Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri: Waziri Mwigulu atemwa, Lugola aula. Mbarawa ahamishwa

Nimesoma mahali akitajwa Mwalasusa kuwa alihusika na kina DAB katika maandalizi ya nyaraka hizo.
Mungu aniepushe nisije sema maneno mabaya dhidi ya mtumishi wake.
Lakini kwa nafasi aliyo kwisha kufikia Mwalasusa basi kujihusisha na mikono michafu kama ya DAB haki mtumishi anautafuta mwisho mbaya sana.
Nakumbuka yaliyo mkuta Mwalasusa ni sawa na yaliyopata mtokea Askofu mmoja Wa KKKT kule nadhani Mtwara. Kuleta mtengemano na watumishi na waumini aliomba radhi kwa kulala kifudifudi ndani ya kanisa. Jee alivyunja heshima yake kwa jamii? Hapana bali alijiongezea utukufu mbele za waumini na mbele za Mungu.
Mie muumini wa Kiluteri, namuheshimu sana Askofu Mwalasusa, namuomba ageuke na kumtazama kristo kisha anawe hiyo mikono kama amepata kuihusisha kazi yeyote na DAB. Huyo ni chukizo, na chukizo lolote mbele ya wanadamu linaweza pia kuwa chukizo mbele ya Mungu.
 
Mbona naona barua ya maelezo ya sauti kubwa tu sijaona barua ya ikulu ikimwendea mwigulu kama kuna kitu kakiuka afukuzwe?
 

Attachments

  • barua ikulu.jpg
    barua ikulu.jpg
    24.7 KB · Views: 33
Barua yenyewe fake
1. Angalia kumbukumbu namba
2. Taasisi ya asha migiro imeingiaje
3. Namba ya chini ya sanduku la posta ina maana gani
4. Barua haina hata sahihi
5. Yani tarehe na kumbukumbu namba zipo mstari mmoja, huu ni uongo.
6. Umbali kati ya mstari wa kumbukumbu namba na kmb namba yenyewe. Yan mtu akiweka huo mstar ina maana kua kumb namba ingejazwa kwa mkono ila kwa hii barua sio. Ni hayo tu
 
Ngurumo huwa hawezi ishi kabisa bila kumtaja Bashite,
Bashite anaishi maisha yake akipokea mshahara wa RC wakati Ngurumo anaishi kwa kutegemea labda miaka miwili mbele naye atapata bahati ya kuingia kwny universal basic income ya Finland
 
Tazama kiambatanisho cha Barua ya Ikulu.
Siamini macho yangu kama Askofu Malasusa ameweza kuwakana wana kondoo na hatimaye kumtumikia shetani. Ila akumbuke kuwa shetani humthamini mtumwa wake pale anapoona anatetea maslahi yake jukumu likiisha mahusiano yanaishia pale mfano Cardinal Pengo anaonekana kama karatasi la chooni baada ya kumaliza muda wake wa kumtumikia shetani. "Ubaya una mwisho"
 
Mods huu upuuzi mwingine hivi mnauruhusu ku-trend humu kwenye jukwaa la watu wazima? Huu udaku ni wa instagram siyo humu ambapo kuna wahariri wa threads. Pls Mods ipeni thamani JF yetu
 
Screen-Shot-2017-03-01-at-09.33.31.png
Barua yenyewe fake
1. Angalia kumbukumbu namba
2. Taasisi ya asha migiro imeingiaje
3. Namba ya chini ya sanduku la posta ina maana gani
4. Barua haina hata sahihi
5. Yani tarehe na kumbukumbu namba zipo mstari mmoja, huu ni uongo.
6. Umbali kati ya mstari wa kumbukumbu namba na kmb namba yenyewe. Yan mtu akiweka huo mstar ina maana kua kumb namba ingejazwa kwa mkono ila kwa hii barua sio. Ni hayo tu
"taasisi ya asha rose migiro" hiyo ni sehemu ya anuani ya zilipo ofisi za wizara ya mambo ya ndani kule UDOM,
baadhi ya vitu vimefichwa pengine ili kumlinda aliyeivujisha ila barua ni authentic
 
Mungu atusaidie tufike salama huko tunako tarajia kufika
Kuna jamaa huku uswahili kinondoni mkwajuni mafere ananunua nyumba nyingi na kuzijenga upya ana ukwasi wa ajabu anafahamika kama Ndg Joachim na pia wanadai yuko Kitengo kikuu ndio huyu anayetajwa hapa nini. Bonge la mtu hivi.
 
Tazama kiambatanisho cha Barua ya Ikulu.

Kinachoshangaza mnahangaika na kusumbuka kumjadili huku mkimuonea huruma ya ' Kinafiki ' Mwigulu Nchemba lakini Yeye mwenzenu ndiyo Kwanza anakipenda Chama chetu cha CCM bila ya ' Kinyongo ' chochote. Halafu nadhani ipo haja sasa Watu waelewe nini maana ya Ikulu kama Taasisi kuliko kila siku ' Wapuuzi ' fulani kuibuka na ' Propaganda ' za ' Kipumbavu ' kabisa ili mradi tu waweze ' Kuichafua ' Serikali ya Rais Dkt. Magufuli.

Hakuna Ikulu ambayo ina Watu makini na weledi wanaweza kufanya aina hii ya ' Ujinga ' ambao tunaaminishwa hapa. Mwacheni Rais Dkt. Magufuli atutumikie Sisi ambao tulimwamini na tulimpigia ' Kura ' zetu mwaka 2015 na nyie ambao mna ' chuki ' nae subirini ifike mwaka 2020 kama Mtu wenu mnayempenda / mnayemtaka ' akibahatika ' ataupata huo Urais japo mpaka sasa nikitizama huko ' Upinzani ' sijaona ' a right Candidate ' wa siku moja Yeye kuja kuwa ' our Head of State '.

Mnaidhalilisha mno ' hadhi ' ya ' Ikulu ' na sijui mnafaidika na nini labda.
 
Siku kama 4 zilizopita nilianzisha Uzi kama huu,kuhusiana na hiyo barua,hata sekunde haikuchukua wakawa wameisha uondoa sijui Leo itakuwaje
mambo yote siku hizi ni JamiiForums.com, hii jf ishakuwa taasisi ya ccm, hawataki uiseme ccm au serikali vibaya
 
Back
Top Bottom