Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Rais Jakaya Mrisho Kikwete yupo New York kwa ziara ya Kikazi nchini Marekani itakayomchukua siku 12.Mheshimiwa Rais ameongozana na Waziri wa mambo ya Nchi za Nje pamoja na ujumbe wa watu 20.
Siku ya Jumanne (22/09/09) Rais atahudhuria Mkutano unaohusu Mazingira na Hali ya Hewa Duniani.Mkutano ambao utafunguliwa na Rais Obama,Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano Mkubwa wa mazingira utakaohudhuriwa na karibu Viongozi wote Duniani utakaofanyika Copenhagen-Denmark mwezi wa Disemba/2009.
Siku hiyo hiyo ya Jumanne Rais Obama atawaandalia Chakula cha Mchana Viongozi wa Nchi 16.Viongozi wa Nchi 10 kati ya hao ni kutoka Africa kusini mwa Jangwa la Sahara,Rais Obama atazungumza na Viongozi hao ambao wametoa wanajeshi kuunda Jeshi la kulinda amani Nchini Sudan,Rais Kikwete amealikwa katika Mkutano huo.
Siku ya Jumatano (23/09/09) Rais Kikwete atafungua rasmi Mkutano wa Nchi za kiafrika zinazopambana kuutokomeza ugonjwa wa malaria,Nchi hizo 12 zinajulikana kwa jina la ALMA.Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Kundi hilo.Mkutano huo pia utahudhuriwa na Balozi wa UN anayeshughulikia kuutokomeza ugonjwa wa Malaria,Balozi huyo ni Dr.Jay Wisten.
Siku ya Alhamis (24/09/09) Rais Jakaya Kikwete atauhutubia Mkutano wa 64 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa.Siku hiyo hiyo ya Alhamis ujumbe wa Rais utakutana na Carter Center kujadili masuala ya Uchaguzi na Demokrasia.Carter Center ni moja kati ya Jumuiya za kimataifa zitakazoshiriki usimamizi wa Uchaguzi mwakani,pia kujifunza na kuangalia uwezekano wa Watanzania walio nje kupiga kura.
Rais na Ujumbe wake atakutana na Wafanyabiashara mbalimbali kuwahamasisha kuwekeza Tanzania,Atahudhuria Ufunguzi wa Ubalozi wetu huko Washington DC Na kuhudhuria Uzinduzi wa Jumuiya wa Watanzania waishio Marekani.Rais na Ujumbe wake wanatarajiwa kurudi Tanzania Jumapili ya tarehe 04/10/09.