo kuanza utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.

Kwa upande wao wananchi tofauti wamezungumzia siku 100 za Rais Magufuli madarakani na wao kutoa maoni yao kwamba aliyoyafanya yameonekana na kinachotakiwa ni kumuunga mkono kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa weledi. Naomi James, mkazi wa Dar es Salaam anasema taifa lingempoteza kiongozi wa kweli kama asingechaguliwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

“Duh, ninawaza kila mara nikimuona Rais Magufuli kupitia vyombo vya habari akitoa maagizo au kuzungumzia jambo fulani, kama angekosa nafasi hii Tanzania tungekuwa tumefanya kosa kubwa sana, kweli ni kiongozi wa watu,” anasema James. Akizungumzia siku 100 za kuwa madarakani kwa Rais huyo, James anasema, Rais Magufuli si mtu wa kugeuka na kuna masuala mengi anaweza kuyasimamia kwa dhati na kila mmoja wetu akakubali kuwa huyu ni kiongozi anayesimamia haki na ana uchungu na wananchi wake.

Anatoa mfano wa kauli yake ya kukerwa na hujuma na wizi unaofanywa na baadhi ya watendaji ndani ya serikali, ambao wanaliibia taifa na kuwafanya Watanzania wengi kuishi maisha ya taabu. “Nakumbuka kwenye moja ya kampeni zake za kuwania urais nilikuwa Morogoro, alipopanda jukwaani alitetea wanyonge hadharani na alionesha moyoni jinsi alivyoumizwa na watu wanaoiibia serikali bila kujali kuwa kuna watu wanakosa mlo mmoja kwa siku. Aliahidi kupambana nao bila kigugumizi na ndivyo anavyofanya,” anasema James.

Hamisi Shomari, mkazi wa Mbezi Juu, Dar es Salaam, anasema Watanzania wengi sasa wanamini Rais Magufuli anaweza kurejesha bila wasiwasi usimamizi thabiti wa serikali na nidhamu ya utendaji ndani ya serikali. Anasema hayo yanawezekana kwa kuwa tangu kuapishwa kwake, kazi alizofanya hadi leo zinaonesha nidhamu ya kiongozi wa umma na amekuwa akitekeleza bila woga wala kumuonea mtu.

Shomari anasema, mbali ya matatizo ya watumishi wa umma kuhusu stahiki zao, wengi wao walifanya kazi kwa mazoea na kwamba hata jambo dogo la kutolea uamuzi lilifanywa au kutengenezewa ugumu ili mradi tu rushwa itolewe. “Cha ajabu hivi sasa mambo mengi yanakwenda na mengi tunapata suluhu ndani ya muda mfupi. Awali ulikuwa ukienda na shida yako ofisi ya umma, tambua kwamba utamaliza hata mwezi kupewa jibu labda kama utapenyeza rupia (fedha), lakini leo unaweza kupewa majibu ndani ya saa 24. Haya ni mabadiliko,” anasema Shomari.

Anasema kinachotakiwa kwa wananchi na watumishi wote bila kujali itikadi za vyama, dini na rangi zao ni kila mmoja kuwajibika kwenye nafasi yake, kama ni mkulima alime kwa tija, kama ni mwalimu afundishe kwa tija na mtumishi afanye kazi yake kwa weledi, ili kumsaidia Rais na nchi itaendelea. Mwananchi mwingine aliyetoa maoni yake ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kitila Mkumbo, ambaye anasema jitihada za Rais Magufuli zinaweza kuzaa matunda iwapo kila Mtanzania atabadilisha mtazamo wake wa kupenda vya bure, na badala yake afanye kazi kwa bidii.

“Rais ameanza vizuri, ila jitihada zake pekee hazitoshi. Jamii nzima ya Watanzania ibadilike, tuache kufanya vitu kwa mazoea na kupenda vya bure na utajiri wa haraka haraka, bali tupende kufanya kazi kwa bidii,” anabainisha Profesa Mkumbo. Anasema siku 100 za Rais Magufuli zina mambo mengi mazuri aliyotekeleza ingawa zipo changamoto kadhaa, lakini kwa hali ilivyo anaonesha ni mtu wa kutekeleza mambo kwa kasi zaidi tofauti na serikali zilizopita.

Wakizungumzia suala la elimu, wananchi waliohojiwa kwa ajili ya makala haya wanasema wamefurahishwa na uamuzi wa Rais Magufuli kuamua elimu kwa watoto wa Tanzania wanaosoma shule za serikali kuwa bure na wazazi wachangie sehemu yao mahitaji binafsi ya watoto wao. James Joachim, mkazi wa Temeke Wailes, Dar es Salaam anasema siku 100 za Rais Magufuli ofisini zimewafanya Watanzania wengi wamkubali kwa hatua alizokwishachukua na kwamba kwa siku zinazokuja Tanzania itapiga hatua kubwa ya maendeleo.

Akizungumzia elimu, Joachim anasema jambo hilo awali lilionekana kama kiini macho au propaganda ya kuomba kura kwenye majukwaa ya kisiasa, ila baada ya kuanza utekelezaji wake, anaamini yote aliyoahidi Rais, yatatekelezeka. Priscilla Kimario mfanyabiashara wa Rombo, Kilimanjaro anasema baadhi ya wananchi walishakata tamaa kufanya bishara nchini kutokana na vikwazo vingi na mazingira ya rushwa, lakini hivi sasa anafurahi mazingira ya biashara yamekuwa wazi, hayana mizengwe.

“Nimekuja Dar es Salaam kufunga mzigo Kariakoo, ninafanya biashara kwa amani kwani vikwazo vikiwemo masuala ya kodi ilikuwa vurugu tupu, ila sasa unalipa kodi una furaha, kwa maana hakuna kubughudhiwa kwa sababu wahusika wanaogopa kuwajibishwa,” anasema Kimario. Anasema utaratibu wa sasa wa makusanyo ni mzuri kwani hata takwimu zinazotolewa na mamlaka ya mapato nchini, zinaonesha kwamba kweli kodi zinazokusanywa zinafika serikalini na zinapangiwa kazi kulingana na umuhimu wake.

Kimario anasisitiza Watanzania wengine kutimiza wajibu wao, kama ni wa kulipa kodi walipe kwa wakati kwani takwimu zinatotangazwa za makusanyo ni nzuri. Anasema inawezekana Tanzania ikajiendesha yenyewe kwa kutegemea fedha za ndani kuliko kuomba nje fedha zenye masharti. Siku 100 za Rais Mafuguli zimekuwa na matokeo mazuri yanaonesha mwelekeo wa serikali katika kutimiza malengo endelevu ya Tanzania yenye neema tele na wananchi wengi wanaomba Serikali ya Awamu ya Tano isilegeze kamba.
 
Naunga mkono hoja, tumsupport kwa asilimia 100% ila pia tumkosoe anapoboronga.

Pasco
 
Sasa utamsuport vipi kwa 100% na wakati huo akiboronga umkosoe ? Asilimia za kumkosoa zitakua ngapi wakati zote umemaliza kwenye kumsupport
 
Kwako,mtu anaua upinzani,anavunja mikataba ya wafanya kazi,hafati sheria,amewapa nguv watu anaowateua yeye na sio wawaklishi wetu...uhmmm kaaanza vzr kwako
 
Sasa utamsuport vipi kwa 100% na wakati huo akiboronga umkosoe ? Asilimia za kumkosoa zitakua ngapi wakati zote umemaliza kwenye kumsupport
Mkuu Yamakaga, ku support ni jambo moja, na kukosoa ni jambo jingine. Mfano kwenye vita vya ufisadi na tumbua tumbua, naunga mkono kwa asilimia 100% Magufuli is doing the right thing and at the right time but in a wrong way. Hivyo kwenye nia na dhamira safi ya utumbuaji, support ni 100 %.

Lakini katika utekelezaji wa hiyo tumbua tumbua he is not doing it right. Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi za binaadamu ukiwemo udhallilishaji, kuna double standards etc.

Hivyo yeye kama kiongozi wetu Mkuu, he got to do the right thing at the right time and do it right. Kumkosoa does not mean kutomsupport.

Pasco
 
Back
Top Bottom