Aibu gani hii watanzania tunayotwikwa ameshindwa kushughulikia sakata la mtwara huyoooooo kiguu na njia.
Labda anataka kuzuga kuwa anapunguza gharama.Nilitaka kushangaa asiende Davos,maswali ya msingi.
1.Kwanini anatumia Swiss air?ndege ya serikali imekuwaje?
2. Wametuambia watuL atakaokutana nao lakini madhumuni ya yeye kukutana nao ni nini?
3. Kurugenzi ya mawasiliano mnaposema raisi ataendelea na ratiba ngumu katika siku ya pili mnamanisha nini?au ni ujumbe gani mnatupatia?kama ni ngumu nani kampangia?na baada ya nyie kiliona Hilo umechukua hatua gani?
4. Vipi Mmemwandaa kujibu maswali ya wanahabari huko ulaya kihusu Ile ripoti ya watu wa haki za binadamu?asije tokwa na povu kama Canada.
Mwenye majibu plz
Umenona NIMELALAMIKA??? kwanini WAJIHAMI?
Mkuu hawezi kuwatajama kwa sababu za kiusalama
Mkuu mimi nadhani ni siri ya Taifa! lakini sina ushahidiOrodha yao nayo ni siri ya taifa!
Ni kweli hasa ikizingatiwa kuwa wanaoongozana nae wengi wanatia aibu licha ya hasara. Unategemea nini kwa mtawala wa kiswahili asiyezingatia ethics? Usishangae kuna akina mashangshaazi watoto wa mjomba na mashoga wa mkewe wanaokwenda kushangaa shangaa na kufanya shopping uchwara. Namna hii kwanini deni la taifa lisiumke?
Hilo tangazo la Ikulu lina kasoro nyingi sana. Binafsi natilia shaka kama kweli Kikwete amealikwa na Rais wa Ufaransa. Shaka yenyewe iko kuanzia kwenye mapokezi na nafasi za watu atakaokutana nao pamoja na taasisi atakazotembelea. Nahisi hapo amejipenyeza tu (amezuga) kwa muda lakini safari halisi ni kwenda Davos Uswisi kwenye huo mkutano wa World Economic Forum.
Lakini kwenye hilo tangazo hata pasipo kuumiza kichwa, kwa ujumla limekosa umakini katika uandishi. Kwanza kitu kama MTENDAJI MKUU WA MFUKO PRIVATE FUND na SHIRIKA LA UCHUMI DUNIANI (WEF)ni taasisi ambazo hazipo na ukiambiwa maandishi kama hayo yameandikwa na mtu anayefanyakazi IKULU hiyo ni aibu kwa Taifa. Tangu lini World Economic Forum (WEF) ikawa Shirika la Uchumi Duniani. WEF ni kongamano linalokutanisha watu mbalimbali kujadili masuala ya kiuchumi duniani. Ama ukiwauliza hao watu wa Ikulu Mfuko Private Fund uko wapi na unaendeshwaje sijui watajibu nini. Hata hilo jina la huyo mtendaji inaonekana limekosewa.
Ni muhimu kuwa makini katika mambo ya msingi japo kwa wengine wanaona ni mambo madogo, kwa wenzetu unapokosea japo herufi moja kwenye jina la mtu inaweza ikaleta madhara makubwa sana
Kati ya Kikwete, Obama na Cameron nani ana risk kubwa ya kushambuliwa. Mbona Cameron akienda nje (kutoa Afgan na Iraq) nchi inajulishwa anaenda wapi na wajumbe gani? Vile vile Obama anapotembelea nchi nyingine kwa ziara ya kiserikali nchi inajulishwa anaambatana na nani. Ni usalama gani anaogopa Kikwete?
Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko Private Fund.