MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,038
- 2,224
Nashindwa kuelewa lengo la rais ilikuwa ni nini alipoitikia mchakato wa kuanzisha katiba mpya. Nilidhani ni uelewa umekuwa mzuri na huenda ni mtu anayeona mbali.
Katika hatua hii ya sasa yaonekana wazi kwamba kazi yote iliyofanywa anaiharibu. Mpangilio wa wabunge wa katiba mpya unaonyesha wazi kwamba katiba mpya sasa haihitajiki tena. Hayo ndo yanaonekana na mimi nashindwa kuelewa huyu ni rais wa aina gani aliyeamua kupoteza pesa za nchi kwa mtindo wa aina hii.
Katiba imekufa kwa aina ya wajumbe walioteuliwa. Ni wajumbe ambao wamewekwa kuhakikisha kwamba inakufa. Hiyo ndo inanifanya nimuone rais huyu kama mtu ambaye ni wa ajabu. Mtu asiyeonyesha uzoefu hata baada ya miaka kumi ya utawala.
Ni nini kilichomtokea hadi waunde NGO feki ili kuwaingiza akina Kingunge? Tangu lini mtu huyu akawa ni mtu wa tiba asilia (mganga wa kienyeji)? Ni kwa nini rais alikubali kuingia kwenye njama za aina hii ili kuharibu draft hii ya katiba? Wana CCM wote walioingizwa kwa makundi maalumu walipitia vyama feki vilivyoundwa haraka, rais alifahamu hayo, lengo ikiwa ni kuongeza wingi wa wana CCM. Kama wangekuwa ni wenye niya njema, ni sawa lakini kumbe ni kuhakikisha katiba haipiti! Yeye kama rais anafaidika na nini?
Katibu wa Bunge naye sasa kaja na hoja ya mwenyekiti wa bunge la katiba. Kaweka vigezo ambavyo kila mtu anafahamu huyo ni nani. Awe mwanasheria mzoefu, mzoefu wa shughuli za bunge, n.k. Naona alichoshindwa kusema ni kwamba awe na kipala na mzaliwa wa Bariadi.
Rais, kwa nini pesa hiyo isingetumika kuboresha shule za kata? Kwa wa-TZ wenzangu, lini tutapata viongozi wasiyo na mizaha na maisha yetu?