Rais Kikwete anahusika moja kwa moja na mgawo wa umeme nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete anahusika moja kwa moja na mgawo wa umeme nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  Rais Kikwete anahusika moja kwa moja na mgawo wa umeme nchini
  [​IMG]


  Isango

  [​IMG]
  KWA wanafalsafa nilishasema hakuna neno la bahati mbaya.
  Kila neno hutolewa kwa kukusudia jambo fulani, huwezi kutamka kitu fulani ukasema kuwa ni bahati mbaya, mfano umetukana mtu, ukiulizwa unasema ni bahati mbaya, mbona hakuna bahati mbaya katika kutukana mawe? Au miti? Kwa nini ukaja kwa huyu na ukasema hivi wakati huu.
  Katika moja ya mambo yanayoonekana kukosa majibu mwaka huu, ni sakata zima la kampuni ya Kimarekani ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond. Kampuni hii inaonekana wazi sasa kuwaumiza vichwa watawala wetu kwa kukosa majibu ya msingi. Watanzania wengi wameumiza vichwa kufikiri sana na kila kukicha wanalalamika, suala la Richmond limekuwa ni moja ya mambo mazito nchini kujadiliwa.
  Limejadiliwa likaonekana kuwa halina rushwa, hii ni kutokana na ripoti ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Edward Hosea, baadaye iliundwa kamati ya Bunge kuchunguza sakata hili na kuonekana kuwa kuna ufisadi mkubwa usiomithilika, tena uliofanywa na viongozi wa juu.
  Baada ya Kamati Teule ya Bunge kufanya kazi yake, kulitolewa mapendekezo mbalimbali ambayo serikali ilipaswa kuyafanyia kazi, mojawapo ya mapendekezo hayo ilikuwa ni kuwawajibisha wote waliohusika na kashfa hii nzito iliyofilisi taifa letu kiasi cha sh 152,000 milioni kila siku kwa miaka takriban mitatu.
  Taarifa nyepesi isiyokidhi hata kuwajibu watoto wadogo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, kuwahadaa Watanzania. Katibu Mkuu akasema kuwa wahusika wamepewa onyo, na kuwahakikishia Watanzania kuwa hakukuwa na dalili zozote za rushwa katika sakata hili na Rais Jakaya Kikwete hahusiki na Richmond .
  Luhanjo anasema: “Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na maneno na vijembe ati kuwa kuna mkono wa Rais Kikwete katika kutoa tenda ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopata Kampuni ya Richmond.
  Kiini cha maneno hayo ni kauli za baadhi ya wanasiasa zilizopazwa sauti na baadhi ya vyombo vya habari.
  Tunapenda kusema, tena kwa msisitizo, kuwa maneno hayo si ya kweli na hayana msingi wowote. Rais hajahusika na uamuzi wa tenda hiyo kupewa kampuni ya Richmond. ”
  Kauli hiyo ilipokelewa na Watanzania kwa hisia tofauti, lakini kama ambavyo nimekwisha sema kauli za viongozi wetu kwa sasa kila inapotolewa tuipokee kwa umakini mkubwa, kama ambavyo kauli nyingi zinazopingana ambazo amekuwa akitoa Rais mwenyewe wala si kupitia kwa wasemaji wake.
  Ni kutokana na kashfa ya Richmond, IPTL, taifa letu limekuwa likipata mgawo mbaya wa umeme, kwa sababu tu Shirika la Umeme limekuwa likiyalipa mashirika hayo pesa nyingi kiasi cha kushindwa hata siku moja kujitegemea ama kujiendesha lenyewe.
  Kwanza ilitolewa tahadhari kuwa mitambo ile kama isingenunuliwa taifa lingeingia gizani, hivyo ili kukwepa giza afadhali mitambo ya Dowans inunuliwe. Hiyo ilikuwa hoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania Dk. Idris Rashid.
  Hatujui mtendaji huyu wa serikali aliwasiliana vipi na mkuu wake wa nchi au alimshauri vipi, mpaka akawa na ujasiri wa kupendekeza mitambo hiyo haramu inunuliwe, hata kama katika kuinunua tulikuwa tunapingana na sheria ya nchi kuhusu manunuzi ya umma.
  Nchi yetu kweli imeiingia gizani, chanzo cha tatizo kinafahamika, mkuu wa nchi akatoa “amri” kuwa sasa mitambo ya IPTL iwashwe. Sentensi kama hiyo ilionekana kuwa ni nafuu ya Watanzania, kuwa wataepushwa na giza hili. Wizara husika zikaamriwa, huenda kwa amri ile ile kama iliyotumika wakati wa kuingiza Richmond, na mawaziri husika wakaingia mkenge kudanganya Watanzania.

  Oktoba 21, 2009 Rais Jakaya Kikwete alitoa agizo kuwa mitambo ya IPTL iwashwe.
  Oktoba 25, 2009 tayari meli yenye shehena ya mafuta iliwasili Dar es Salaam kwa ajili ya kuleta mafuta ya kutumika kwenye mitambo ya IPTL.
  Tufikiri kwa makini na kwa kina bila woga, tena kwa ujasiri wa uzalendo, tutajiuliza, hivi ni kweli hakuna mkono wa Rais katika giza linaloendelea nchini? Au katika hili suala la kukatika umeme Tanzania?
  Tafakari kuwa Rais Kikwete alitoa tangazo mitambo ya IPTL iwashwe, Oktoba 21, 2009, kisha tukaambiwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa serikali imeagiza mafuta ya kutumia kwenye mitambo ya IPTL Uarabuni, Baada ya siku chini ya sita, tukataarifiwa kuwa mafuta yameletwa na merikebu ya mizigo na yamefika Bandari ya Dar es Salaam yakisubiri kupakuliwa ili mitambo hiyo iwashwe.
  Tena meli nyingine inabidi zisogezwe haraka ili kupisha upakuaji wa shehena ya mafuta ya IPTL.
  Tujiulize tena, meli kutoka Uarabuni huchukua siku ngapi? Au mafuta yaliagizwa kabla ya Ikulu kuzungumza? Na ilikuwaje mafuta yakaagizwa kabla ya Ikulu kutoa tamko? Ikulu ilipataje kujua kuwa giza litaingia, na nchi itatumia mitambo ya IPTL? Ni wachache sana watakaokubali kuwa giza hili limepangwa tena kwa ajili ya kutafuta umaarufu wa kisiasa ambao hauna uzalendo hata kidogo, bali ni udhaifu mbaya sana wa uongozi, unaoashiria rushwa mpaka uongozi wa juu wa nchi.
  Meli hii ilikimbia kiasi cha kuvunja rekodi ya safari za meli kutoka Uarabuni kuja Tanzania, chini ya muda wa siku sita tu. Imewezekanaje?

  Kama kweli mafuta yalishaagizwa kutoka Uarabuni kabla tujulishwe kwa nini yaliagizwa?
  Nani aliagiza? Alikuwa anatekeleza agizo lipi? Alijuaje amri ya rais kabla haijatamkwa? Alijuaje kuwa IPTL wangekubali kuwasha mitambo? Alijuaje kuwa IPTL hawana mafuta ya kuwasha mitambo?
  Hata hivyo nijuavyo, nchi yetu haiendeshwi katika udikteta, ni nchi ya kidemokrasia, pesa zetu zina bajeti na bajeti hupitishwa na Bunge, je, pesa hii ya kununua mafuta ya IPTL ilipatikana kupitia mfuko upi?
  Na kwanini haikusubiriwa lijadiliwe bungeni kama suala la dharura wakati Bunge lilikuwa linaanza wiki inayofuata? Rais atatolea maamuzi pesa za Watanzania bila ridhaa yao mpaka lini?
  Nakumbuka aliwahi kutumia amri kama hii kusema pesa zilizorudishwa na wezi wa EPA zipelekwe katika benki ya pembejeo za kilimo.
  Kufuatia ushahidi huu, nimeweza kuona majibu yafuatayo yanaweza kuhusishwa kabisa kwa rais wetu na kashfa ya giza la nchi yetu.
  Lakini yakiendelea madudu hayo yote, tujue kuwa hakuwa sahihi aliyewahi kusema kuwa nchi yetu kwa sasa mgawo wa umeme utakuwa historia, baada ya kutoka Marekani na kuongea na wawekezaji wa Richmond . Mambo haya kwa jinsi yalivyo tunaomba basi ajitokeze tena Katibu Mkuu Kiongozi, aseme na katika giza hili Rais Kikwete hahusiki ili watuthibitishie kwa hoja juu ya madai tunayoyaona ambayo si ya kawaida katika sakata hili.

  Tunaogopa nini kumuwajibishwa Rais Kikwete na serikali yake kwa kushindwa kuwaletea wananchi umeme wa uhakika, badala yake wamekuwa wakitufanyia biashara sisi maskini?
  Rais anatumia pesa zetu haijulikani ni kwa nia ipi kufanya biashara na IPTL kwa kasi ya ajabu huku nchini kote ikitolewa tahadhari ya El-nino, na umeme wa Tanzania tunategemea wa nguvu za maji? Kuna nini katika giza lililopo? Hivi si Rais Kikwete ndiye aliyewaahidi Watanzania kuwa sasa mgawo wa umeme utakuwa historia nchini, baada ya kuwapo kwa kampuni za kuzalisha umeme wa dharura wa kupitia Kampuni hii ya Richmond?
  Tamko nyonge la Ikulu lililotolewa na Luhanjo liliwahi kusema kuwa: “Rais alikataa Kampuni ya Richmond isipewe malipo ya awali (down payment) ya dola za Marekani milioni 10 na kutaka ukweli kuhusu uaminifu na ukamilifu (integrity) wa kampuni hiyo ujulikane.
  Rais alikataa maombi yaliyopelekwa kwake na Wizara ya Nishati na Madini ya kumuomba aagize Wizara ya Fedha, iilipe kampuni hiyo fedha hizo.
  Rais aliagiza Wizara ya Fedha ibaki na msimamo wake na kuitaka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wafanye mambo mawili.
  Kwanza, wafanye utafiti zaidi kujua undani wa Kampuni ya Richmond. Isije kuwa ni kampuni bandia wakapewa fedha wakatokomea nazo na mitambo isipatikane na hukuna namna ya kuipata kampuni wala wahusika wake.
  “Pili, aliagiza wawatake viongozi wa Kampuni ya Richmond kwanza walete mitambo, ikishafika, ndipo walipwe.
  Maagizo hayo ya Rais yalizingatiwa na Kampuni ya Richmond ikapewa sharti hilo lakini, ikashindwa kulitekeleza na kuishia kuingia mkataba na Kampuni ya Dowans iliyokuja kuleta hiyo mitambo badala yake.”
  Hivi baada ya hapo, Rais alimchukulia nani hatua kwa kuona kuwa aliyoagiza hayakutekelezwa?
  Baada ya kujua kuwa Richmond haikuweza kazi na kabla haijaingia mkataba na Dowans, yeye kama mwenyekiti wa baraza la mawaziri alipokeaje hilo, huku akijua kuwa Richmond imelipwa pesa huku ikiwa haijafanya kazi? Kwanini alikaa kimya muda wote mpaka sasa?
  Kama hahusiki awawajibishe waliohusika japo naye hawezi kukwepa kashfa ya zamu hii, kuwa anahusika moja kwa moja na dili ya uagizaji wa mafuta ya IPTL, yeye na watu wake wa karibu. Na hili haliniondolei ujasiri wa kusema kuwa Kikwete ni fisadi, anawaangamiza Watanzania kwa kutumia giza ili akwapue pesa zao akishirikiana na makampuni ya umeme. Mungu azidi kutubariki, atufunulie akili zetu tuweze kujua tunayofanyiwa.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  It's very sad kuona nchi kama Tanzania iliyojaliwa neema nyingi na Mungu imekosa viongozi wa maana. Hivi kweli Tanzania iliyo na wasomi wazuri leo hii inashindwa kutumia raslimali zake kwa maendeleo ya wananchi?? hata kutumia gesi ya asili ambayo tumepewa bure Mungu tunashindwa???

  Viongozi wote wa CCM na serikai yake ni pumbafu tupu!!!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  mshwetani wakubwa
   
Loading...