Rais Magufuli "A One Man Army"

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
16,081
14,116
Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu!!

Kila nikimsikia Rais akiongea amekuwa anaonyesha uchungu mkubwa kwa nchi na hasa kwenye ufujaji wa pesa za umma na uwajibikaji. Kwa hili inabidi Watanzania wote kwa pamoja tumuunge mkono. Kama kutumbuliwa tu kweli kuna majipu yametumbuliwa hata kama wengine watayaita vichunusi ........... na bado kazi inaendelea!!

Lakini kila mazuri wakati mwingine yatakuwa na mapungufu yake. Kwa mtizamo wangu awamu ya tano kila muda unavyosogea mbele unazidi kuona ni jinsi gani kila kinachoendelea nchini kinamtegemea Rais pake yake. Mambo yanayo ibuka kila siku mitandaoni ya kila siku kama ya ukweli basi kazi anayo. No wonder imebidi achukue likizo kabla hata ya miezi sita kwisha na Kadnari Pengo anadai Rais kesha anza kuona ugumu wa kazi yake. Labda hapati msaada wa kutosha kutoka kwa Wasaidizi na Washauri wake. Ile speed ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais siioni tena. May be vyombo vya habari na mitandao wameacha kutuhabarisha.

Ni muda sasa sijasikia cha Makamba, Mwigulu au Kipenzi cha Rais Makonda ...... Kigwangalla ndiye naona anajitutumua kuliko hata Waziri wake ingawa watu wanadai anaboronga!! Au inawezekana viongozi wanaogopa panga lisiwaangukie kama Mama Kilango-Malecela!!?

Kwenye movie za zamani (kwa wale wenye umri wetu) mtamkumbuka Sylvester Stallone (Rambo) au Arnold Schwarzenegger na picha zao za One Man Army .... Jamaa mmoja alikuwa wanaweza kupiga kikosi kizima cha jeshi saa nyingine bila hata silaha!!

Tumuombee Rais wetu afanikiwe katika vita hii ............ hata kama atapigana peke yake!!

Magufuli ..................... A One Man Army!!!!!
 
Go Magufuli go ..................... A One Man Army!!!!!
Well said, tumuombee kwa Mungu ili amuongezee nguvu na ni kweli inaonekana ni jeshi la mtu mmoja na kwa maana hiyo sterling huwa hafi mpaka mwisho picha na mwisho huwa ndio shujaa wa filamu
 
Ikumbukwe kuwa kwa sasa mawaziri wameanza kuweka shamba katika maandalizi bajeti baada ya kufyeka poli lililokuwa limejaa wezi, wavivu na wabadhilifu wa mali za umma katika wizara zao.

Tatizo kubwa Tanzania ni wivu/husida au mlengo wa itikadi/vyama

Viongozi wakionekana kwenye media kila mara, basi utasikia wenye wivu wanasema hii serikali inayofanya kazi mbele ya media.

Kwa sasa hawaonekani, utasikia tena wanasema kasi ya kutumbua majipu imepungua au imewashinda.

Damned if they do, damned if they don't.
 
Mkuu nashangaa sasa hivi wananchi wanachanganyikiwa na Magufuli.. Kwa jinsi bajeti ilivyosukwa ukianza utekelezaji naamini watanzania watapagawa kabisa na Magufuli maana kajopanga haswa kuwafikia wananchi na kuwavusha.
 
Labda malaika mmoja kaingia kwenye kundi la shetani! Hii manake nini? Ni rahisi malaika kubadilika kuwa shetani kuliko kubadili kundi la shetani kuwa malaika! Muda utatuambia!
 
Mh.Magufuri yupo vizuri ilitakiwa wasomi mbali mbali watoe michanganuo yao ya kujenga Nchi kwa Maendeleo ya baadae na si ivi wapo mbali wakimkosoa tuu..naona Mh. ana dhamira ya kweli ya kweli ya Maendeleo kwa Watanzania wote ingawaje wapo wachache wanapenda wawe wao tuu wakila keki ya Taifa...
 
Washairi mna miluzi mingi.... Miluzi mingi humpoteza mbwa!!

Hakuna MTU anajenga nchi peke yake dunia hii....
Mwache ajenge hata ikipolomoka ni sawa tu. Kwani JK alivyowakaribisha mjenge naye mlijenga nini kama si kumbomoa mwenyewe, sasa leo mnajifanya kuleta kujua tena, mnapiga chapuo ili naye awaite mfanye tena mayenu. Magufuri hayuko na wale unaowapenda wewe ila anao wale alioamua kuwa nao yeye.
 
Taifa la watu milioni 50
lenye wasomi tele ujibebeshe mzigo wa kuongoza peke yako ni kukosa busara....
huwezi wewe kuwa ndo standard ya kila kitu
lazima watu wengine wafanye kazi na standards ziwepo wazi zijulikane...

kuna watu wanamdanganya Magufuli kuwa atavaa viatu vya Nyerere....
hapo ndo itakuwa his downfall.....
 
Ikumbukwe kuwa kwa sasa mawaziri wameanza kuweka shamba katika maandalizi bajeti baada ya kufyeka poli lililokuwa limejaa wezi, wavivu na wabadhilifu wa mali za umma katika wizara zao.

Tatizo kubwa Tanzania ni wivu/husida au mlengo wa itikadi/vyama

Viongozi wakionekana kwenye media kila mara, basi utasikia wenye wivu wanasema hii serikali inayofanya kazi mbele ya media.

Kwa sasa hawaonekani, utasikia tena wanasema kasi ya kutumbua majipu imepungua au imewashinda.

Damned if they do, damned if they don't.
Hata Simbachawene mpigaji maarufu na huyu aliyepiga za Lugumi na kumteua partner wake kibiashara kuongoza NIDA naye alikuwa anafyeka msitu....

Lazima tukubali kuwa kwenye msafara wa Mamba na Kenge wamo, tumsaidie raisi kuwaondosha kenge kwenye msafara wa mamba kwani kila mamba jike akitaga mayai makenge yatakuwa yanakula. Na mengine hayana adabu yatakula hata vitoto vya Mamba.

Mshaurini JPM alete katiba ya wananchi imsaidie kupata CREAM ya nchi hii imsaidie kuleta maendeleo. Hakuna mwanasiasa msafi hapa Tanzania bila kujali chama. Waziri asingelazimika kuwa mbunge
 
Tunafunga na kukesha tukimuombea sana tu muungwana ila na yeye pia ana part yake,Asi tuangushe kama alivo tuahidi,mpaka sasa mwendo sio mbaya ila kuna breaki hapa na pale pengine ndio kuvuta spidi ya take-off, kila la heri Kiongozi wetu mpendwa tuko nawe kiroho.
 
Tumuombee
Kwa kweli maombi yana hitajika sana, ila linapo kuja swala eti anaongoza peke yake hali kuna wengine chini yake ina nishangaza kidogo na kuni kumbusha the late Bingu wa Mutharika aliye kuwa Malawi alivyo pambana na ubadhilifu ulio lelewa na chama chake hadi kumfungulia kesi mtangulizi wake Bakili Muluzi aliye kuwa ame jijenga na kulindwa na chama,Mutharika alipo ona gozigozi kwenye chama na katiba ina mruhusu akaanzisha chama chake juu kwa juu na alipambana na akawanyoosha hadi Mungu alipo ridhika na kazi aliyo mtuma akatwaa kiumbe wake.
 
Tatizo la siasa za Afrika ni kwamba zinazungukia watu badala ya kuzungukia sera.
 
Hapo sasa ................!!

Tanzania kila Rais anapokuja anakuja na vitu vyake vipya utafikiri ni chama kimebadilika. Wakati wa kampeni nakumbuka Magufuli alikuwa anawagawia manifesto ya CCM wagombea kila alikokuwa anapita lakini leo inaonekana kama anafanya mambo yake binafsi!!
 
Pamoja na sifa zote hizi lakini hajengi mfumo na shida itakuja kuwa likitokea lolote kutakuwa na ombwe kubwa anachojenga ni mfumo wa kidikteta una mazuri na mabaya yake
 
Hapo sasa ................!!

Tanzania kila Rais anapokuja anakuja na vitu vyake vipya utafikiri ni chama kimebadilika. Wakati wa kampeni nakumbuka Magufuli alikuwa anawagawia manifesto ya CCM wagombea kila alikokuwa anapita lakini leo inaonekana kama anafanya mambo yake binafsi!!
Magufuli alipokwenda kuchukua fomu za kugombea urais alikuwa mpole kweli.

Waandishi walipomuuliza mipango yake, unlike watu kama Makamba waliosema mengi, yeye alikataa kusema na kudokeza tu kwamba atafanya yale yaliyomo katika mipango ya chama.

Labda kwa sababu alikuwa haja formulate priorities mwenyewe, au aliogopa kuzisema.
 
Back
Top Bottom