Rais Kikwete kweli ni Jembe

Watanzania tuna safari ndefu sana ya maendeleo katika taifa hili. Hebu fikiria nchi yetu ni maskini na inataka ipige hatua za maendeleo ili mungu akijalia nayo ipande kwenye nchi za dunia ya kwanza, Lakini unashangaa mtu mwenye nia hasa ya nchi hii kusonga mbele anasema JK ETI NI JEMBE. JAMANI HEBU FIKIRIA KAMA JK NI JEMBE KWA LEVEL YA WATANZANIA hivi kuna future kweli katika nchi/Taifa hili.Muda mwingine huwa naamini hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya kujikombakomba. Pole sana ndio nyinyi ambao mpo tayari hata kuiba kura, na dunia hii wajinga hawaishi.
 
Jamaa ni jembe wa kukwea pipa kila Asubuhi kwenda nchi za nje. Jamaa ni jembe kweli. Hakuna rais aliyepanda ndege mara nyingi kama yeye.
 
Sikumbuki Rais wa Tanzania alietawala katika mazingira magumu kama JK huyu jamaa kwa kweli ni kiongozi kama ingekuwa ni kiongozi uchwara mchumia tumbo kama Mkapa hali ingekuwa mbaya zaidi sasa hivi tuna japo matumaini kupitia katiba mpya tunaweza ikomboa nchi yetu toka kwa mabeberu watake wasitake.

 
AHADI ZA KIKWETE WAKATI WA KAMPENI 2010-2015
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36. Kulinda haki za walemavu - Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Haya ahadi ni hizi na tuangalie ujembe wa JK katimiza ngapi mpaka sasa.
 

JEMBE-Lina TUNDU katikati,ambapo MPINI huchomekwa.........
 
Mtoa mada acha matusi. Kama raisi jembe inamaana kuna mipini yake?
 
JK kama kiongozi ana mafanikio na madhaifu yake pia. Kwa kuangalia pande mbili, mafanikio ni kidogo sana.
Tukimpima kwenye nyanja za Kisiasa, Kidemokrasia, Utawala bora na Kiuchumi, sioni alipofanikiwa labda kisiasa.
Kiemokrasia; aliuvuruga uchaguzi wa 2010 na kuwa uchaguzi ulioshindwa vigezo vya huru na haki. Alichofanya baada ya hapo ni kujisafisha kupitia mchakato wa Katiba mpya.
Kiuchumi; Je deni la Taifa limepungua au limepungua? Mfumuko wa bei? Std ya maisha ya Mtz?
Utawala bora; sheria ni msumeno?
 
Jembe katika nyanja ya utalii wa nje, nafikiri katika awamu zote JK ndiye rais ambaye amevunja rekodi ya kufanya safari za nje kuliko wenzake waliomtangulia.
 
when serious matters are being analyzed in an "IMBECHILI" way
 
Tuna safari ndefu. Nchi hii ni maskini na umaskini umesababishwa na viongozi ambao wewe unawaita majembe
 
Mseme yote JK Anabaki kuwa Jembe na mtoa mada hajakosea. Mie mwenyewe namkubali JK Kwa jinsi anavyokabiliana na changamoto Mbalimbali.KWELI JK NI JEMBE
 
Jembe katika nyanja ya utalii wa nje, nafikiri katika awamu zote JK ndiye rais ambaye amevunja rekodi ya kufanya safari za nje kuliko wenzake waliomtangulia.

Tukiangalia kwenye kila nyanja, JK atafeli kila eneo isipokuwa ujenzi wa miundominu ya barabara tu, kama data za Dk Magufuli ni za kweli.
Vinginevyo mleta mada ajipange upya.
 
Mseme yote JK Anabaki kuwa Jembe na mtoa mada hajakosea. Mie mwenyewe namkubali JK Kwa jinsi anavyokabiliana na changamoto Mbalimbali.KWELI JK NI JEMBE

Mtoa hoja amezungumza kijumla jumla, ameshindwa kuainisha ni eneo gani hasa JK ni jembe. Mleta hoja angerejea nyanja nlizoainisha- uchumi, siasa, miundombinu, utawala bora, demokrasia nk, angeweza kuona mapungufu ya JK kirahisi sana.
Wewe unayemuunga mkono tueleze sasa JK ni jembe kwenye maeneo gani kati ya hayo .
 
Teh teh teh teh! mimi namfurahia Jembe na serikali ya ccm maendeleo wanayoyataja ukilinganisha na miaka 50 ya CCM kuongoza nchi ni hakuna kabisa!
 


Ebooooo huu si upoyoyo, hivi kama umeweza kuorodhesha utumbo wote huo halafu itakuwaje usiweze kuorodhesha utumbo mwingine wa majibu ya utumbo wako wa awali!?!?.
 
Kibaraka usie na haya wewe! Mungu yupi unae mzungumzia?tutolee kamasi hapa nguruwe mkubwa wee.

jitazame kabla hujatazamwa kwa hiki ulichokiandika je wewe ni mwanasiasa kweli?
 

uhuru wa habari upo wapi?"kumtukana jk ni sawa ila kumsifia inapobidi na kustahili humu jf hapana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…