G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,592
- 36,006
Kwanza aachie uhuru wa bunge na wabunge. Bunge lirudi kwenye mwanga na lionekane likijadili mijadala yake kwa uhuru kwelikweli.
Hatua ya pili baada ya hapo aruhusu katiba ya wananchi ipitishwe kwa maslahi ya wote. Katiba inayotoa usawa na isiyoegemea upande mmoja ambayo itatoa hukumu kwa kila mmoja wetu bila kupendelea mtu na kumuogopa mtu kuanzia rais aliyeko madarakani mpaka raia wa chini kabisa. Katiba itakayoweka nguzo kwenye kila mhimili na kuheshimiwa kwelikweli.
Hatua ya tatu sasa apeleke mikataba ifuatayo bungeni ikajadiliwe upya kwa uhuru wake na kutoa hukumu ya haki kwa kila mhusika
1) Mikataba yote ya madini
2) Mikataba yote ya gesi asilia
3) Mikataba yote ya manunuzi e. g ndege, vivuko na meli
4) Mikataba yote ya ujenzi mkubwa mfano reli, viwanja vikubwa vya ndege, madaraja makubwa
5) Mikataba yote ya uzalishaji wa nishati ya umeme.
Pia bunge lipitishe kila kitu kikubwa chenye maslahi ya taifa kabla hakijafanyiwa maamuzi ikiwemo kuthibitisha teuzi mbalimbali za kitaifa.
Tukiweza hapo kila mhimili wa dola utakuwa na integrity na kamwe hakutakuwa tena na ubabaishaji.
Akifanya hayo tutamuunga mkono na kamwe hatutageuka nyuma kwakuwa tutakuwa na imani kubwa kwake. Kinyume na hayo kamwe hatuungi mkono porojo zisizo na maana wala manufaa yoyote yale.