Rais Kikwete mbona unanishangaza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete mbona unanishangaza?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Nov 25, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimefuatilia utendaji wa awamu ya nne kwa ukaribu sana tena kwa muda wote.Kwa kweli vitendo hakuna kabisa.Inakuwa kana kwamba viongozi wetu wamepikwa na chuo fulani special cha kudanganya.Lakini hata hivyo, kwani siasa ni nini hasa,si ndio mambo yenyewe hayo? Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio mabaya tena yakusikitisha.Wananchi waliokaa kwenye vijiji vyao kwa muda mrefu wanshangaa ardhi yao ikiwa imeuzwa na watendaji serikalini na huku wao wenyewe wakiambiwa waondoke huku wakiwa hawana mahali pakwenda. Ni vitendo vya kinyama tena vinavyoshangaza.Katika matukio yote sikuona kiongozi mkuu yeyote wa serikali akikemea vitendo hivyo kwa uzito nilioutegemea na viongozi kuchukuliwa hatua.Hakika kumsikia Rais Kikwete akiongelea swala hilo katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro imenishangaza kidogo.Kwa nini sasa, wakati wananchi wameendelea kuteseka kwa muda mrefu kiasi hicho bila hata kupata msaada wowote? Nadhani ni katika harakati zile zile za kisiasa.Lakini katika mtindo huo, tunalipeleka wapi taifa hili? Naomba nimuambie Rais Kikwete wazi kwamba ,wananchi wanachohitaji sio maneno,wanahitaji vitendo zaidi.Katika hili tunategemea wale wote walioshiriki katika kupora ardhi ya wananchi na kuwanyanyasa kwa njia moja au nyingine wafikishwe kwenye vyombo vya sheria au wachukuliwe hatua za kinidhamu.
   
Loading...