mkafrend
JF-Expert Member
- May 12, 2014
- 3,047
- 1,503
Watanzania, salaam!
Napenda kukiri kuwa mimi ni mwanachama wa CHAMA CHA MAPINDUZI tangu nilipoacha kazi katika Jeshi la Polisi mwaka 2010. Vilevile nimegombea ubunge jimbo la Buyungu kupitia CCM Mwaka 2010 na 2015 na mara zote kupata nafasi ya pili. Ni uchaguzi pekee wa mwaka 2015 niliopokonywa ushindi na baadhi ya viongozi wa chama na vyombo vingine.
Nimeona vizuri nianze na utangulizi huu ili kuondoa dhana dhaifu ya baadhi ya watu wanaodhani kuwa wanachama hatumshauri Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuhusu mambo yenye mshiko na taifa hili.
1. Kwa ujumla nina uelewa mkubwa na kanda ya ziwa na kanda ya kati kuliko maeneo mengine nchini. Hivyo, kuhusu maeneo haya naomba ifahamike kuwa wananchi (ingawa si wote) wana uhaba wa chakula. Serikali na CCM wasikae kimya wala kujifariji kuhusu hili. Tathmini ya haraka na ya kina ifanyike kisha mkakati wa kusaidia kaya zenye uhaba wa chakula ufanyike. Si vizuri kesho viripotiwe vifo vinavyotokana na njaa na ukosefu wa chakula. Njia pekee ni kupunguza matumizi kwenye baadhi ya sekta na fedha inayopatikana inunuwe chakula;
2. Ipo mtizamo wa baadhi ya viongozi kujenga dhana kuwa watakaosaidiwa chakula lazima kwanza waoneshe mashamba waliyolima yakakaushwa na jua - dhana hii ni dhaifu sana. Wakati wa uokozi kwenye majanga hatuwezi kuanza kuulizana mashamba kwa kuwa tutahatarisha maisha ya wananchi wetu (Je, watanzania si ndiyo walitupigia kura za kuitwa watawala??) kwenye matatizo kwa nini watengwe. Iwekwe mikakati kabambe itakayowasukuma kushiriki kilimo kipindi cha mvua lakini wakati huu wote wasaidiwe;
3. Kuhusu tetemeko la ardhi Kagera - Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza fedha zilizopatikana toka kwa wadau zitumike kujenga taasisi za umma. Hii ni nzuri kwa kiasi kidogo sana. Matumaini yangu ni kuwa fedha zile pamoja na kujenga taasisi za umma bado sehemu ya fedha hiyo inapaswa isaidie kaya zilizoathirika na tetemeko ambazo uwezo wake kifedha ni mdogo (Rejeeni picha za tetemeko ambazo Serikali na vyombo vya habari ilizisambaza - zilikuwa picha za wananchi waliokaa nje, hemani nk nk. Hii inaonesha kwamba wachangiaji waliguswa na picha hizo zilizosisimua na kusikitisha);
Hivyo, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli - aone kuwa kutosaidia wananchi wa Kagera wenye hali mbaya kiuchumi ni kuwadhurumu. Na hii itakuwa na mwitiko mbaya juu ya uwajibikaji wa Serikali kwa watu wake.
4. Ingawa hili halihusu matukio niliyotaja hapo juu lakini wasaidizi wake wa kiitifaki wahakikishe wanamsaidia kufanya rehearsal ya namna ya uhutubiaji wananchi na kimwandalia hotuba. Imetokea kwa siku za karibuni watu kumwelewa vibaya hasa pale anapotamka maneno kama KATERERO, BUTERANKUZI, NGONO, na kauli zilizonukuliwa akiwa Magu alipouliza kuwa ``Mnasema mna njaa sasa niingie jikoni niwapikie''.
Maneno haya si mazuri kuyasikia toka kwa kiongozi mkubwa wa kitaifa. Viongozi wa CCM mnaposhindwa kumshauri Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu masuala ya protokali na diplomasia za mazungumzo huenda chama chetu mkakizika kikiwa hai.
Huu ni ushauri tu kwa kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu wa chama na jirani yangu. Zuri nililoshauri lichukuweni na baya liwekeni akiba.
Msakila KABENDE
Mwanasiasa Mchanga - CCM
MUNGU IBARIKI TANZANIA!