Rais Kikwete: Nabii asiyekubalika nyumbani kwake?

Just a question for the JK apologists, Hivi JK alichaguliwa kuwa raisi ili afanye nini? Na so far aliyotakiwa kuyafanya yametekelezeka kwa % ngapi??
 
Rais Kikwete kazi yake kubwa kutembea nchi za nje tu hakuna chochote anachofanya nchi imejaa kila Ufisadi,njaa Umasikini,Ulaji rushwa umeongezeka na Ufisadi ndio huo unazidi Nchi imeuzwa ikiwa watamchaguwa tena wananchi basi wananchi wamejaa na usingizi tunachotaka ndugu zangu Wana JF Maendeleo na kipatikane chama kingine tuone mafanikio ya chama kingine kiondowe Ufisadi,Rushwa,Ujambazi,Wizi wa Mali ya Umma Tuamke ndugu zangu WaTanzania Tumelala usingizi mzito ndugu zangu Wana JF Mungu atusaidie Ameen.
 
Nilienda mahali kidogo nimerudi namuandalia majibu mlalahoi

Je huko ulikokuwa umepata confirmation kuwa waendeshaji wa jamii (jambo) forums walikamatwa na kuwekwa selo wakati wa Kikwete na sio wa Mkapa kama ulivyodai mapema?
 

Kaka sikatai hapa nilikuwa najaribu kuyatafuta mazuri ya JK na sio kuwa nakubaliana na siasa na msimamo wake kwani hauridhishi but hebu tujaribu kuangalia kwanini nasema ni afadhali JK. Kwanza tukija CCM wenyewe ni chama kama cha kimafia ambacho kimekaa kuangalia nani anajaribu kukikosoa ili kimshughulikie unadhani mtazamo huo utaweza kuibadilisha uendeshaji wa chama? Au unataka kuniambia Sitta na wenzie ndio watakaobadilisha chama unakuta jibu hakuna.

Kuhusu CCM ni 10% of the population wewe ni mtu usiyeifahamu siasa ya tanzania. CCM naweza kukwambia ni 60% of the population. Vijijini huko hakuna mtu anayejua chama cha siasa zaidi ya CCM. Chadema wanajua hiki na kazi nzito kuwaelemisha watanzania kuwa CCM imekumbatia mafisadi na ndio maana nguvu ya CCM iko vijijini na sio mijini. Hivyo basi ni mimi na wewe tunaokaa katika keyboard tukaripuka hapa ndio 10% the rest wanafahamu chama ni CCM na huna vya kuwaambia hiyo ndio inayowafanya CCM wawe na nguvu. Sasa tukitazama CCM imejaa mauvundo ambao mwisho wa siku unajiuliza nani ana uafadhali yule ambaye anajali maslahi binafsi kama Lowassa au JK mpenda masifa. Ndio unakuta bora JK kwani japokuwa anapenda sifa bado ana ile damu ya uzalendo.

Tuje katika meremeta, IPTL na mengineyo. Mwafrika alinionyesha article inayosema kuwa Kikwete alisign IPTL. Come on hivi waziri anakuwa responsible kwa kusign kitu wakati chini yake kuna wanasheria, makatibu wakuu na maafisa walikuwa wapi??? Mnataka kuniambia nyie mkiwa mawaziri ukiletewa mkataba utajua kama huo mkataba ni dili?? Kwanza wewe utaangalia sheria inasemaje, pili vigezo vyote vilifatwa?, Tatu nani alifuzu unakuta vigezo vyote vimefaulu mnataka kuniambia waziri atoke aende marekani kucheki kama IPTL inaexist au la that is pathetic na ludicrous to be honest huwezi kuongoza idara kihivyo let alone wizara.

Tuje katika infrastructure. nimeshakueleza kuwa utekelezaji wa project mbalimbali unategemeana na malengo ya serikali. Unataka kuniambia waanze na barabara nzuri bunda, msata, kila eneo linazalisha aina moja ya zao halafu wakulima wawe na gharama kubwa za kusafirisha mazao ya mijini unadhani ndio akili hiyo au wewe umesoma economics ya kijijini. Wapi bora kutengeneza barabara mijini kwenye masoko ya bidhaa au kule katika kuzalishia? Kimtazamo wangu ni afadhali utengeneze kule katika mijini maana ndio kwenye viwanda na wateja then uanze kutengeneza maeneo ya wakulima kufuatana na umuhimu wa barabara. Otherwise ukifanya zote kwa pamoja barabara zinakuwa haziishi kwasababu serikali inakuwa haina hela. Likewise, ukiwa unatengeneza barabara vijijini utamaliza lini kuna maeneo haya natija ya kuwa na barabara nzuri hata ulaya kuna maeneo ukienda barabara kama bunda vijijini je unadhani wao hawakuona umuhimu wa wakulima wao kule vijijini msitake kutuzingua bwana JK amejitahidi kwa hili.

Tuje katika madudu aliyoyakuta sawa alikuwa na yeye ni mmoja katika mawaziri hivyo basi anabear part of the responsibility unasema kwanini hakusema rais aliyepita alifanya madudu.Kwanza kaa ukijua ukimcritise rais aliyepita na kumsulubu ukae ukijua na wewe jiandae kuyapata hayo hayo kama sio msafi (muulize Chiluba wa Zambia yalimkuta nini). Kwani rais si mtu ni institution iliyojengwa na watu hivyo basi akiondoka watu wake hubakia let alone mko chama kimoja unataka apate tabu kuongoza nchi. Be realistic my friend unataka kuniambia JK asimame katika mimbari kama hayawani aseme Mkapa ndio matatizo yote. I think not anajua repurcussion zake labda wewe ukishakuwa rais sema hivyo but mtu mwenye akili zake timamu hawezi hata kuthubutu kusema hilo jambo. Kawatawale jamaa zako but sio watanzania JK ana mazuri yake
 

Ndio uongozi ulivyo kuendelea kusimamia na kufanikisha mipango uliyokuwepo kama MMEM na MMES hata obama anaendeleza vita afghanistan na iraq aliyoikuta so huwezi kutenganisha kwamba anasimamia miradi ya mmem na mmes..

Project mpya za maji, barabara mikoani naweza kutaja kwa uchache Mbeya -Rukwa, Handeni- Msata, Arusha-Babati-Singida etc hata kama zilikuwepo ndyo ilivyo mkapa alikuta mradi wa barabara ya kwenda kusini kwa mwinyi akasimamia vizuri

Innovation na creativity ziko nyingi ndugu including kilimo kwanza, utalii (vyuo vya utalii) na mkakati ambao umeongeza watalii na Tanzania kufahamika duniani zaidi wakati wake...

Huwezi kusema hajafanya chochote huo si uchambuzi wa mambo bali upofu.
 

Bado hujajibu swali la kuwa -- tofauti ya ufisadi wa Kikwete na ule wa Sitta au Lowassa ni upi. BTW bado nasubiria majibu yako kwa alichoandika Kibanga


Chadema imeshinda Tarime, Kigoma na kwingineko, je huko nako ni mijini? Je wanakoshinda CUF ni mijini tu? Get data zako mkuu maana naona leo unachemka kweli!

Sasa tukitazama CCM imejaa mauvundo ambao mwisho wa siku unajiuliza nani ana uafadhali yule ambaye anajali maslahi binafsi kama Lowassa au JK mpenda masifa. Ndio unakuta bora JK kwani japokuwa anapenda sifa bado ana ile damu ya uzalendo.

Tofauti ya ufisadi wa Kikwete na Lowassa ni upi? rudia tena alichoandika Kibanga


Mimi nikiwa waziri na watu wakaniletea mkataba kama wa IPTL, moto nitakaowasha hapo hakuna atakayeuzima kirahisi. Lakini nikiwa fisadi kama Kikwete, nitajifanya tu kuwa sijui kinachoendelea


Longo longo kibao lakini bado hujasema alichofanya Kikwete kwa mifano hai


Kikwete hawezi kumsulubu Mkapa kwa vile wote wawili (Kikwete na Mkapa) ni mafisadi waliokubuhu.

Swali kwako - mkataba wa buzwagi umesainiwa wakati wa uongozi wa nani?
 

Ha ha ha ha ... wanathubutu hata kutaja kilimo kwanza (mabilioni ya fedha yametumbuliwa) - mradi wa kifisadi wa wana ccm
 

Good point but before i answer your question nikuulize maswali yafuatayo.
a. CCM ina majimbo mangapi vijijini ?

b. Wapinzani nao je?

c. Mkataba wa buzwagi nani alikuwa rais? Na hivi unajua kwamba Mkapa alikuwa ni Bully leader?

Acheni kujenga hoja za kwamba JK before nijibu maswali haya
 

Tufanye hivi,endelea kumsapoti JK na ndoto zake za kutuletea maisha bora kwa kila Mtanzania,na mie nibaki na mtazamo wangu kuwa JK ni msanii,mbabaishaji na aliyeshindwa kazi.Of course,atarudi madarakani 2010-15 (na kwa sapoti ya watu kama wewe huenda mkapiga kelele katiba ibadilishwe awe rais wa milele).

Hakuna kazi ngumu kama kumshawishi mvuta sigara aache kwa vile sigara yaweza kuleta kansa.Ila akipata TB ataacha mwenyewe wala hakutakuwa na haja ya kushawishiwa.Likewise,kitakachobadili mtizamo wako sio hoja za hapa JF bali hatma ya nchi yetu.
 
Good point but before i answer your question nikuulize maswali yafuatayo.
a. CCM ina majimbo mangapi vijijini ?

b. Wapinzani nao je?

Kulinganisha na nini? Ukilinganisha mijini vs vijijini, wapinzani wana majimbo mengi vijijini kuliko mijini.

c. Mkataba wa buzwagi nani alikuwa rais?

Na hivi unajua kwamba Mkapa alikuwa ni Bully leader?

Acheni kujenga hoja za kwamba JK before nijibu maswali haya

Aliyekuwa raisi wakati mkataba wa buzwagi ukisainiwa (hotelini) ni Kikwete. Kikwete alimtuma rafiki yake kipenzi Karamagi kwenda kuuza nchi kwa wazungu kule ulaya kwani waliona aibu kufanya hivyo ndani ya Tanzania.
 
Ha ha ha ha ... wanathubutu hata kutaja kilimo kwanza (mabilioni ya fedha yametumbuliwa) - mradi wa kifisadi wa wana ccm

Fedha zimefika kila wilaya na matrekata yamenunuliwa kama hutaki kushiriki kujenga nchi endelea kulalamika

Another innovations: JK loans, wajasiriamali wadogo wadogo wamepewa mkopo wengi wa access funds kuendesha project zao..
 
Ha ha ha... independent voter anayemtetea Kikwete kwa nguvu zote. Unaweza kufanya spin zako kwenye vijiwe vya kahawa lakini sio hapa

Kwisha habari ukirudi utaanza kutukana maana ukikosa hoja ndio kimbilio lako..
 
Fedha zimefika kila wilaya na matrekata yamenunuliwa kama hutaki kushiriki kujenga nchi endelea kulalamika

Another innovations: JK loans, wajasiriamali wadogo wadogo wamepewa mkopo wengi wa access funds kuendesha project zao..

Komiko Ali wa baghdadi bwana, hawezi hata kuweka data kusapoti anachoandika!
 
Kwisha habari ukirudi utaanza kutukana maana ukikosa hoja ndio kimbilio lako..

Angalia kiroja ulichoandika hapa ... hizi ndizo mnaita hoja huko madrassa!? kutetea mafisadi kama Kikwete kwataka moyo yahe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…