Rais Kikwete,Rais Kagame waialika Yanga

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakata Mrisho Kikwete amewapa mwaliko mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati mara mbili mfululizo, Yanga SC kupeleka Kombe lao Ikulu.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Yussuf Mehboob Manji amesema kwamba wanashukuru kwa mwaliko huo na watakwenda huko, wakirejea kutoka Rwanda ambako wanakwenda kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame wa huko ikiwa ni pamoja na kuitumia ziara hiyo ya mwaliko kuiandaa timu kwa kuweka kambi maalum huko kujiandaa na ligi kuu ya Tanzania.

Manji pia alisema wanatarajia kufungua tawi la klabu yao nchini Rwanda, kufuatia uhusiano mzuri uliopo, baina ya klabu hiyo na nchi hiyo kwa pamoja na rais wake, Paul Kagame.
Manji alisema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ta Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kuhusu mwaliko wa mabingwa hao Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame kutoka kwa rais wa Rwanda, Kagame.

"Tunategemea kufungua tawi jipya la Yanga nchini Rwanda, hiyo itasaidia kuongeza wanachama nje ya nchi kwa kuanzia na Rwanda,"alisema Ofisa huyo Mtendaji Mkuu wa Quality Group Limited.
Yanga itakua Rwanda kwa wiki moja kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wakiwa watacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Rayon Sports, Polisi na APR.




Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji baada ya kuwasili Rwanda na kupokewa na Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Milutin Sredojevic 'Micho' (kushoto)



Manji kulia akijadiliana mambo na Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga



Yanga baada ya kuwasili mjini Kigali, Rwanda.

 
Ni kweli kabisa lakini inaonyesha Manji kadhamiria safari hii,mpaka kaamua kuacha shughuli zake kwa ajili ya mambo ya mpira tu,kwa wanaomjua Yusuf vizuri watanielewa jinsi jamaa alivyokuwa ngumu kumuona b4 hajaingia kwenye mambo ya mpira
 
Dar Es salaam Young Africans at the level of T.P Mazembe in 3 years to come,Bravo Viongozi wote wa team ya Wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom