RAIS KIKWETE ana UJASIRI MKUBWA!!!!!!!!!

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Kikwete asisitiza Serikali kutompiga Dk. Ulimboka



na Mwandishi wetu




RAIS Jakaya Kikwete ameendelea kuyapuuza na kukana madai yanayoihusisha serikali yake na tukio la kutekwa nyara, kuteswa, kupigwa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka.

Akizungumzia suala hilo, alisema ingawa kumekuwa na maneno mengi kuhusu tukio hilo la kikatili dhidi ya Dk. Ulimboka ambayo yataendelea kusemwa, ukweli unabaki pale pale kwamba, kuihusisha serikali ni kuionea.

Akifafanua, Rais Kikwete alisema atashangaa iwapo kutakuwa na mtu ambaye anaweza akajitolea kufanya kitendo cha namna hiyo dhidi ya Ulimboka kwa niaba ya serikali.

“Hizi taarifa za mashaka zitaendelea kuwapo. Habari ziko nyingi na zitaendelea kusemwa. Serikali ifanye hivyo kwa sababu gani? Nitashangaa kwamba eti kuna mtu anaweza akafanya kitendo cha namna hiyo kwa niaba ya serikali,” alisema.

Rais Kikwete ambaye alikuwa akilihutubia taifa kwa kukutana na wahariri Ikulu jijini Dar es Salaam jana, alitoa taarifa hizo baada ya kuwapo kwa taarifa katika vyombo vya habari ambazo zimekuwa zikiwataja baadhi ya maofisa wa juu wa taasisi za kiusalama kuhusika na utekaji nyara na kujeruhiwa kwa Dk. Ulimboka ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.

Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Rais Kikwete kukanusha taarifa zinazoihusisha serikali yake na unyama aliofanyiwa Dk. Ulimboka baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza wakati wa hotuba yake ya mwishoni mwa mwezi Juni.

Akijibu swali kuhusu madai ya madaktari kwamba serikali yake imekuwa ikielekeza vipaumbele vyake katika maeneo mengine na kusahau masilahi ya madaktari na sekta ya afya, Rais Kikwete alisema japo hapendi kujisifu kwa hilo, wamefanya kazi kubwa kuboresha mazingira ya kazi ya madaktari na yale ya mahospitalini.

Alieleza kusikitishwa na kisha akahoji kuhusu madai ya kukosekana kwa mashine ya T scan katika hospitali zote za umma ambayo gharama yake imekuwa ikifananishwa na bei ya gari moja la kisasa aina ya Toyota VX 8.

Akifafanua, Rais Kikwete alisema swali kubwa la kujiuliza ni kwa nini mashine hiyo ya T Scan iliyoko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo thamani yake ni dola za Marekani 700,000 imekuwa ikiharibika mara kwa mara.

“Pale Muhimbili kuna T Scan, swali la kujiuliza ni kwa nini mashine ile imekuwa ikiharibika mara kwa mara hata kusababisha wagonjwa wanaokwenda pale kutakiwa kwenda katika Hospitali ya Regency? Hilo ndilo swali la kujiuliza,” alihoji Rais Kikwete.

Mbali ya hilo, Rais Kikwete alisema serikali imechukua hatua nyingi nyingine za kuboresha mazingira ya kazi katika hospitali nyingi nchini ikiwa ni pamoja na kununua vifaa mbalimbali vya tiba katika hospitali mbalimbali za umma.

“Akutukanaye hakuchagulii tusi. Nimesikia wanasema serikali haijafanya lolote au pengine kuna tatizo la vipaumbele. Hii si kweli hata kidogo….pale Muhimbili leo hii wagonjwa wanaotaka kusafishwa figo wanafanyiwa hivyo wakati awali walikuwa wakitakiwa kwenda Nairobi,” alisema.

Akiizungumzia hospitali hiyo hiyo alisema leo hii kitengo cha mapokezi wanapofikia wagonjwa kwa mara ya kwanza kimeboreshwa kwa kuwa na eneo maalumu la kupumzisha wagonjwa.

Sambamba na hilo, alisema hatua zaidi zilikuwa zimechukuliwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa kuimarishwa kwa kitengo cha meno ambacho hivi sasa kina hadhi ya vile vilivyoko katika hospitali kubwa duniani.

Hakuishia hapo, alikwenda mbele na kueleza kwamba, katika Hospitali ya saratani ya Ocean Road ambako wagonjwa walikuwa wakilala chini, limejengwa jengo jipya ili wagonjwa waweze kulala vizuri wanapoendelea na tiba na kwamba hilo pia limefanyika katika hospitali nyingine mbalimbali nchini.

Akizungumzia kuhusu idadi ya madaktari, Rais Kikwete alisema wakati nchi ilikuwa na madaktari wa magonjwa maalumu (specialists) wasiozidi 50 wakati walipoingia madarakani wamefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba idadi yao inaongezeka na kufikia 500 hivi sasa.
===================================================================================================
Source: Tanzania Daima
===================================================================================================

MYTAKE: Rais J. Kikwete yaani pamoja na serikali yake kuwekwa uchi kwa makala iliyosababisha Gazeti Mwanahalisi kufungiwa, anakuwa shujaa katika kujiaminisha kuendelea kukanusha "Serikali haikumteka na kumtesha Dr. S. Ulimboka????

Kweli ana moyo mgumu sana na usio na aibu.

Kama ni hivyo kwa nini wasimchukulie hatua za kisheria Ndugu Kubenea???? ili ukweli ujulikane???

Wananchi tutaendelea kuilaumu Serikali hadi watakapotuthitishia kuhusu tukio hili.

Kesi ipo mahakamani kwa nini Rais anaendelea kuiongelea suala hili???



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom