Rais Kikwete ni extra ordinary

Kuna mahali alisema, "...kama kuna mtu atakaye ona mapungufu kwenye hii katiba basi ana matatizo..."
"...wakati huo nilikuwa kijana na kidume kweli. Nilikuwa sijamzaa mwanagu rz1" Oct, 09, 2014 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 

baba yako ni extra extra extra ordinary
 
Nakuunga mkono kaka;sijawahi kumshangaa kiongozi yeyote kama JK.Huwa najiuliza ana lengo gani na hii nchi!
 
Raisi Kikwete ni raisi dhaifu, hana maamuzi yoyote ya maana zaidi ya kubebewa akili na Lukuvi na Wassira.
 
Yaaani hotuba ya Mh jana, duuuuu! soga tupu za Msoga, aliniacha hoi aliposema " nani kama wajumbe wa bunge la katiba? Akina mama ambao ni migongo ya kupandia kwa wanasiasa," le le le leeee! Nikajua kweli TZ kazi tunayo
 


Kiukweli Kikwete Jana alitakiwa kuwa wazi Juu ya kura ya Maoni....bila kupepesa macho ....Kama Sheria imetamka wazi ni lini angebase kwenye Sheria ..,na mengine angewaachia technical team ya attorney general chamber

Pengine tunaona katiba ni Mbaya lakini utekelezaji UKianza watu watakubali Kwani hakuna jambo zuri LINALOpata uungwaji mkono 100% linapoanza
 
jina lako tuuu(MALISA) linatosha kumjulisha mtu kuhusu andiko lako kabla hata hajalisoma. vipi jamhuri ya kaskazini bado mnaendelea na mikakati ya kuiunda???
risala ya kikwete ni hotuba bora kabisa kwa vigezo vyoote na amewazima vibaya nyie wajinga mnaotaka mwanya ili mumsakame kuwa ametoa ahadi hewa. sisi tunasubiri chochote kitakachoamuliwa na wao tunaenda pamoja
 
Aksante mkuu.Kikwete hana uwezo wa namna hii.
 
wewe u miongoni wa watu wanaotembea barabarani wakiwa marehemu ndo maana hujielewi-unapelekwa tu kama Mkokoteni-pole sana
 
Dunia haijawahi kuwa na raisi kama Jk hana maamuzi magumu kila kitu anaambiwa na Wassira na Lukuvi hiyo aibu ya jana haijawahi kutokea tanzania ccm ni janga la taifa
 
wewe u miongoni wa watu wanaotembea barabarani wakiwa marehemu ndo maana hujielewi-unapelekwa tu kama Mkokoteni-pole sana
na wewe ni sawa na maiti inayosubiriwa kuzikwa muda wowote ndo hujitambui kabisa
 
Mi nasikia harufu ya damu. Huwezi kuendesha ubabe namna hii tena kwa masuala ya watu halafu unaendelea kujifaragua kwa majivuno na ukabaki salama. History will judge you. CCM na viongozi wao wachumia tumbo your days are numbered na kitakachoenda kuwamaliza ni shule za kati ndio watakuwa the vanguard. Kama unabisha soma Mwongozo wa TANU 1971, Mwongozo wa CCM 1981, Programu ya CCM 1987, Hotuba ya Mwalimu Nyerere 1987 alipokuwa anaacha uenyekiti wa CCM, Hotuba ya Mwalimu ya 1992 kwa Mkutano Mkuu wa CCM uliopitisha mfumo wa vyama vingi. Jipimeni mko wapi kama sio mita chache tu kutoka kuzimu.
 
Kuna watu wanaweweseka sana. Ukweli ni kwamba, whether kura ya maoni itabigwa kabla au baada ya uchaguzi, bunge maalum limetimiza wajibu wake na hatua hiyo haitarudiwa

Sawa ila kubali kataa, watanzania ni misukule wasijitambua!
 


Kikwete ni kigeugeu...

mtu atakaemuamini kikwete ktk maneno yake, atakuwa ni mtu wa ajabu sana....
 
KIKWETE baba lao, kishawanyamazisha tayari, mliobaki ni mavuvuzela tu. Wengine tumeshamuelewa tunasubiri kumwaga kura za ndiyo kuikubali Katiba iliyopendekezwa


Mkuu, unatakiwa kujua hili:

"...kiongozi wa umma hatakiwi kuficha msimamo wake kwa wananchi anaowaongoza (kuwawakilisha) au anayeshindwa kutoa uongozi (leadership) kuhusu musuala yote (madogo au makubwa) yenye maslahi na/au kwa mustakabali wa taifa lake..."

Pia, unatakiwa kujua hili:

"...kiongozi wa umma anayeficha msimamo wake kwa wananchi anawaongoza (kuwawakilisha) au anayeshindwa kutoa uongozi (leadership) kuhusu masuala yote (madogo au makubwa) yenye maslahi na/au kwa mustakabali wa taifa lake ni HASARA KWA TAIFA LAKE..."


NOW, tatizo ninaloona katika mijadala yetu mingi (JF, Facebook, Twitter, etc,) ni kuwa wachangiaji wengi (e.g. thatha) huwa wanakuwa na upande (sides) ambapo wanashindwa kuandika ukweli wa mada husika na badala yake hukumbilia kutoa kashfa, kejeli, matusi, etc.

Mwisho,

Hakuna ubishi kuwa Rais wetu (His Exc. Mr. Jakaya Mrisho Kikwete) ameshindwa kuonyesha uongozi katika masuala mengi yanayohusu nchi. Mathalani, katika suala la Katiba amekuwa na rangi nyingi sana......,sometimes he leaves some of us feeling very much embarrassed for his mimic and unsought comments on the way Katiba Mpya should be perfectly handled to finality.

And, kumsifu mtu ambaye anakosa kuonyesha uongozi ni kupoteza muda, though najua kuwa kwa tabia na mazingira ya Tanzania na Watanzania...sio tatizo kumsifu au kumwabudu mwizi, fisadi, aliyeshindwa kuongoza, aliyeshindwa kusimamia rasilimali za wananchi, etc.

Ubarikiwe as you try to make changes into your brain ili wakati mwingine uweze kutoa michango katika mijadala kwa kusema ukweli na sio kuandika upotofu.


 
Ukiwa mdhaifu ni Janga, hawezi kumkera mtu anaonekana kama angekuwa mwanamke angeitwa mama huruma, Anataka amfurahishe kila mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…