rais kweli una mapenzi mema na hii nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

rais kweli una mapenzi mema na hii nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 21, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,082
  Likes Received: 5,556
  Trophy Points: 280
  jamani imebidi niulize mh rais ,maana niijitahidi sana kuleta mada za rushwa wizara hii sasa leo nimesoma hapo nikaona niulize kuna nini huko wizararani...???
  Ufisadi waivuruga Maliasili


  na Hellen Ngoromera


  [​IMG]
  SAKATA la uchotaji wa mabilioni ya fedha zilizotolewa na Serikali ya Norway kama sehemu ya ufadhili katika Wizara ya Malisili na Utalii uliofanywa na baadhi ya watendaji wa wizara hiyo, limechukua sura mpya baada ya watendaji wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa hiyo kufikishwa mahakamani.
  Katika sakata hilo, zaidi ya sh bilioni 2.4 zinadaiwa kutumika kifisadi na maofisa hao, hivyo kusababisha Serikali ya Norway kuja juu kutaka wapewe maelezo jinsi fedha hizo zilivyotumika, vinginevyo watafuta ufadhili wao.
  Akizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Ladislaus Komba, alisema watendaji hao wamefunguliwa kesi kwa kile alichodai kuwa wamebainika kwamba walihusika kufanya ufisadi huo.
  Alisema katika vikao walivyoketi ambavyo vilimhusisha Katibu Mkuu Hazina, yeye na watu wa Ubalozi wa Norway nchini, ilibainika kuwa fedha zilizopotea katika mazingira tatanishi ni sh milioni 120 za ununuzi wa pikipiki 70 hewa.
  Kwa mujibu wa Dk. Komba fedha nyingine ambazo ni zaidi ya sh bilioni 1.3 zilitumika kwa ajili ya kodi pamoja na kuwalipa mishahara vibarua.
  Hivi karibuni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwapo kwa ufisadi huo aliouita wa kutisha unaodaiwa kufanywa na maofisa wake kwa kushirikiana na watu wengine wa nje ya wizara yake.
  Kwa mujibu wa Waziri Mwangunga, ufisadi huo unadaiwa kufanywa na maofisa wa wizara yake kati ya mwaka 1994 na 2006.
  Inadaiwa kuwa fedha hizo zilitumika vibaya katika kuendeshea makongamano na semina, mikataba hewa ya manunuzi ya pikipiki zinazofikia 70, ulipaji ushuru wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), misaada inayotolewa na wafadhili pamoja na kuwaajiri watumishi na kuwalipa fedha zinazotolewa na wafadhili kama mshahara.
  Alibainisha kuwa, kutokana na hilo wafadhili walikasirishwa na kitendo cha misaada wanayolipa kulipiwa VAT wakati utaratibu uliowekwa ni kwamba misaada haitakiwi ilipiwe ushuru kwani huo ni uzembe wa maofisa wake kutoandika barua Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ili wasamehewe kodi.
  Kuhusu suala la mikataba ya manunuzi ya pikipiki, waziri huyo alisema wafadhili walitoa sh milioni 70.9 kama msaada wa kununulia pikipiki, lakini hadi leo hakuna iliyonunuliwa, kwani kampuni ambayo maofisa wa wizara yake waliingia nayo mkataba, mmiliki wake alishafariki dunia. Hata hivyo, alisema wanaendelea na taratibu za kuichukulia hatua za kisheria kampuni hiyo waliyoingia nayo mkataba. Kuhusu pesa hizo kutumika katika makongamano, Waziri Mwangunga alisema maofisa hao walikuwa wakitumia fedha hizo kuzidisha bei za vitu, kutoonyesha vielelezo vya namna pesa walizopewa zilivyotumika na mambo mengine, jambo ambalo liliwakera wafadhili hao na kusisitiza warejeshewe fedha za ufadhili huo.
   
Loading...