Rais Lungu: Ni lazima kila mtu apimwe ukimwi

Rais Lungu: Ni lazima kila mtu apimwe ukimwi

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
_97396915_042e24cf-b928-40ee-903b-3a6b5811ebbb.jpg

Rais wa Zambia Edga Lungu amesema kuwa kwa sasa ni lazima kila mtu apimwe hali yake ya ugonjwa wa ukimwi nchini humo.

Zambia ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya ukimwi kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa na wanaishi na virusi vya ukimwi

Bwana Lungu alisema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo. Alitoa tangazo hilo wakati wa uzinduzi na baraza la ukimwi kwenye mji mkuu Lusaka.

Bwana Lungu alisema kuwa suala hilo limezungumziwa na baraza la mawaziri.

Chanzo: BBC Swahili
 
Magu nae aige mazuri ya rungu.. hawa watu tukitengwa wawe wanajiachia kimakundi mwenye ngoma anagongana na mwenye ngoma na asie na ngoma anatulia au anagongana na asiye na ngoma itakuwa poa sana hadi gonjwa linaangamizwa. Mbona Arabuni waliweza..
 
Nchi za magharibi watu wanaoishi kwanye sehemu zenye takwimu kubwa za HIV pamoja na wageni kutoka nchi kama Africa au Russia wakienda emergency department wakichukuliwa vipimo wanashiriwa kipima HIV pia.
 
Dawa ya ukimwi kuacha zinaa .wenyewe wanasema michepuko sio DILI baki njia kuu
 
And then what? Maana watu wanaambukiza wengine kwa bahati mbaya na wengine kusudi.
Ukishapimwa unajijua upo kundi mojawapo mna deal zenu kwa raha zote bila wasiwasi wala uoga
This is so impractical., ukishalazimisha kupima UKIMWI then what?! unatangaza majibu ya status ya kila mtu au unawawekea label huyu kaathirika na huyu hajaathirika?! nakumbuka South Afrika walijaribu wakashindwa sababu this thing haiwezekani., believe me or not elimu juu ya maambukizi ya vvu imesaidia sana kupunguza rate ya maambukizi kuliko kitu chochote ambacho wanaweza kufanya
 
This is so impractical., ukishalazimisha kupima UKIMWI then what?! unatangaza majibu ya status ya kila mtu au unawawekea label huyu kaathirika na huyu hajaathirika?! nakumbuka South Afrika walijaribu wakashindwa sababu this thing haiwezekani., believe me or not elimu juu ya maambukizi ya vvu imesaidia sana kupunguza rate ya maambukizi kuliko kitu chochote ambacho wanaweza kufanya
Ukikutwa nao unapigwa chata tu kuwa ushaukwaa. Mbona natural kuna magonjwa yalivyo tu ni chata tosha kama mkanda wa jeshi n.k wanaougua hawagusi mtu ovyo
 
Aanze yeye kuwa mfano halafu raia watafuatia.
 
Watupime wote kisha mwenye ngoma awekwe chapa kwenye tako au paja alafu watangaze kuwa kila ukikutana na mtu mnaonyeshana kama wote mna alama ngoma inogile kama mmoja ndo anayo mtaangalia wenyewe rais afanye hivyo kuokoa kanda ya ziwa vinginevyo tutakwisha huku, unaesema watu wabaki njia kuu sawa je mwenza wako akichepuka hivi haya maisha magumu ya kiafrika unayajua vizuri? Huku usukumani mme anamwacha mkewe na watoto anamwambia naenda kutafuta anakaa huko miaka 7 bila kurudi what do u expect?
 
Back
Top Bottom