wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,549
Sidhani kama ushauri wangu kwako itakuwa ni kukukosea heshima,kwenye ukweli tuseme tu ukweli bila kupepesa macho.
Mh Rais umekuwa ukiihadaa Dunia kwamba chama chako CCM pamoja na wewe binafsi mnapendwa mno na watanzania jambo ambalo si kweli hata kidogo.
Ulipoingia madarakani ulipiga marufuku mikutano ya kisiasa ukidai kwamba huu ni wakati wa kufanya kazi na siasa zingefanyika 2020.
Cha ajabu wewe na chama chako ndo peke yenu mnafanya siasa kwa kuwarubuni wapinzani na kisha serikali inatumia pesa nyingi mno kufanya uchaguzi feki wa marudio,uchaguzi wa kuihadaa Dunia kwamba Tanzania kuna Demokrasia ,kumbe Demokrasia ya Tanzania ni kuipenda CCM.
Rejea kauli yako ,nakunukuu"Nakulipa mshahara,nimekupa gari na nyumba halafu unamtangaza mpinzani kashinda".
Mh Rais,wewe ni Baba wa watoto wote,lakini unabagua wanao.
Pesa zinazotumika kwenye chaguzi feki za marudio zilipaswa kutumika hata kutunza watoto yatima,watoto wa mitaani,wagonjwa na wajane,Mungu hawezi kubariki taifa lililojaa hila na chuki kwa wengine.
Rejea Habari ya Kaini na Abel,ndicho kitaikuta Tanzania.
Mungu hubariki taifa lenye upendo na mshikamano wa utakatifu,na siyo tambiko la mwenge na kuwaambia watu warejee CCM,CCM ndo kitu gani? CHADEMA ndo kitu gani?haya madude yamekuja juzi tu,Tanzania ilikuwepo na itakuwepo hata baada ya haya madude kutoweka.