Rais Magufuli aitaka Israel kufungua ofisi ya ubalozi

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametoa wito kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kufungua ubalozi wa Israel hapa nchini.

Magufuli.jpg

Rais Magufuli alisema hayo Alhamisi hii alipokutana na balozi wa Israel hapa nchini, Yahel Vilan Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais alimhakikishia balozi huyo kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano wake na taifa hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu, Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba balozi huyo kupeleka ujumbe kwa Netanyau kuhusu nchi hiyo kufungua ofisi za ubalozi nchini.

Rais Magufuli amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani kwenye masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za jamii.

Aidha Rais Magufuli alisema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua Ubalozi Isarael na amemuomba Mhe Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini
 
Mimi nilijua wao ndio waadhirika kwa kufunga ubarozi wa Israel apo awali kumbe ni sisi maana inaonyesha wao hawajali mpaka tuwabembeleze.
 
Afanye atakavofanya msimamo wetu Tanzania kuhusu palestina na Israeli ni uleule aliowacha nyerere ...
Na sidhani waisrael kama wanaupenda
 
Ni Jambo Zuri

Tanzania kama nchi yenye amani, ni vizuri iwe na balozi zote yaani Ubalozi wa Palestina na Israeli

Hii itasaidia wakati mwingine kuwakutanisha mabalozi hao ili kujaribu kuwapatanisha.

Pia ni vizuri wapate fulsa wote wawili kujieleza kwanini hawataki kupatana haraka kama tunavyo wategemea

Kwani Ubalozi wa Palestina huwa una andaa mikutano inayotuonyesha jinsi wanavyoonewa na Israeli bila kuwasikiliza Waisraeli kwa upande wao.

Sasa hii ni fulsa kuwasikiliza na Waisraeli pia kwanini wanalalamikiwa na majirani zao.

Ni fulsa nzuri pia kwa nchi kupata ujuzi na utaalamu katika nyanja mbalimbali toka kwa Waisraeli ili tunufaike kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Kwasisi wengine tunawaheshimu Israeli kwani ni Taifa Teule la Mungu.

Ambarikiye Israeli naye Atabarikiwa.

Karibu Israeli.
 
Mkuu:
Hayo ni mawazo yako binafsi kama ulivyo bainisha.
Kwani haya mataifa mengine yame laaniwa. Na hayafai kuwepo pasi na kuwa Taifa teule.
Huko ni kujidhalilisha kwa kuukana uasilia wako kwa dhana ya Mungu kukosea.
 
Jamaa kapoteza mvuto hata kabla ya kutimiza miaka miwili. Nape kafungua milango ya "michano" ya live.
 
Back
Top Bottom