Hakuna Rais aliyetawala kipindi kigumu kama JK. Alianza na Tatizo la UMEME, NO Uzalishaji, Likaja la tofauti za fikra baina yake, na Upande wa Mkapa, Mangula, Salim A, Salim, Butiku, Kaduma na wenzao, Likaja la Mafisadi, Sikuamini Jeetu Patel Alivyowekwa Rumande, Lipo bado la Mramba na Mgonja, Likamalizia la Lowasa Kujiuzulu. Uchumi duni bila uzalishaji, Wizi na Hujuma Reli, Bandari, Uzalishaji umeme, na Maofisini, Uhuru vyombo vya habari na uhuru wa watu kusema, Kukabiliana na changamoto za wasomi wa shule za kata kutoka kila kata na kila aliyemaliza form four anajua kukosoa na kupenda upinzani bila kujua ni yeye karuhusu.
Elimu ya juu, mfano hai. 2002 Nyegezi SAUT Peke yake ilikuwa na wanafunzi 300 leo wanakimbizana na Ellfu 15, nyegezi tu, acha matawi yake ya Mwenge Moshi, Dar, Ruco Iringa, Tabora, Mtwara, Songea nk. Udom pia, Nelson Mandela, Tumaini, St. John. Wote wanaomaliza ni wanasiasa na wanajua sana kuongelea uchumi na kukosoa. Magazeti, Redio, Zanziber, Uamsho, Serikali tatu, Katiba, Udini, Ukabila, Rushwa za ndani na nje ya chama. Doh!!!! Jamani, Mwacheni JK Afanye kazi. Tutamkumbuka, tunamchukia leo. Rais wa kumpenda ni wa kunywa nae chai. Mwl. JKN. Huenda kuchukiwa sn ni dalili njema ili tumkumbuke baadae.