RAIS MAGUFULI: 2019 MWAKA WA KAZI

RAIS MAGUFULI: 2019 MWAKA WA KAZI

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
8-4-950x634.jpg


RAIS John Magufuli amewataka Watanzania kuufanya Mwaka Mpya wa 2019 kuwa mwaka wa kazi kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali kama vile kilimo, biashara, uvuvi na nyinginezo ili kujiletea maendeleo. Alitoa mwito huo kwenye mkesha wa Kitaifa wa kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema Tanzania imebarikiwa kuwa nchi yenye amani, upendo na utulivu katika awamu zote, hivyo wananchi hawana budi kuitumia fursa hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo.

Alisema kutokana na kuimarika kwa hali ya amani, utulivu na upendo nchini, serikali yake imeamua kupambana na kuondoa kero mbali mbali kama vile rushwa, dawa za kulevya na nyinginezo ili kuinua hali za maisha ya wananchi wanyonge. Alisema mkesha huo wa kitaifa ni fursa muhimu kwa Watanzania kujitathimini kila mwaka kuona malengo waliyojiwekea kama taifa au mtu mmoja mmoja yamefanikiwa na kwa kiwango gani.

Aidha, alisema katika miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano kumekuwa na mkakati wa kujenga na kuimarisha uchumi wa Tanzania kwa kujenga miundombinu mbalimbali ya kiuchumi. Aliitaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, ujenzi wa bwawa kubwa la kuzalisha umeme wa Mto wa Ruji utakaozalisha zaidi ya megawati 2,000 pamoja na ujenzi wa barabara maeneo mbali mbali nchini. Kwa mujibu wake, ujenzi wa miundombinu hiyo inatokana na dhamira ya serikali kutimiza ndoto ya kuwa na Tanzania ya viwanda pamoja na kukia uchumi wa kati na kuwapunguzia gharama za maisha wananchi.

“Hivi sasa huduma za jamii kama vile afya na elimu zinazidi kuimarishwa; serikali inajenga hospitali za wilaya kwenye wilaya zote ambazo hazikuwa na hospitali hizo, inaimarisha upatikanaji wa dawa hospitalini, kutoa elimu bure pamoja na kuimarisha huduma mbalimbali za jamii,” alieleza. Mbali na ujumbe huo wa Rais wa Mwaka Mpya, baadhi ya viongozi wa dini pia walisisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu uliopo nchini. Msaidizi wa Askofu wa Kanisa Kuu la KKKT-DMP Azania Front jijini Dar es Salaam, Chediel Lwiza alisema Taifa halina budi kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwapatia Watanzania tunu ya amani, lakini pia kuwaweka pamoja kwa utulivu kama taifa, familia, vikundi na mtu mmoja mmoja.

“Tuendelee kuiombea nchi katika Mwaka Mpya wa 2019 ili iendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano; tuwajibike katika jamii, serikalini, nyumba za ibada pasipo kushurutishwa katika kutimiza kazi tunazopaswa kuzifanya,” alieleza Lwiza. Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum alisema katika mwaka mpya wa 2019, Watanzania hawana budi kujipanga kwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na nidhamu kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo pamoja na kuendelea kutunza umoja wa kitaifa
 
Back
Top Bottom