Rais Magufuli afanya teuzi mbalimbali, Brigedia Jenerali Suleiman Mzee awa Kamishna Jenerali Mpya wa Magereza

Huyu msabato nyota inaendelea kuwaka, lakini nimegundua ni muadirifu kama ilivyokuwa kwa yule kijana (Daniel wa kwenye naandiko).

Kitu kingine nilichogundua waumini wa kisabato (baadhi) wakipewa nafasi wanafanya vizuri, namuona naibu kamishina wa tra, balozi Mpoki, kuna kamishina wa takukuru nk.
Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
 
Kuna kila sababu kubadili mifumo na mafunzo ya majeshi yetu,ikiwezekana yote yapigishe kozi chuo kimoja alafu baadae ndiyo zitoke post huyu aende Magereza huyu Polisi na huyu TISS,PCCB,JWTZ huyu Uhamiaji.Hii itafanya mafunzo yale ya msingi yafanane lakini pia kutoa lile gap la wengine kuonekana bora kuliko wengine au wa ovyo kuliko wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Magereza imejaa watu wa aina gani? Wamesomaje? Wanaendelezwa au kujiendeleza vip from time to time?
Rais amefanya vema. Labda wataanza sasa kuamka
 
Huyu msabato nyota inaendelea kuwaka, lakini nimegundua ni muadirifu kama ilivyokuwa kwa yule kijana (Daniel wa kwenye naandiko).

Kitu kingine nilichogundua waumini wa kisabato (baadhi) wakipewa nafasi wanafanya vizuri, namuona naibu kamishina wa tra, balozi Mpoki, kuna kamishina wa takukuru nk.
Sawa tumejua na wewe msabato.
 
Ukiangalia mjadala utajua wtz ni wachovu kiakili,,,Nasema tena hakuna watu wakakamavu,shupavu,wazalendo sema serikali huwa inalidumaza hilo jeshi kutokana na kulipa bajeti ndogo kupita kiasi,hata huyu mjwtz asipopewa mafungu ya kuijenga na kuliendeleza jeshi LA magereza atafeli tu,,,,tuwape fedha za kutosha watekeleze miradi,,,kuhusu mafunzo ya uaskari sina wasiwasi na magereza wako vizuri tena mno
 
Unaweza kujiuliza sijui TPDF wao wanawezaje kujitengeneza kuwa vile alafu hawa majeshi mengine wanashindwaje? Ukimuweka hata Service Man/Girl wa JKT na askari wa vyombo vingine tofauti na TPDF utaona kabisa utofauti wao SM/SG ana uwezo mkubwa sana hasa kwenye utimamu wa mwili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazima tofauti iwepo,JKT,JW ni watu wa kutii amri.Polisi ni kutii amri na kuangalia sheria,magereza ni kurekebisha tabia na kuadhibu.Ni lazima kozi zitofautiane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magereza kwenda zimamoto sikubaliani kabisaaaaa!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa tanzania hakuna shida hatufanyi kazi kulingana na utaalam wa mtu. Tanzania tunafanya kazi kulingana na status mfano dr., prof., nk hivyo mtukufu ameona kila kitu kinawezekana hata upande wa jeshi baadae anaweza akahamua wabadilishane askari magereza wote waende mfano tpdf au JW na wale wa tpdf/JW wakawe askari magereza!!
 
fire bado wadogo hawana watu wengi wenye vyeo vya DCP wala CP kama majeshi mengine
Wana deputy commissioner wakutosha kwa sasa labda kwa upande wa makamishna (CF) wapo kama watatu. Ila niliwahi ona mahala kamishna jenerali wa zimamoto atatokea polisi ama magereza
 
Ukiangalia mjadala utajua wtz ni wachovu kiakili,,,Nasema tena hakuna watu wakakamavu,shupavu,wazalendo sema serikali huwa inalidumaza hilo jeshi kutokana na kulipa bajeti ndogo kupita kiasi,hata huyu mjwtz asipopewa mafungu ya kuijenga na kuliendeleza jeshi LA magereza atafeli tu,,,,tuwape fedha za kutosha watekeleze miradi,,,kuhusu mafunzo ya uaskari sina wasiwasi na magereza wako vizuri tena mno
wewe ndio umeongea point tupu mkuu.. ukwel ndio huo MAGEREZA wana bajeti ndogo sana ukilinganisha hata na POLISI, kuna kampeni wameanzisha magereza sasa ya ujenzi wa nyumba pamoja na kilimo kikubwa ili kujitegemea kwa chakula lakini vitendea kazi hakuna unakuta gereza zima tractor lipo moja tena bovu la enzi za mkapa huko ilhali ukieda JKT unakuta kuna tractor zaidi ya 7 kwa kambi moja tu. Sahv wanajenga nyumba baadhi ya magereza lakini kwa shida sina yaan nyumba zinafika usawa wa renta zinakaa miaka zaidi ya miwili zinasubiri fungu tu na halitoki.. JPM kuna mawwili huenda dharau zimejaa au wasaidizi wake hawamuelezi ukweli.. kuna mdau mmoja hapo juu kasema kwamba ukimchukua SERVICEMAN wa JKT eti ni tofauti kabisa na askari wa cheon cha chini wa majeshi mengine nikammpuuza tu wakati kwasasa depo kama 4 zilizopita zote askari wa magereza ndio haohao waliokuwa SERVICEMAN kwa miaka miwili huko kambi mbalimbali za JKT... watoe pesa ndani ya jeshi afu ndio tuje tuhukumu...
 
Wana deputy commissioner wakutosha kwa sasa labda kwa upande wa makamishna (CF) wapo kama watatu. Ila niliwahi ona mahala kamishna jenerali wa zimamoto atatokea polisi ama magereza
labda kwa sasa ila hata hao ukifatilia ndani utakuta hawakuwa zimamoto rejea yule kamishna wa fedha na mipango kama bado yupo anaitwa MBARAKA SEMWANZA alitoka MAGEREZA alikuwa mkuu wa chuo pale UKONGA
 
labda kwa sasa ila hata hao ukifatilia ndani utakuta hawakuwa zimamoto rejea yule kamishna wa fedha na mipango kama bado yupo anaitwa MBARAKA SEMWANZA alitoka MAGEREZA alikuwa mkuu wa chuo pale UKONGA
Ukimtoa semwanza waliobaki wote ni wazimamoto
 
Rasmi ile kauli ya Mtukufu kuwa ipo siku atateua Mwanajeshi kuwa Kamishina Jenerali wa Magereza imetimia leo Baada ya kumteua Brigedia Jenerali Suleiman Mzee kutoka JWTZ kuwa Kamishina Jenareali wa Magereza na Naibu Kamishina John Masunga Toka Magereza kuwa Kamishina Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji!!
View attachment 1342600
Brigedia Jenerali Suleiman Mzee Kamishna Jenerali Mpya wa Magereza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2020 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Wizara, Mahakama, Mikoa na Majeshi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amewataja walioteuliwa kama ifuatavyo;

Wizara.

Rais Magufuli amemteua Bi. Mary Gasper Makondo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mary Gasper Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Anachukua nafasi ya Bi. Doroth Mwanyika ambaye amestaafu.

2Rais Magufuli amemtea Dkt. Hassan Abbas kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Anachukua nafasi ya Bi. Suzan Mlawi ambaye amestaafu.

Rais Magufuli amemteua Prof. Riziki Silas Shemdoe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huo Prof. Riziki Silas Shemdoe alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Prof. Joseph Buchweishaija ambaye amestaafu.

Rais Magufuli amemteua Bi. Zena Ahmed Said kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bi. Zena Ahmed Said alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala. Anachukua nafasi ya Dkt. Hamis Mwinyimvua ambaye amestaafu.

Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Kadio kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Christopher Kadio alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya Mej. Jen Jacob Kingu ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais Magufuli amemteua Bw. Leonard R. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huo Bw. Leonard R. Masanja alikuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala.
Mikoa.

Rais Magufuli ameteua Bi. Judica Haikase Omary kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga.
Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Mashauri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
Rais Magufuli amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
Majeshi.

Rais Magufuli amemteua Brig. Jen. Suleiman Mungiya Mzee kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza. Brig. Jen. Suleiman Munyiya Mzee anachukua nafasi ya Phaustine Kasike ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Rais Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) John William Hasunga kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. DCP John William Hasunga anachukua nafasi ya Thobias Andengenye ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Ardhi.

Rais Magufuli amemteua Bw. Nathaniel Mathew Nhonge kuwa Kamishna wa Ardhi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Nathaniel Mathew Nhonge alikuwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
Mahakama.

Rais Magufuli amemteua Bw. Wilbert M. Chuma kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama.
Rais Magufuli amemteua Bw. Kelvin D. Mhina kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani.
Rais Magufuli amemteua Bi. Shamira S. Sarwat kuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
==========

Rais Magufuli amewateua Jaji Dkt. Gerald Ndika, Wakili – Julius Kalolo Bundala na Wakili – Genoveva M. Kato kuwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hawa itatangazwa baadaye.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Dar es Salaam

31 Januari, 2020
View attachment 1342867View attachment 1342868
Hivi katika masuala ya kidiplomasia hakuna wabobezi wa masuala hayo kuwa ndiyo wenye kustahili kuteuliwa kuwa mabalozi? Naona kuna kamtindo kametokea ktk awamu hii kwa watumbuliwa kwenye nafasi mbalimbali, tena wengi wao wakiwa hawana hata wasifu wenye kuendana na masuala ya kidiplomasia kupoozwa kupitia nafasi hizo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: JMF
Back
Top Bottom