Rais Kikwete ni "dhaifu"; Rais Magufuli ni "One man show"

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
Wakati wa utawala wa Rais Kikwete, tulikuwa tunaaminishwa kuwa ni Rais dhaifu asiyechukua maamuzi.

Kila kashfa iliyokuwa ikitokea nchini alibebeshwa Rais Kikwete na kudaiwa hachukui maamuzi kama Rais wa nchi ili kuzuia kashfa mbali mbali. Hata Lowassa mpaka leo anajitetea na kusema, kashfa ya Richmond anaifahamu vizuri Rais Kikwete.

Waeneza propaganda hawakutaka kutuambia kama Rais Kikwete ameziacha taasisi zifanye kazi zake kwa sababu kama wangesema hivyo basi hata hoja yao ya kusema Rais ni dhaifu ingekuwa haina nguvu.

Kimantiki, waeneza propaganda walikuwa wanatuambia Rais Kikwete lazima awe ‘’one man show’’ ili kuhakikisha kashfa hazitokei nchini. Kosa la Rais Kikwete lilikuwa ni kuziacha taasisi za nchi zifanye maamuzi yake bila kuingiliwa na taasisi ya Rais.

Uamuzi wa Rais Kikwete uliwawezesha waeneza propaganda kupata hoja mbali mbali za kisiasa ambazo zilikuwa zinasababishwa na uwepo wa taasisi/idara legelege.

Leo hii waeneza propaganda wamebadilisha tena malengo yao baada ya malalamiko yao kujibiwa kimatendo na wameanza kutuaminisha Rais Magufuli ni ‘’one man show’’ na kwa sababu hiyo wanataka taasisi au idara za serikali zisiingiliwe na taasisi ya Urais katika utendaji kazi wake.

Tulimsikia Tundu Lissu akisema bora wakati wa utawala wa Rais Kikwete kwa sababu hakuziingilia taasisi katika maamuzi yake.

Kwa maana nyingine wapiga propaganda wanatuambia Rais Magufuli lazima awe kama Rais Kikwete ili nchi irudi kwenye kashfa zinazosababishwa na uwepo wa taasisi/idara legelege zilizosababisha kashfa kama za Richmond,Dowans,Kagoda,Meremeta,Escrow, nk.

Ikumbukwe ni hawa hawa kwa miaka zaidi ya nane walituambia kuwa Lowassa ni fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania lakini kilichotokea baadaye kinafahamika.

Ibara ya 33(1-4) ya Katiba ya Tanzania inasema,
33-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Ukichambua kwa undani utagundua Ibara ya 33(1-4) ndiyo imebeba nguvu na madaraka ya Rais wa Tanzania.

Hii ibara haikuwekwa kwa bahati mbaya bali waliyoiweka walifahamu vizuri muundo wa nchi ambao unachagizwa na uwepo wa taasisi/idara ambazo ni legelege.

Kama Rais Magufuli atakubaliana na kelele za wale wanasema hawataki Rais ambaye ni ‘’one man show’’ basi ajiandae pia kutumbukia kwenye kashfa mbali mbali kama ilivyotokea kwa Rais Kikwete.

Rais Magufuli lazima ayakumbuke pia maneno ya Mwl. Nyerere aliposema, ‘’mtu yeyote mwenye akili timamu akikupa mawazo ya kipumbavu na wewe una akili timamu na unajua ni ya kipumbavu na ukayakubali, atakudharau’’.
 
de969430f4391e715bf9927132fe3c74.jpg
 
Tunatumia muda mwingi kujadili WATU na MATUKIO kuliko JINSI gani tunatatua MATATIZO. Matukio yanaturudisha nyuma kimkakati. Tubadilike!
Ninakubaliana na mtazamo wako lakini kumbuka msingi wa siasa zetu uko kwenye vyama vya siasa ambavyo vinajenga mtu/watu badala ya kujenga taasisi ya chama.
 
Hahahhahah kwa kweli wapinzani watafte jipya ila kikwete kawaweza kuwaletea magufuli
Unaweza kuniambia hao wapinzani wamepata athari gani mpaka sasa kutoka kwa Magu ambazo zinatija kwa Taifa?
 
Wapinzani walikua waasisi wa kauli kua " ili tanzania iendelee anahitajika rais mwenye maamuzi magumu" amekuja magufuli na maamuzi yake magumu wanatuambia eti ni dikteta, wameshasahau hata walikua wanatuambia nini! Hawa sio wa kuwapa nafasi! Watatupotosha!
 
kwani uongo??yani kwa kifupi magufuli hajui hata anatupeleka wapi, hajui nini anafanya anaenda enda tu...yani akifa sasa hivi sijui atakumbukwa kwa lipi
 
"MsemajiUkweli, post: 19149542, member: 91662"]

Waeneza propaganda hawakutaka kutuambia kama Rais Kikwete ameziacha taasisi zifanye kazi zake kwa sababu kama wangesema hivyo basi hata hoja yao ya kusema Rais ni dhaifu ingekuwa haina nguvu.
Kauli hii tu inaonyesha unavyozungumzia propaganda badala ya uhalisia

Tanzania hakuna taasisi iliyo huru inayoweza kufanya kazi bila kuingiliwa na Serikali
Takukuru wanaripoti kwa Rais
Polisi wanaripoti kwa Rais
Majuzi tumeambiwa hata mihimili ya sheria na bunge ule wa serikali ''umezama'' zaidi

Hivyo hakukuwa na suala la Kikwete kuchia taasisi zifanye kazi

Richmond ilifichwa na PCCB kwa mara ya kwanza.
Hata ilipoabinika walipika taarifa hakuna aliyechukuliwa hatua.

Majadala ya kesi yalikuwa kwa DPP na DCI wakilumbana.
Hakuna aliyechukua hatua na kesi zikaisha hivyo hivyo

Kila siku tume ziliundwa ukiwa ni ushahidi kuwa hata serikali haikuamini vyombo vyake

Na hata ilipotumia vyombo hivyo, ilikuwa kuzuga tu na kuondoa watu barabarani
Hivi tume ya IGP, PCCB na Mwanasheria mkuu kuhusu EPA ilitoa taarifa gani?

Siku hizi haki ni kwa maelekezo kwa msemo wa maelekezo kutoka juu

Hivyo hoja kwamba kuna taasisi huru Tanzania haipo na hilo linaifanya mada nzima kuwa mfu, potofu na propaganda tu

Kuendelea kujadili ni kukubaliana na upotoshaji huu usio na maana kwa Taifa
 
Back
Top Bottom