Rais Joyce Banda amfukuza kazi Mkuu wa Polisi Malawi!

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi mkuu wa polisi Peter Mukhito, kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa na vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali.
Bibi Banda aliapishwa kuwa Rais Jumaamosi baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika wiki iliyopita.

Amekuwa makamu wa Rais tangu mwaka 2009, lakini alikorofishana na Bw Mutharika na kujiondoa kutoka chama chake kinachotawala.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kuondolewa kwa Bw Mukhito, lakini mwandishi wa BBC nchini humo anasema ameshtumiwa kwa uongozi mbaya wakati wa ghasia za kuipinga serikali zilizotokea mwaka jana.

Bw Mutharika, mwenye umri wa miaka 78, alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Alkhamisi iliyopita ingawa kifo chake hakikuthibitishwa mpaka siku ya Jumamosi.

Alitawala Malawi kwa kipindi cha miaka minane lakini hivi karibuni alishtumiwa kwa kufisidi uchumi na kutawala kwa mabavu.

Malawi imekumbwa na ukosefu wa mafuta na fedha za kigeni tangu Uingereza na wahisani wengine kufuta misaada yao.

Mwandishi wa BBC Raphael Tenthani akiwa mjini Blantyre anasema aliyekuwa mkuu wa polisi alianza kupata sifa mbaya mwaka uliopita baada ya kumhoji mhadhiri mmoja kwa kulinganisha vuguvugu la upinzani katika nchi za Tunisia na Misri kuwa sawasawa na mgogoro wa mafuta nchini Malawi.

Tukio hilo hatimaye lilisababisha kufungwa kwa tawi moja la chuo kikuu cha Malawi.
Mnamo mwezi wa Julai mwaka jana ,takriban watu 19 waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali kuhusu uchumi unaozidi kuzorota nchini humo.
Wakati huo huo maafisa wa serikali wanasema matayarisho yanafanywa kurudisha maiti ya Rais Muthariika kutoka Afrika ya Kusini ambako alisafirishwa baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
 
9 Aprili, 2012 | BBC - Swahili

120408080057_malawi_304x171_afp_nocredit.jpg

Rais Joyce Banda amemfukuza kazi mkuu wa Polisi nchini Malawi Peter Mukhito

Sawa sawa kumtimua kazi...........Unadhani hata mi niwe Rais leo..lazima Mwema alambe mchanga tu.
 
Mh! Mbona mapema hivyo? Huyu mama anafaa kuletwaa magogoni atusafishie lile pango la wanyang'anyi.
 
ata jeykei alianza ivyo2 kwa nguvu ya soda,ni mapema kumsifu lets wait en c

Elewa kwamba alishawahi jitoa ktk chama tawala baada ya kuona mambo hayaendi

sasa kapewa lungu unadhani nini kinafuata?

lakini pia usifananishe Raisi wa Tanzania na wa Malawi
 
anatakiwa awaondoe wabaya wake wote fasta. hili siyo la ajabu hata nchi kama nigeria ishafanyika tena kwa kuwanyongelea mbele
 
Rais mpya wa Malawi Bi. Banda amemfuta kazi mkuu wa polisi kutokana na utendaji mbovu na uonevu kwa raia.
Chanzo: BBC
 
siasa za wenzetu nzuri sana. Watu wanathubutu na wanaweza kufanya thubutu zao. Mama kakorofishana na mkuu wake, kaunda chama akiwa makamu na sasa chama chake kinaongoza nchi
 
Elewa kwamba alishawahi jitoa ktk chama tawala baada ya kuona mambo hayaendi

sasa kapewa lungu unadhani nini kinafuata?

lakini pia usifananishe Raisi wa Tanzania na wa Malawi

Kweli siasa mchezo mchafu Bingu wa Muthalika alisifika sana kua amepambana na uovu mpaka wakamtishia kumfukuza uanachama akahama chama leo tunaambiwa kuwa aliteua wanaolinda uovu!
 
Ofcourse anatakiwa pia amtimue mkuu wa majeshi!
UKitaka uraia wa Malawi wee nenda Kyela jifunze kinyaki polepole unajisogeza Karonga bidae ukiiva kwenye kilugha chao unasogea Mzuzu then LIlongwe!
Wakikuuliza kabila unasema wewe Nkonde
 
Back
Top Bottom