Rais Magufuli aguswa na utendaji wa Mbunge wa CUF, atamani angekuwa MwanaCCM

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,997
Rais Magufuli amempongeza Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maftaha Nachuma kwa utendaji kazi wake.

Rais Magufuli amesema, ''Pamoja na kwamba CCM tuliteleza kidogo lakini Mbunge huyu ni mchapakazi kweli''.

Aliendelea kusema, ''Tunahitaji Wabunge wa aina hii, tumezunguka naye katika ziara yangu na kujionea kazi zake anazozifanya, Yeye anataka maendeleo ya wananchi wake''.

Alimalizia kwa kusema, ''Kwa kweli ninakupongeza, hongera sana. Una moyo mzuri hata sura nzuri''.

''Inawezekana sura ikawa CUF CUF lakini moyo wake ni CCM, Ningetamani siku moja ukahamia CCM, ningefurahi sana'' alisema Rais.

Mbunge Maftaha alimshukuru Rais kwa kumpa ushirikiano wa karibu katika kazi zake za kuwatumikia wananchi wa Mtwara Mjini.

VIDEO:
 
Huyu angekuwa wa kundi lile la Pale mtaa wa Mtendeni angesifiwa hivi? Ukiona unasifiwa na mtu aliyemdhalilisha ndugu yako jana ujumbe unaopewa ni kwamba utengano ni nguvu na umoja ni udhaifu!!
haaahaa wahenga walisema" UKISIFIWA NA ADUI YAKO TAFAKARI MAPEMA MAANA UTAKUAVUMEKOSEA SEHEMU",,
 
Zamani ulikuwa hivi...
safi sana kamanda wetu,acha na huyu gamba ambae ata anufaiki na ufisadi wa magamba wenzie anabaki kuleta habari za uzushi tu! tunampa adhabu ya kumpuuza huyu gamba la mamba.
mtikisiko wa ubongo una muhusu

Lakini ghafla umekuwa hivi...

hahahahah atafukuzwa mara ya pili
 
Back
Top Bottom