Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,228
- 618
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa atastaafu rasmi kama Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano Alhamisi ya Novemba 5, mwaka huu, wakati Rais mpya na wa tano atakapoapishwa.
Aidha, Rais Kikwete ambaye jana alipanga foleni kwa kiasi cha takriban dakika 5 pamoja na wapiga kura wengine wa kijiji cha kwao cha Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani kwa ajili ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika jana.
Rais Kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete, aliwasili katika Kituo cha Kupigia Kura cha Hospitali ya Msoga saa 6:21 mchana na kwenda moja kwa moja kwenye foleni ya wapigakura akiwa na watu kiasi cha 12 mbele yake.
Rais Kikwete aliwaambia waandishi wa habari kuwa tarehe yake rasmi ya kustaafu ni Alhamisi ya Novemba 5, mwaka huu, siku 11 kutoka leo, wakati Rais mpya wa Tanzania, Rais wa Tano atakapoapishwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
"Kwa bahati mbaya bado iko mbali na nalazimika kusubiri mpaka Novemba 5, wakati nitakapokabidhi madaraka kwa Rais wetu ajaye" alisema Rais Kikwete.