Rais Magufuli aanza kubadilika kiutendaji na usemaji

Rais Magufuli aanza kubadilika kiutendaji na usemaji

Amesema ukiona au kusikia mtu analalamika dhidi ya Serikali yake basi ujue ni muathirika wa mfumo butu uliominywa dhidi yake! Mianya ya rushwa na fedha chafu kuminywa!Good enough ni kuwa sasa mnamfuatilia JPM kuliko mtu mwingine yeyote na kizuri zaidi mnasambaza taarifa zake kwa kasi zaidi regardless mnazipindishaje! Mnasaidia kuwa julisha waTanzania kuwa JPM anapiga mzigo Go JPM Go umewashika pabaya Baba!

Mgawa rushwa kama Mnyeti.
 
Yap haifanyi biashara popote pale wanapofanya hizo shughuli zao ndio dhana ya uzalishaji inaingia hapo
Inawezekana aliesema hiyo alimaanisha uzalishaji in the form of revenue!
lakini tujiulize zaidi.serikali inapeleka fedha kiasi gani za bajeti ya maendeleo huko kwenye halmashauri? hivi ni vichekesho kutegemea uzalishaji uongezeke wakati bajeti ya fedha za maendeleo haifiki hata 30%
 
Tufungue mjadala hapa kwenye hiyo hoja wakati huo wazalishaji(wawekezaji)wanafunga bishara zao


Serikali haina production ya aina yeyeote ile kuweza kuihusisha na maslahi ya watumishi wake. Pengine altaka kumaanisha productivity....sijui. Lakina hata kama alitalka kumaanisha efficiency ambayo ndiyo appropriate bado anakosea. Hii ni lazima.uipime kuipata. Sasa kwa mfumo huu wa utumishi wa umma tulionao ni kazi sana kupima efficiency. Ndio maana hata kwa kutekeleza majukumu ya kawaida kabisa mtumishi wa umma (na serikali yenyewe) anataka kupongezwa!
 
hapo umenena lakini ipo siku atagundua mwanae bashite anamuhalibia atajiona muuuuuuuu
 
Bora maskini wa jamii ya rohingya huko Myanmar kuliko maskini wa fikra kama wewe. Hii nchi babu yenu Mamvi asingeiweza kuirejeshea misingi imara na endelevu ya uwajibikaji. Maendeleo huja hatua kwa hatua. Uozo uliokuwepo ulimlazimisha (na kwa nia ya dhati kabisa)kuwa MAGUFULI wa aina hiyo. Wahenga walisema ukicheka na nyani utavuna mabua. Nyumbu mlivyo na akili za kukaririshwa mmesahau ghafla mliyokuwa mnatuhubiria kwamba mkipewa nchi mtafanya mengi ambayo kimsingi MAGUFULI ndio anafanya. Sasa mmegeuka tena na kubeza kila kitu. Kwa taarifa yenu si lumumba wala wananchi wanyonge pekee wanaotamani ukali uongezeke bali ni dunia mzima wanautamani uongozi huu
Tupia basi nakala ya utafiti ulofanyika kuhusu "hiyo" taarifa yako.
 
Nyie 12000 mnahangaika sana na hamuwezi kumpenda
 
Mshahara mil 9
1.Hauna makato ya aina yeyote
2.Kila kitu bure kuanzia chakula,malazi,usafiri,matibabu na familia pia.
Then the rests wanaambiwa mahudumia wananchi,why hiyo mil 9 isiwe inatolew kila mwezi kuhudumia WANANCHI?
 
At least ameongea kwamba haongezi mishahara hadi uzalishaji uongezeke this is a sign kwamba uzalishaji umeshuka hivyo ukuaji ni sawasawa na hakuna watumishi wanataka waambiwe ukweli sio longolongo za uhakiki maana wanajua nyongeza hizo sio zawadi ni haki yao alafu danadana kila siku ari ya kumsaidia kuwatumikia watanzania inashuka
[HASHTAG]#WATUMISHIFUNGAMKANDA[/HASHTAG]
Nadhan si uzalishaji hapo NI MAKUSANYO yameshuka,
 
Kagundua kua Watanzania wameanza kumchoka. Pitia fb instra na mitandao mingine ya kijamii then soma comment uone. Zaidi ya 70% ya comment kwenye post nyingi zinaonyesha hazimkubali kabisa
Ni sawa usemavyo,lakini tambua huko kuna asilimia chache sana,pia uwezekano wa watu kuwa na account na device zaidi ya moja ni mkubwa,refer tambo za ukawa maeneo ya mjini
 
Nampenda Magufuli, ila sijamuelewa eneo moja, anasema wamefukuza wafanyakazi waliofoji vyeti akawasema weee mpaka akafikia kusema mitandaoni wanaomsema ni wale 12,000, wakati fulani shoga yangu alikuja kunionesha mange anavotukana nikaona anawafuasi million moja na laki tatu!

PAle pale kawaongelea walofoji vyeti halafu ANAMSIFIA MTU ANAEDHANIWA kuwa mmoja wa hao! Kama Baba naona amekosea! Baba wa Taifa anatakiwa kuwatreat watoto wake wote sawa! naona hafanyi haki kwa hili!
 
Back
Top Bottom